Tabia hizi mbili za Hayati Magufuli zilifuta Mazuri yake Mengi sana, Watanzania kuna la kujifunza hapa

Tabia hizi mbili za Hayati Magufuli zilifuta Mazuri yake Mengi sana, Watanzania kuna la kujifunza hapa

Alikuwa ni Rais wa HOVYO sana kutokea katika Nchi yetu. Rais anayemiliki kikundi bunafsi cha kuteka, kutesa na kuua maarufu kama WASIOJULIKANA. Tumrudishie Mungu sifa zake kwa kumnyakua maana alikuwa anatupeleka kubaya kiuchumi na kijamii
Utamkumbuka
 
Sema mwamba unaushabiki Sana unauchadema mno binafsi sina huo ushabiki ulionao wewe nashukuru Sana Mungu kwakutokuwa mshabiki wa chama Cha siasa shida unakuwa mtumwa wa kifikra kama wenzako wa matanga hiv huo ushabiki unawasaidia nini?
Huyu CHADEMA wamemuharibu
 
We mwenyeww kuna watu unawakera hapo nyumbani kwako lakini ndio hivyo huwez furahisha kila mtu maisha haya ni kuvumiliana tu ila namlaumu aliepanga njama za kumuua baasi
 
Muacheni marehemu apumzike kwa amani. Marehemu husemwa Kwa mazuri tu. Mabaya ya marehemu yanahitaji huruma ya Mungu kwa kadiri ya mema aliyotenda. RIP JPM
Amani?labda kama yeye mwenyewe ndiye mungu kama mlivyodai.
 
1. Kabla ya JPM watu walikuwa wakiuliwa na hata baada yake bado tunasikia taarifa za watu kuuliwa huko Ngorongoro na kwingine.
2. Uongo ni sifa kuu ya viongozi wetu wote, juzijuzi tu tumesikia kauli ya kiongozi mkuu wa serikali bungeni akisema ngorongoro hali ni shwari lkn siku hiyohiyo tukatangaziwa kifo cha askari mmoja (hapo hatukutangaziwa idadi ya vifo vya raia) kifupi unayomuhumu JPM ndo hayohayo wafanyayo viongozi wetu leo.
3. Kiongozi yupo asiye mbinafis nchi hii? Tena kwangu JPM alikuwa na unafuu kuliko hawa mafisadi wanaojilimbikizia mali na mamilioni ya Watanzania masikini huko ughaibuni.
Wote mnaomshutumu JPM ni wabinafsi kuliko yeye maana yeye alisimamia mali za watanzania ziwanufaishe watanzania wote lkn nyie hamkutaka! Mnataka mvune wachache!
Huyo nae aliletwa na jiwe ndio maana unaona mfanano.
 
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .
Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .
Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .
Hivi mnajua kuwa kadri mnavyoendelea kumwandika zaidi na zaidi JPM mnamfanya kuwa maarufu zaidi kuliko rais Samia mnayetaka kumtetea? Ni afadhali mngetumia muda mwingi zaidi kuelezea mazuri ya Samia badala ya kuandika mabaya ya Hayati Magufuli (Rip).
 
Habar zisizo nanushahidi au za kutunga nadhan haziruhusiwi humu jamvini..mods tafadhali take your position
Wacha ujinga, kwani hii ndiyo thread ya kwanza kumhusisha Mwendazake na ngono kwa wateule wake? Au wewe ni mgeni JF?
 
Hizo assumption zako ni invalid..hata kama marisasi sijui nini bado wangekuwa na Nia mbaya wangehakikisha lengo la kummaliza linatimia...mpaka katika level ya madaktari ..usifanye mchezo na dhamira ya moyo jomba....futa delete kabisa hiyo mawazo
Wewe Babeli Unamtetea sana yule dikteta kwani una nasaba naye? Basi wahi Chato kuchimba kaburi ukazikwe naye karibu
 
Mama Samia hana hizo tabia je Tanzania ipoje sasa? Jk pia hakuwa na hizo tabia nchi alifikishaje? Unajaili vitu vya ovyo ovyo Watanzania wengi wanataka maendeleo bila kujali wana raisi wa aina gani na ndio maana ukimuondoa Mwalimu Nyerere anayefuata kwa kukubalika ni Magufuli hivo vitu ulivyoandika wewe ndio vinaangaliwa na wenye itikadi ya vyama na wanasiasa wenzake ila kwa sisi ambao hatuna itikadi ya vyama tunaangalia utendaji wa mtu na namna anavyofanya maendeleo.
Mbona ndio anasemwa sana ni unaesema kuwa anakubalika? Umetumia mizania gani kubaini ambalo mtazamo wako unaonekana kama nikinyume na uhalisia?

Hivi ujui pia kuwa Mwl Nyerere ndio Rais ambae alipata misukosuko mingi sana kati ya marais wote waliongoza hadi Sasa, au haujui kuwa Mwl ameshawahi kupitia katika majaribio kadhaa ya kupinduliwa? Haya majaribio ya kupinduliwa mara kadhaa ni ishala ya kukubalika....?
 
Habari wana JF, kwenye hii dunia hakuna mtu alie kamilika nna maana kila mtu ana tabia au vijitabia ambavyo watu wengine hawavipendi au vinakufanya mtu kufanya ufanya mambo isivyo.

Hivyo Pia JPM pamoja na mazuri yake yote yanayomfanya aonekana ni Rais bora mpaka alikuwa na tabia mbili kubwa ambao kwa namna moja au nyingine zilimpotezea ubora wake :-
1.Mtu wa Visasi ,kwenye hii Dunia kila siku tunakosana na kutofautiana na watu wengi sana katika Haya wengi husamehe wengine hawawezi hivyo hutulia na kusubiri muda muafaka wa kulipa visasi.

Kiongozi watu aliweza kulipa visasi kwa vikundi mpaka kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja ,kuna watu walikuwa maskini ,Nchi waliiona Chungu kwa sababu za visasi tu ,kwamba nlikuwa sina mamlaka sasa ninao mtakoma ,hii tabia iliharibu sana Nchi na ndio watu walisema ukatili.

2.Hakuwa Muwazi ,Katika Uongozi kuna mambo unaweza waficha wananchi wako lakini Mambo yanayo husu Maendeleo yao ni bora tukajua ,Tulikopa sana ,Tulipewa misaada Mingi ,tulipewa Pesa za COVID-19 ,kuna hela zilikusanya kwa Nguvu zikiwemo za madeni ya Nyuma kutoka kwa Matajiri na watu kama kina Sabaya na kwenda kufanya maendeleo bila watanzania kujua .
Mambo haya yote watanzania ilibidi wajue ,ili hata tunavyo ambiwa Deni la Taifa ni Trilioni 70 tunaelewa sio kuficha Taarifa .
Hivyo watanzania visasi havifai mtu ulikosana nae Darasani ,ukiwa Waziri ,JF ukipata Cheo kikubwa zaidi Tusahau na kusonga mbele .
Lakini mbali na mapungufu hayo makibwa mawili bado JPM ni mfano wa kuigwa kwa wazalendo wote aliipenda sana Tanzania .
Visasi na Kutokuwa Muwazi sio sifa nzuri kwa kiongozi .

Ukitaka kuonekana mbaya dai chako….
 
Mimi nilimshusha tu alipoacha kutupandisha madaraja na kutuongezea mishahara! kwa sababu ya kununua ndege, kujenga flyovers, nk.

Halafu wakati huo huo akapandisha makato ya bodi ya mikopo kutoka 8% mpaka 15%!! Hakika maisha ya watumishi wengi wa umma yalikuwa ni magumu sana wakati wa utawala wake.

Saizi yamekua maraisi??
Mbona bado tunalia
mishahara imepanda lakini kimaisha hamna mabadiliko!!… hela unaipata ukifika sokoni vitu bei kubwa kuliko ela uliyo nayo
 
Wewe Babeli Unamtetea sana yule dikteta kwani una nasaba naye? Basi wahi Chato kuchimba kaburi ukazikwe naye karibu
Hapana tuwe wakweli..mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni..lazima tutende haki inayompasa..tusitende dhambi sisi ya hukumu kama vile sisi ni malaika...nooo..
 
..assumptions zako ndio invalid.

..kwa mfano, unajuaje kama walikuwa na mpango wa kummaliza hospitali ila walichelewa?

..mwisho, nadhani utauliza kwanini ndege iliyompeleka Lissu Nairobi haikutunguliiwa kwasababu uwezo na dhamira walikuwa nayo.
Tuqchane nayo haya madudu watakuja jieleza wenyewe polisi..
 
Mbona ndio anasemwa sana ni unaesema kuwa anakubalika? Umetumia mizania gani kubaini ambalo mtazamo wako unaonekana kama nikinyume na uhalisia?

Hivi ujui pia kuwa Mwl Nyerere ndio Rais ambae alipata misukosuko mingi sana kati ya marais wote waliongoza hadi Sasa, au haujui kuwa Mwl ameshawahi kupitia katika majaribio kadhaa ya kupinduliwa? Haya majaribio ya kupinduliwa mara kadhaa ni ishala ya kukubalika....?
Wewe kwa upeo wako mtu kusema kukubalika unaangalia nini au inamaana gani?
 
Hiyo ya pili nadhani ungesema tu kuwa alikuwa muongo. Maana ukisema hakuwa muwazi maana yake alikuwa anafanya bila kutushirikisha ila yeye alikuwa anafanya hivi sisi anakuja kutuambia kinyume chake
 
Back
Top Bottom