Tabia mbaya makondakta daladala za Bunju kuja au kuelekea mjini

Tabia mbaya makondakta daladala za Bunju kuja au kuelekea mjini

Google Diggers

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
944
Reaction score
1,138
Haina haja ya salamu.

Hawa wavaa vibaya na wasema hovyo wanatabia nyingi mbovu. Hapa nielezee kidogo nauli. Wandugu kama hujui bei watakukanyaga watakutoza kiasi wanachotaka wao.

Kabla mafuta hayajapanda Kwa sababu za vita ya Ukraine vs Russia nauli ilikuwa 750 kutoka pande zote za mbali. Hapa naongelea anywhere kwenda au kurudi kwenda mjini.

Nauli ikaenda juu wakapandisha, Kwa sababu Latra hawakutoa muongozo mapema hawa viumbe wali-injoi soko.

Kwanza wakawa wanapiga 1000 Latra wakatoa bei ikawa 850. Sasa ole wako utoe buku wanailamba. Bunju Mwenge 600 ole wako umpe 850 labda awe mtumishi wa Mungu. Lakini hawa wajamaa wanaila.

Mwenge Bunju ni 600 ukiwapa 750 wanakula.

Kwa kifupi Latra wamelala sana.
 
Mkuu wewe si upande gari uende unapoenda. Kila mtu hawezi kuwa vile unapendelea. Jifunze kuishi nao
 
Tukutane sideway kwa jumbe kwa kikao cha dharura! Hawawezi kutuchezea hawa [emoji45]
 
Haina haja ya salamu.
Kwanini hauna haja ya kutusalimia? au unahisi na sisi wana JF ni sehemu ya hao uliokuja kuwalalamikia hapa jukwaani?

Mbona kama vile wewe na hao wasema hovyo hamna tofauti.
 
Bunju - Mwenge ni tshs 700 siyo 600. 600 ni Tegeta -Mwenge. Bunju Ubungo, Morocco, Makumbusho = 850/=. Ukitoa Elfu Moja unarudishiwa 150/.
 
Katika njia ambayo LATRA na wenzao wamechemsha ni njia hiyo ya kuelekea Tegeta, Bunju.

Bunju - Mwenge 600/-
Bunju - Simu 2000: 850/-
Bunju - Makumbusho 850/-
Kibo - Morocco 850/-
Kibo - Mwenge 600/-
Tegeta - Mwenge 600/-

Hii ndiyo haieleweki kabisa, sijui wameoanga nauli mwa kigezo gani;
Tegeta - Kariakoo 700/-
 
Watz wengine wangese Sana tunaongelea jambo la msingi wanaleta ukum*ma
 
Back
Top Bottom