Taasisi zote makini za kijamii huweka misingi imara ya itikadi zao kuanzia kwa watoto. CHADEMA jifunzeni kwa chipukizi CCM

Kwa siku kadhaa nimeshangazwa na wafuasi wa chama cha Mbowe kushambulia idara ya chipukizi iliyo chini ya UVCCM kana kwamba ni jambo la ajabu sana kuwahi kufanyika. Wanaoshangazwa na uwepo wa chipukizi wanatakiwa kujikumbusha kuwa chipukizi CCM haijaanza leo. Ni idara ambayo ipo kwa miaka mingi kwenye awamu zote. CCM imara inajengwa kwa mambo mengi sana kuliko wafuasi wa Mbowe wanavyodhani.

Taasisi zote za siasa, dini na zingine zote za kijamii zinazohusisha watoto huwa zinakuwa na programs maalum za kuwafundisha watoto itikadi zao na maono ya hizo taasisi. Kwa mfano kanisa la kisabato wana idara za PF na Adventures kwa ajili ya kuwanoa watoto. RC, KKKT, na madhehebu mengine nao wana programs zao kwa ajili ya watoto. Wenzetu waislamu wao wako makini kabisa kwa kuwa na madrasa. Watoto ndo Future ya taasisi hivyo ni muhimu kuwakuza wakielewa mwelekeo wa taasisi. Vyama vya siasa navyo pia hufanya hivyo.

Badala ya kuiongelea Chipukizi CCM ninawashauri CHADEMA wajitafakari na kuangalia namna gani wanaweza kuandaa viongozi wa baadae. Inachosha kila siku tunasikia Mbowe, Lema, Lissu, Sugu, Heche, Msigwa, Mnyika na John Mrema. Ni ngumu kusikia jina jipya limechomoza. Hao BAVICHA hawana makali mbele ya hao mafaza. Yaani hao mafaza ndo BAVICHA pia. Uimara wa chama ni wanachama wake na sio vinginevyo.

Mwisho ninawashauri CHADEMA impe kazi komredi Lucas mwashambwa kuwapa semina BAVICHA ili kuzidi kujiimarisha kisiasa. Mwashambwa ni kijana mzalendo mpenda nchi yake kwahiyo sidhani kama atakataa kuwanoa BAVICHA.
Siyo Kila jambo ni la upinzani...Mimi sijawahi kuwa mwana CHADEMA lakini kama mwana CCM ambaye wazazi wangu ni waanzilishi naona ukakasi kupandikiza unazi Kwa watoto kupitia ideology ya vyama. Tutafute njia Bora za kuwalinda watoto wetu na mambo haya hatarishi ya ideology...Dini zinatosha maana Zina common values. Vyama vina ideologies ambazo hazifanani wengine mabepari wengi wajamaa wengine wameamua kugeuza vyama vyao kuwa vitega uchumi, why corrupt children at a very young age?

Acheni ushabiki maandazi, siku haya mambo yakigeuka ndiyo mtajua kwamba hakuna uovu unaozaa mema
 
Siyo Kila jambo ni la upinzani...Mimi sijawahi kuwa mwana CHADEMA lakini kama mwana CCM ambaye wazazi wangu ni waanzilishi naona ukakasi kupandikoza unazi Kwa watoto kupitia ideology ya vyama. Tutafute njia Bora za kiwalinda watoto wetu na mambo haya hatarishi ya ideology...Dini zinatosha maana Zina common values. Vyama vina ideologies ambazo hazifanani wengine mabepari wengi wajamaa wengine wameamua kugeuza vyama vyao kuwa vitega uchumi, why corrupt children at a very young age?

Acheni ushabiki maandazi, siku haya mambo yakogeuka ndiyo mtajua kwamba hakuna uovu unaozaa mema
Mambo hayako hivyo unavyowaza wewe. Ongea facts sio hisia zako
 
Mtoto hapigi kura
Hana uwezo wa kuchanganua mambo kwa undani
Kumweka mtoto kwenye siasa sio jema kwa watoto wetu
Dkt Dorothy Gwajima
Tupe mwongozo kwa hili
Relax... enjoy the show
 
Kwa siku kadhaa nimeshangazwa na wafuasi wa chama cha Mbowe kushambulia idara ya chipukizi iliyo chini ya UVCCM kana kwamba ni jambo la ajabu sana kuwahi kufanyika. Wanaoshangazwa na uwepo wa chipukizi wanatakiwa kujikumbusha kuwa chipukizi CCM haijaanza leo. Ni idara ambayo ipo kwa miaka mingi kwenye awamu zote. CCM imara inajengwa kwa mambo mengi sana kuliko wafuasi wa Mbowe wanavyodhani.

Taasisi zote za siasa, dini na zingine zote za kijamii zinazohusisha watoto huwa zinakuwa na programs maalum za kuwafundisha watoto itikadi zao na maono ya hizo taasisi. Kwa mfano kanisa la kisabato wana idara za PF na Adventures kwa ajili ya kuwanoa watoto. RC, KKKT, na madhehebu mengine nao wana programs zao kwa ajili ya watoto. Wenzetu waislamu wao wako makini kabisa kwa kuwa na madrasa. Watoto ndo Future ya taasisi hivyo ni muhimu kuwakuza wakielewa mwelekeo wa taasisi. Vyama vya siasa navyo pia hufanya hivyo.

Badala ya kuiongelea Chipukizi CCM ninawashauri CHADEMA wajitafakari na kuangalia namna gani wanaweza kuandaa viongozi wa baadae. Inachosha kila siku tunasikia Mbowe, Lema, Lissu, Sugu, Heche, Msigwa, Mnyika na John Mrema. Ni ngumu kusikia jina jipya limechomoza. Hao BAVICHA hawana makali mbele ya hao mafaza. Yaani hao mafaza ndo BAVICHA pia. Uimara wa chama ni wanachama wake na sio vinginevyo.

Mwisho ninawashauri CHADEMA impe kazi komredi Lucas mwashambwa kuwapa semina BAVICHA ili kuzidi kujiimarisha kisiasa. Mwashambwa ni kijana mzalendo mpenda nchi yake kwahiyo sidhani kama atakataa kuwanoa BAVICHA.
Chipukizi wa CCM ni watoto wa vigogo. Wanawaandaa watoto wao kubeba mikoba. Na mlivyo mazuzu mnawapigia makofi eti wanaandaa chipukizi.
 
Kwa hiyo hao vigogo wameweka watoto wao nchi nzima? Au watoto wa vigogo inawanyima vipi nafasi ya wao kuwa viongozi? Kwani ni wapi katika katiba yetu imekatazwa mtoto wa kiongozi kugombea nafasi ya uongozi? Kwa mawazo yako hayo maana yake leo George Bush pamoja na uhuru Kenyatta wasingekuwa viongozi wa mataifa yao kwa kuwa tu wazazi wao wamewahi kuwa Na Rais siku za nyuma. Kwani wewe nani kakukataza mwanao kugombea uongozi katika ngazi ya aina yoyote ile?
 
Chipukizi wa CCM ni watoto wa vigogo. Wanawaandaa watoto wao kubeba mikoba. Na mlivyo mazuzu mnawapigia makofi eti wanaandaa chipukizi.
Mbona huongelei watoto wa wachezaji wakubwa waliokuja kuwa wachezaji pia? watoto wa wanamuziki walikuja kuwa wanamuziki? Mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi sio dhambi kwasababu ni kama kurithi tu kipaji na hakuna sheria iliyovunjwa. Pia kumbuka kuna viongozi wengi sana nchini ambao labda wangetamani watoto wao kuwa viongozi ila bahati mbaya hao watoto hawana vipaji wala interest na hayo mambo. Unaweza kumweka mtoto wako ashindane na Mtoto kama Qayla Nurdin wa Shetta?
 
Back
Top Bottom