Taasisi za Serikali zisizopokea simu za Huduma kwa Wateja…

Taasisi za Serikali zisizopokea simu za Huduma kwa Wateja…

1. Utumishi upande wa ajira.

Kama umekosea kujaza taarifa au ulipakia cheti bila kuthibitisha kwa wakili sasa unataka kubadilisha utapata tabu sana.

Mimi nina degree mbili moja nilisoma UDSM na nyingine Open University of Tanzania sasa taarifa zangu zote zinasoma UDSM kila nikijaribu kurekebisha inashindikana simu hawapokei.

2. NHIF (Bima ya afya).
Kuna siku nimeona tumbo halipo sawa nikaamua kwenda Hospital kupima magonjwa yote yanayohusiana na tumbo.

Si nikaambiwa Typhoid haipo kwenye Bima.

Nikaamua kuwapigia lakini cha kushangaza simu zinaita tu, hata ukiwapigia mwaka mzima.

3. Chuo kikuu Huria cha Tanzania
The Open University of Tanzania
Hasa ofisi ya DVC Academic.
Ukiwa na shida kwenye ofisi hii utapata tabu sana.
 
Baada ya wafanyakazi Nan watafuta?

KATIBA mpya ndo inaandikwa hivyo.
 
Tigo

TIGO ukiwapigia chagua kuongea na mhudumu in English chap wanapokea wanajua mzungu kumbe uko Mbagala, unamaliza, ukipiga kiswahili wanajua wa matopeni basi saa 4 asubuhi unaacha cm inaita unaenda kuoga kisha unavaa nguo na kwenda kula huku unacheki muvi ukimaliza kula ukija saa 10 jioni unakuta bado cm inaita na haijapokelewa!
 
Back
Top Bottom