Tabia ya kulalamika hufanywa na watu wazembe na malofa

Naunga mkono hoja
 
Du...Mbona Unalalamika sana. Si utemane nao tu walalamikaji.
 
Kulalamika hakutampeleka mtu kokote zaid zaidi unapunguza baraka na kujiongezea frustration zisizokuwa na maana!
Umesema kweli ndugu yangu. Nimeishi usemi wako hapo juu. Nilipogundua kuwa kulalamika hakunisaidii nikaacha kulalamika. Maisha yangu yalibadilika yakawa bora zaidi tofauti na hapo mwanzo. Ushauri: ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA YA KUBORESHA MAISHA/HALI YAKO.
 
Kuliko kulalamika ni bora tuchukue hatua Tuamue kuzikwa au kusafirishwa,makelele sio mazuri.
 
Ooooh CCM sijui nini, kila siku tunalalamika baada ya kuitoa madarakani....wenye akili wakiona chama hawakielewi wanakitoa madarakani tu....

Oooh mafuta yamepanda bei jamaa wanaitafuna nchi tu, wenzenu hata mkate ukipanda bei tu wanaitoa serikali...huku tunabaki JF tunaandika mashairi tu..
 
Taikon wa fasihi hupoi, huboi, ni full Moto.

👍👍👍
 
Kuna kitu umekiongea kina ukweli. Hata sku moja huwezi kusikia mpanbanaji analalamika ila mvivu anajivika gauni la kuwa yeye ni mnyonge kutia tia huruma ili mambo yalegee bila kufanya jambo.
Dunia haiendi kwa kuomba omba na kulegeza uso machozi mengi na huruma. Dunia inaenda kwa matendo yenye nguvu, ushupavu, kuforce na kujiamini zaidi.
Ili utembee lazima utumie nguvu kama utaonea huruma nguvu zako kwamba zitaisha au miguu yako na magoti vitachoka manake kaa chini usitembee ila kazi ya kutembea ni matumizi ya nguvu sio huruma huruma.
Survival of the fittest and perish of the weakest
 
Na wewe umizaa [emoji28]. Dunia inaendeshwa Kwa sheria ya jino Kwa jino.Yeye akuumize,Wee umeshindwa Nini kumuumiza?
Utatoka lini nje mkuu,daily unachungulia kwa mlango
 
Dunia ikiwa na watu wa aina hii basi hakuna mtu atakayejaribu kufanya ujinga kwa mwenzake na kutakuwa na haki na amani, simple dunia itakalika vizuri zaidi.
Sababu watu watakuwa wanaheshimiana tena kwa lazima.

Kama Tanzania ingekuwa na watu wa aina hiyo basi serikali isingethubutu hata kufikiria kuhusu kupandisha bei chochote sababu wangekuwa wanajua nini kingetokea.
Lakini wanajua watanzania ni watu wa kulalamika tu hivyo serikali itaamua ichukue maamuzi au lah hadi kwenye vitu ambavyo ni lazima uchukue maamuzi fulani.

Kama kila mtu akiwa na uwezo wa kujitetea basi hakutokuwa na wa kumuonea mwengine na hakutokuwa na uonevu.
 
Zingekuwa nguvu ndo kila kitu katika dunia bila akili basi sijui ingekuwaje hapa duniani.......akili nyingi nguvu kidogo ndo mpango.......tuwekee mfano mtanzania gani wewe uliyewahi mshuhudia akitaka kufanikiwa kwa kuonewa huruma.
Hata unavyotype unatumia nguvu na akili...ile kunyanyua mkono tayari kuna nguvu imetumika haijalishi ni kiasi gani
 
Ukiona mtu Anakuletea Jambo linalokunufaisha ujue yeye ananufaika mara Mia zaidi yako. Ukiona hanufaiki ujue huo ni mtego kwako.

Ondokana na hii fikra, kuna watu wengi tu wapo tofauti na huo mtazamo
 
Lawama ni nzuri mdomoni, ila hazitaleta chochote mezani, Watanzania tupende utamaduni wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii, - Hayati Benjamini Mkapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…