Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Tabia hizi hazina matokeo mazuri, yale unayotarajia upate. Utahisi ukifanya hivyo itakusaidia kumpata mwanamke. Lakini zina matokeo ya tofauti. Zinamfanya asikupende zaidi.
Kwa upande wako utaona kuwa mwanamke hana mpango nawe. Au kila ukianzisha mazungumzo ya mapenzi ye anakwepa. Au utaona majibu yake yanakua ya hovyo kadri siku zinavyozidi kwenda.
Lakini kwa upande wake yeye ni tofauti. Ye anaona hujamsisimua vizuri. Au mwanzoni ulimsisimua lakini sasa umepoteza mvuto kwake. Kwaiyo anafanya kila njia ili awe mbali nawe, au ajitoe kwako. Hivyo ni muhimu kujua hizi tabia na kuziacha haraka.
Kumng’ang’ania.
Mara nyingi sababu una picha fulani ya yeye. Unamuona kama ndo mke wako mtarajiwa. Unamuona ndo wa kujenga naye maisha. Au unaona bila yeye unakosa furaha.
Vyote hivyo ni jinsi unavyofikiri. Lakini sio mwanamke anavyofikiri. Ye anafikiria muende taratibu lakini we una haraka sababu unampenda. Na vitajionesha tu kwenye tabia yako.
Kuna ule msemo, mwanamke akijua unampenda atakutesa. Kiukweli hakutesi kimakusudi. Bali we ndo unajitesa. Kutokana na mawazo juu yake. We ndo unamfanya asiwe na hisia na wewe. Unamfanya ajisikie vibaya.
Cha msingi badilisha unavyomuona/ unavyomchukulia. Usimpe nafasi ya kuwa mke kabla hajastahili.
Na usijiwekee kwamba ye ndo wa pekee. Akilini jiwekee kwamba yeye ndio akung’ang’anie zaidi ya wewe.
Kutomjali kabisa.
Usipomjali atapata wa kumjali. Hata kama alikua anakupenda vipi. Ukimpotezea, na upendo unapotea.
Pia inaweza kutokana kwamba hujui ufanye nini. Kwaiyo unakimbia ili usije ukaonekana dhaifu.
Wivu kupita kiasi.
Kila unapoonesha wivu ujue unamfanya afikirie kuwa mbali nawe. Na kama ndo anataka kutoka nje, ndo kama vile umemuongezea kasi.
Hii inaingiliana na kutokujiamini. Mwenye pesa zaidi atamchukua. Unahisi mwenye mboo kubwa atamchukua. Mrefu zaidi yako atamchukua. Au mtanashati zaidi yako atamchukua.
Hayo mawazo yatajionesha kwenye tabia yako. Utajikuta unamng’ang’aniza awe nawe. Utajikuta unamtafuta kila saa ujue yupo wapi. Na asipopokea simu ni ugomvi mkubwa. Na akilini mwako utakua huna amani na utamuwaza yeye tu. Au muda mwingine utaamua kuachana naye sababu unahisi atakusaliti. Na unapoteza mwanamke anayekufaa sababu ya mawazo yasiyo kweli.
Kubweteka.
Wakati unamtongoza ulikuaje na sasa upoje? Zamani ulikua unamtoa out, sasa hivi je? Au unaona huna muda huo. Unaamua uwe unampa pesa tu, ukiamini pesa ndo kila kitu na itamfanya abaki.
Je, baada ya kuwa naye unaendelea na maisha yako kabla ya kuwa naye? Au ndo umeamua kumfanya namba moja, vingine umeweka kando.
Je, tangu umekua naye mnachati tu kila saa? Hata kama hamna cha maana mnachati tu. Badala ya kukutana na mkafurahi.
Au unaona mna muda mrefu sasa kwaiyo huna haja ya; Kumuongoza tena, Kujiweka fiti kwa kuwa mmezoeana, Kumrekebisha, unatarajia ajirekebishe mwenyewe kimiujiza, Kuanzisha penzi, unasubiri aanzishe na asipoanzisha unaona hakupendi.
Zote hizo ni dalili za kubweteka. Penzi si kama mti kwamba kuna muda ukifikia utapunguza kumwagilia sababu limeshakomaa. Penzi ni kama tumbo la binadamu. Linahitaji kupata kila muda. Haijalishi ni muda kiasi gani mmekaa, hakuna siku inafikia unasema “penzi letu limeshiba/ limestawi”. Kila siku lifanye jipya na ufurahie kuwa na mwanamke. Kila siku una kitu cha kujifunza kuhusu penzi lenu.
Kutojiamini.
Hii ni hali ya kuwa na woga na aibu. Inatokana na unavyojiona mwenyewe. Ukijiona hustahili, itajionesha kwenye tabia pia. Ukiwa naye utakua unajing’atang’ata. Utakosa cha kuongea. Utashindwa kumkiss. Utashindwa kuanzisha penzi. Sababu unaogopa kukataliwa, au unahisi utachukuliwa vibaya
… Kwaiyo unajikuta unatarajia mwanamke ndo aanzishe vitu we ufate. Matokeo yake ye ndo anakua kiongozi. Na sehemu pekee mwanamke anaweza kuongoza mahusiano ni kuelekea kuachana.