Tabia ambazo wanazo Watanzania tu, hazipatikani kwingine kokote

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Hebu njooni hapa tukumbushane tabia ambazo Watanzania tu tunazo, yaani huzikuti Ulaya wala Marekani, ni hapa Afrika tu

Mimi nina hizi hapa za kwangu wakuu

  1. Umeme ukikata ni LAZIMA utoke nje ili ujue majirani kwao kama upo au haupo
  2. Ukishakula chakula kwa jirani, lazima uzuge uzuge kidogo ili isionekane umeenda kufuata msosi tu
  3. Kuhesabu hela baada ya kutoa ATM
  4. Kupunguza sauti ya TV ili kusikia harufu ya kitu kinachoungua
  5. Kutunza sahani na vikombe vya udongo kwa ajili ya wageni tu
  6. Wakati unakula chakula nyama huwa inatunzwa ili iliwe mwishoni
  7. Kujibu "nakuja" unapoulizwa unaenda wapi?
  8. Mgeni kujifanya anaangalia pembeni anapoalikwa chakula kujifanya hajaona
  9. Wagombea kupita bila kupingwa kwenye chaguzi
  10. Kusema "Nakaribia Kufika" wakati hata hujatoka ndani
  11. Mtandao unapokata kuweka Airplane Mode ili kurefresh connection
  12. Sukari na chumvi kuwekwa kwenye kontena za blueband na chocolate zilizotumika
  13. Viatu kuwekwa chini ya uvungu
  14. Kupiga piga rimoti kama haifanyi kazi
Ukiangalia kwenye hizi, ni tabia gani ambazo ukikutana nazo tu unajua huyu ni wakwetu nyumbani Tanzania, mjukuu wa Nyerere huyu hapaaaa?? 😂😂
 
Nafika hapo dakika sifuri

Moja ya kauli ambayo sijawahi kuielewa
 
Sisiemu kujichagua wenyewe na kujisifia🤣🤣
Na nyingine wakiona raia ni masikini kusingizia wanaosababisha ni wapinzani 🤣🤣🤣

Ya mwisho hela za budget ya Taifa...aidha imekopwa au imepatikana kwenye kodi kusema ni "fedha za mama..."

Halafu linapokuja deni wanasema la Taifa 🤣🤣 (jokers)
 
  • Blah blah blah blah 100 - 0 Vitendo
  • Wepesi wa kurubuniwa, elfu 10 ya 'bahashishi' inamugharimu miaka 5 ya umasikini zaidi.
  • Wepesi wa kusahau. Baada ya hayo hapo juu, miaka mitano engine anarudia makosa yale yale.
  • Mtanzania wa damu hasa ni mnafiki na msaliti. Atakusifu mbele yako, akipata faragha kidogo anakiponda. Mtapanga pamoja kabla ya utekelezwaji anakuuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…