McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Hebu njooni hapa tukumbushane tabia ambazo Watanzania tu tunazo, yaani huzikuti Ulaya wala Marekani, ni hapa Afrika tu
Mimi nina hizi hapa za kwangu wakuu
Hebu njooni hapa tukumbushane tabia ambazo Watanzania tu tunazo, yaani huzikuti Ulaya wala Marekani, ni hapa Afrika tu
Mimi nina hizi hapa za kwangu wakuu
- Umeme ukikata ni LAZIMA utoke nje ili ujue majirani kwao kama upo au haupo
- Ukishakula chakula kwa jirani, lazima uzuge uzuge kidogo ili isionekane umeenda kufuata msosi tu
- Kuhesabu hela baada ya kutoa ATM
- Kupunguza sauti ya TV ili kusikia harufu ya kitu kinachoungua
- Kutunza sahani na vikombe vya udongo kwa ajili ya wageni tu
- Wakati unakula chakula nyama huwa inatunzwa ili iliwe mwishoni
- Kujibu "nakuja" unapoulizwa unaenda wapi?
- Mgeni kujifanya anaangalia pembeni anapoalikwa chakula kujifanya hajaona
- Wagombea kupita bila kupingwa kwenye chaguzi
- Kusema "Nakaribia Kufika" wakati hata hujatoka ndani
- Mtandao unapokata kuweka Airplane Mode ili kurefresh connection
- Sukari na chumvi kuwekwa kwenye kontena za blueband na chocolate zilizotumika
- Viatu kuwekwa chini ya uvungu
- Kupiga piga rimoti kama haifanyi kazi