Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kuna tabia ya hovyo imezidi kukithiri ya baadhi ya watu tena wengi wao masikini makapuku kabisa kuwakejeli na kuwazodoa watu wanaolalamika baadhi ya watoto na ndugu wa viongozi kujikatia mapande makubwa zaidi ya keki ya taifa(upendeleo). Hawa watu wanasema watu wasikosoe au kulalamikia watoto na ndugu wengine wa viongozi eti kwa sababu wazazi wao walipambana hivyo ni haki yao kujichitotea na kuchuma tu mali, vyeo na pesa za nchi watakavyo.
Hawa watu wanaenda mbali zaidi wakisema walalamikaji wazazi wao walikuwa mafala, wavivu au malofa ambao hawakujituma au kujipanga wakati wao hivyo kila mmoja anakula urefu wa kamba yake. Haya ni mawazo ya hovyo na duni sana, yanayopaswa kulaaniwa na wote wenye akili na wale wanaoipenda nchi. Hii nchi bila kujali kama ni demokrasia au sio demokrasia bado ni jamuhuri na sio ufalme au usultani hivyo watu wote wanatakiwa wapate nafasi na fursa za uongozi wa nchi kwa uwezo wao na ushindani(merits) na sio nasaba zao.