Tabia nilizozishuhudia kwa baadhi ya wanaume wa Dar

Tabia nilizozishuhudia kwa baadhi ya wanaume wa Dar

We subiri kiama. Utashangaa unalowea Dar na kuwa wa Dar. Unadhani wote unawaona wamezaliwa Dar?
Sio rahisi, nina shughuli huku bara ndogo ila nzuri tu ambayo mi ndo bosi wangu. Nitafika kushangaa hivi visa labda kwa wiki, nikiwasimulia huku kuhusu hivi visa wanaona kama nawadanganya, nitakuwa naja nao kuja kutalii, maana hawa wanaume watakuwa kama kivutio cha utalii.
 
Unaonekana kama kuna una bifu binafsi na baadhi ya wanaume wa mjini darisalama ili kupata relief ndo umekuja kujipostia thread ya kimbea mbea ungekuwa rijal kama unavyodai ungebaki huko mkoani ila kwa sababu darisalama kuna madili imebidi uje mwenyewe haya wasalimie huko mkoani kwenu
 
Sio rahisi, nina shughuli huku bara ndogo ila nzuri tu ambayo mi ndo bosi wangu. Nitafika kushangaa hivi visa labda kwa wiki, nikiwasimulia huku kuhusu hivi visa wanaona kama nawadanganya, nitakuwa naja nao kuja kutalii, maana hawa wanaume watakuwa kama kivutio cha utalii.
Tatizo ukifika Dar company yako ni vijiweni. Dar ndiyo Tanzania.
 
Muda wa mwezi mmoja umechunguza yote na kuyaona, Mwenyeji wako alikua na kazi kubwa ya kukuwezesha.
 
Habari za mchana mabibi na mabwana. Nina uhakika leo wengi mpo nyumbani au mmeenda matembezini kujinafasi na hii sikukuu ya Pasaka. Wengine pia mpo kazini mkipiga kazi.

Sio lengo langu kuongea kuhusu watu hasa wanaume, na sisi vijana wa shoka ambao ni wa "mkoani" kama tunavyoitwa na wana Dar slum SIO HULKA YETU ila kwa sababu ni wanaume wa hapa Tanzania, tunaguswa na kushangazwa na mienendo ya wanaume wa Dar slum.

Baada ya kuwepo Dar Slum kwa muda wa mwezi mmoja nikifuatilia dili langu fulani, hatimaye nilifanikiwa na kurudi mkoani.

Ila ukweli ni kwamba nimeshangazwa sana na wanaume wa Dar. Asilimia 90% wana haya yafuatayo ambayo kwa mwanaume wa kawaida rijari kama sie wa mikoani huwezi tukuta na hizi tabia;

Wanaume wa Dar Slum:

1. Wanawake wao wanalalamika hawawaridhishi kitandani,

2. Wengi wanalia lia tu kila wanapoombwa hela na wapenzi wao, eti wanataka usawa,

3. Wengine wamewekwa ndani na wanawake, yaani wanalelewa.

4. Wana vitambi, yaani unakuta kijana mdogo kabisa na ni mwembamba ila kitambi hicho,

5. Wanatinda nyusi,

6. Nao wanaoshwa kucha za miguuni na wanaume wenzao.

7. Wanalia lia hamna kazi ila wanachagua kazi za kufanya,

8. Unakuta jibaba zima liko juu ya miaka 25 ila linakaa kwa baba na mama au bado ni tegemezi,

9. Wako dhaifu sana, hawana tabia ya kufanya mazoezi ya kuimarisha afya, wakivamiwa makwao ni full kukimbia kuomba misaada kwa majirani ambao nao ni wanaume wale wale, kitu ambacho sisi wanaume wa mikoani kama kuna ishu ya mabavu na busara huwa tunaimaliza kishujaa,

10. Wanaogopa kuja MIKOANI ambako ndo kuna hela,

11. Makaka poa wapo kila kona na wanaume wengine wanaona eti ni kawaida kuwa Mungu aliwaumba hivyo,

12. Wavivu, unakuta yupo ktk basi na kuna foleni yeye anaenda sehemu ambayo ni kama mita 300 toka liliposimama basi ktk foleni ila yuko tayari asubiri hata dk 50 ndani ya basi.

13. Wanaume Wenye magari wanatembea na madumu ya mafuta,

14. Wachafu, Ukienda mahali wanapoishi kwa wale walio mabachelor ni kama zizi la ng'ombe,

15. Wanaume wanakojoa kojoa popote tu barabarani kama mbwa,

16. Kwa wale vijana unakuta kavaa suruali kaweka chini ya makalio na anaona ni sawa tu kuonyesha nje nje nguo yake ya ndani tena chafu,

17. Unakuta wanaume wenye familia jioni wamekaa kwenye kahawa na kashata wanaongea umbea,

18. Etc

Kwa kweli nimeshangazwa sana na hawa wanaume wa Dar, hayo ni baadhi ya mapungufu yao, ila yako mengi sana!

Na jiji lenyewe ni KERO. Isiponyesha mvua ni jua kali, joto foleni na vibaka, ikinyesha mvua ni matope, madimbwi ya maji hadi mjini posta.

Kwa kifupi, wanaume wa Dar Slum mjirekebishe, wanaume hatitakiwi kuwa hivyo! Mtuige sisi wa mkoani.
Pia wanapenda Magari ya wanaume wenzao
 
Huu ni ujinga kabisa hivi Dar kuna waenyeji kweli labda watu wabagamoyo mm najua Dar es salaam wote wavamia mji kuna kila aina ya makabila Dar yote asili yao huko mikoani mkuu umejitukana mwenyewe tu eti wanatembea na madumu ya mafuta kwenye gari pumbavu
 
Ni kweli mkuu baadhi ya wanaume wa Dar Wakija mikoani wanapenda kulelewa kwa mfano hapa arusha wanaume wa Dar Wengi Wao wana tabia ya kulelewa na wanawake alafu ni wambea yani kila kitu ukimwambia anasema , mwanau Hawez hata kujishughulisha anamtegemea mwanamke yy anachojua ni mechi ya 6 x 6 na ukikaa vibaya anatembea had na marafiki zako. Hapa arusha wanawake Wengi wanalalamika kuwa wanaume wa Dar wanapenda kulelewa. Na ukiishiwa wanakuacha wanahamia kwa mwanamke mwingine.
 
Mulee muleee

Ila hiyo no.18 kiboko yao
 
Asante, salaam ziwafikie wanaume wote wa Dar slum niliowagusa.
Hujamgusa yeyote wewe mbwiga, badala ya kufanya kazi zako unakaa kuchunguza vitambi vya wanaume wenzio. Aibu kwako kwa kudhalilisha uanaume.
 
Muda wa mwezi mmoja umechunguza yote na kuyaona, Mwenyeji wako alikua na kazi kubwa ya kukuwezesha.
Hamna uchunguzi, cha kufanya usikae nyumbani tu, mambo yako wazi wazi, ni macho yako tu!
 
Back
Top Bottom