Tabia ya kulalamika hufanywa na watu wazembe na malofa

Tabia ya kulalamika hufanywa na watu wazembe na malofa

Binadamu ni social animal. Na kama social animals wengine, kama Mbwa mwitu, simba, sokwe nk. Mbabe ndiye anafaidi. Kama mnyonge hata jike hupati, na hili ni muhimu sana. Sasa hivi karibuni kuna oungo umeenea kuwa binadamu wote ni sawa. Huu uongo ndiyo unafanya watu waone wanaonewa kumbe ndiyo asili yetu.
Naunga mkono hoja
 
Heshima kwenu Wakuu!

Hakuna tabia inakera Kama mtu kulalamika, sasa unalalamika nini, yaani upuuzi tuu!
Kulalamika ni tabia walizonazo wazembe na malofa, kila kitu kulalamika, kila kitu kunung'unika, upuuzi mtupu!

Oooh! Wanasiasa wanapiga Sana hela, Kwa nini nawe usijiingize Huko kwenye siasa? Nani kakukataza?
Nani alikuambia kuna mtu hapa Duniani yupo kwaajili yako kama sio akili yako ya kilofa unayoiendekeza!

Ooh! Wafanyabiashara wanaiba, sijui wanaloga, mara sijui wanahujumu uchumi, Nani kakukataza kuwa mfanyabiashara? Kuwa nawe mfanyabiashara ili uwe na maisha Kama mfanyabiashara. Unalalama Kama Mpumbavu Mpumbavu tuu! Alafu unafikiri utaonewa huruma! Hakuna mtu mwenye akili atakayekuonea huruma Kwa ulofa wako.

Oooh! Nalipwa Mshahara kidunchu, sijui wananinyonya, pumbavu! Ulilazimishwa? Nani kakulazimisha, Acha kazi, ili ufanye vile utakavyo na sio kupangia watu na ulofa wako.
Watu wanaolalamika wanapenda Sana kupangia watu wengine chakufanya, upuuzi tuu!

Oooh! Wanawake wanapenda pesa! Sijui blah! Blah! Sasa si utafute pesa kama unawapenda HAO wanawake, Kama huwezi kutafuta pesa temana nao, fanya mambo mengine, sio kulalamika hapa Kama mpuuzi!
Ulifikiri ukiwalalamikia wanawake watakuona huruma, hakuna Duniani na mbinguni ama mahali popote wanapoonea huruma malofa.

Oooh! Sijui Utawala huu haufai, blah! Blah! Kama haufai si muuondoe? Andamaneni, sio kulia Lia Kama watoto wapumbavu! Watu wenye akili zao, mataifa yaliyoendelea yakigundua Utawala uliopo haueleweki wanautoa madarakani kivyovyote, iwe Kwa Amani au kwa vurugu. Na sio kulalamika Kama malofa au wazembe Fulani.

Oooh! Wanaume wanatutelekezea watoto, sijui hawalei watoto wala kutoa matunzo ya watoto, pumbavu! Si ulee mwenyewe! Hakuna aliyekutuma kuzaa na Masikini ukijua wazi Hana kazi, au kipato chake hakiridhishi, mtu yeyote anayelalamika ubaya ulianzia kwake.
Unalalamika nini sasa ikiwa Kama sio wewe mambo yote yasingetokea.
Mkiambiwa msubiri ndoa hamtaki, mnajifanya nanyi mnatamaa Kama wanaume, mbaya zaidi mnashindwa hata kuchagua mwanaume wa ku-date naye. KAZI kuchagua mashalobaro na Handsome boy, wale wachapakazi wenye Sura ngumu mnawatenga, alafu mkishapata madhara mnalalamika.

Oooh! Ananichukulia mke au mume wangu, ukilalamika haitasaidia kitu. Hii dunia inatumia kanuni ya jino Kwa jino. Apandacho mtu ndicho umpe mavuno yake.
Usijitie mnyonge, usipende kujiona lofalofa, dhaifu wa kuonewa huruma, Duniani hakuna kuoneana huruma. Dunia ni fight for fittest, akichukua mke, nawe chukua wake na Watoto, au nenda mbali zaidi.
Sheria Kwa sheria
Nguvu Kwa nguvu
Pesa Kwa pesa
Uchawi Kwa Uchawi
Mungu Kwa Mungu
Moto Kwa moto
Maji Kwa maji
Hakuna kurembana.

Malofa na wazembe wanaweza wasinielewe, Hilo sitajali, najua ni kawaida yao, wengine wameumbwa kuwa swala na Digidigi mbugani.

Acha kulalamika! Fuata ukitakacho, usisubiri mwingine akuletee kitu kitakachokunufaisha wewe, hakuna Jambo Hilo Duniani na peponi.

Yaani Kwa ulofa wako unakaa kabisa ati unafikiri Jambo linalokunufaisha wewe ati mwingine akuletee! Embu tumia hata akili ya kuku tuu! Hilo haliwezekaniki kamwe.

Ukiona mtu Anakuletea Jambo linalokunufaisha ujue yeye ananufaika mara Mia zaidi yako. Ukiona hanufaiki ujue huo ni mtego kwako. Au ujue tayari wewe ni marehemu wanakupeleka kukuzika, maana maiti ndio hutendewa hivyo. Tena wengine mpaka kwenye maiti hutafuta faida.

Oooh! Mungu nakuomba unipe Baraka! Mpuuzi wewe! Mungu akupe mara ngapi, kuzaliwa tuu ni baraka inayokutosha, unataka baraka gani Kama sio kumchosha Mungu na kukuona lofa.
Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa!

Oooh! Madaktari, sijui mainjinia wanalipwa pesa nyingi, Nani alikukataza kuwa Dokta? Nani alikukataza kuwa Injinia? Nani huyo!
Unalalamika unafikiri itasaidia kitu.

Oooh! Wazungu wanatubagua, sijui waarabu na wahindi wanabagua na kututesa, na wewe watese, Nani kakuzuia! Unajua wanaolalamika wanaakili za kijinga Sana. Mtu anakubagua nawe si umbague, au ndio kutokujielewa kwako ndio kunakufanya uteswe! Acha uteseke ili utie akili!

Taikon nataka kusema nini?
Tambua nafasi yako, usipende kuwamilikisha watu wengine nafasi yako. Alafu uje kulalamika lalamika hapa.

Hata aje kuongoza Mungu hapa Duniani malofa hawataacha kulalamika,
Akizingua mtu mzingue
Akikuheshimu Mheshimu!
Akikupenda mtu mpende!
Hiyo ndio haki na kamwe hautakuwa mtu wa kulalamika lalamika Kama mjinga mjinga!

Taikon nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Du...Mbona Unalalamika sana. Si utemane nao tu walalamikaji.
 
Kulalamika hakutampeleka mtu kokote zaid zaidi unapunguza baraka na kujiongezea frustration zisizokuwa na maana!
Umesema kweli ndugu yangu. Nimeishi usemi wako hapo juu. Nilipogundua kuwa kulalamika hakunisaidii nikaacha kulalamika. Maisha yangu yalibadilika yakawa bora zaidi tofauti na hapo mwanzo. Ushauri: ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA YA KUBORESHA MAISHA/HALI YAKO.
 
Kuliko kulalamika ni bora tuchukue hatua Tuamue kuzikwa au kusafirishwa,makelele sio mazuri.
 
Ooooh CCM sijui nini, kila siku tunalalamika baada ya kuitoa madarakani....wenye akili wakiona chama hawakielewi wanakitoa madarakani tu....

Oooh mafuta yamepanda bei jamaa wanaitafuna nchi tu, wenzenu hata mkate ukipanda bei tu wanaitoa serikali...huku tunabaki JF tunaandika mashairi tu..
 
Kuna kitu umekiongea kina ukweli. Hata sku moja huwezi kusikia mpanbanaji analalamika ila mvivu anajivika gauni la kuwa yeye ni mnyonge kutia tia huruma ili mambo yalegee bila kufanya jambo.
Dunia haiendi kwa kuomba omba na kulegeza uso machozi mengi na huruma. Dunia inaenda kwa matendo yenye nguvu, ushupavu, kuforce na kujiamini zaidi.
Ili utembee lazima utumie nguvu kama utaonea huruma nguvu zako kwamba zitaisha au miguu yako na magoti vitachoka manake kaa chini usitembee ila kazi ya kutembea ni matumizi ya nguvu sio huruma huruma.
Survival of the fittest and perish of the weakest
 
Na wewe umizaa [emoji28]. Dunia inaendeshwa Kwa sheria ya jino Kwa jino.Yeye akuumize,Wee umeshindwa Nini kumuumiza?
Utatoka lini nje mkuu,daily unachungulia kwa mlango
 
Dunia ikiwa na watu wa aina yako basi haitakalika kwa Sababu watu watauishi kama wanyama Mana itakua inaongozwa bila sheria, .Kulalamika ni kawaida Kwa mfano Sasa hivi Tanzania gharama za maisha zimepanda hivo basi lazima watu walalamike ili hiyo hali ilekebishwe.Tatizo unaujuaju mwingi kufikili Kila kitu unakijua na unaweza kukitolea ushauri kitu ambacho sio sahahi.


Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia ikiwa na watu wa aina hii basi hakuna mtu atakayejaribu kufanya ujinga kwa mwenzake na kutakuwa na haki na amani, simple dunia itakalika vizuri zaidi.
Sababu watu watakuwa wanaheshimiana tena kwa lazima.

Kama Tanzania ingekuwa na watu wa aina hiyo basi serikali isingethubutu hata kufikiria kuhusu kupandisha bei chochote sababu wangekuwa wanajua nini kingetokea.
Lakini wanajua watanzania ni watu wa kulalamika tu hivyo serikali itaamua ichukue maamuzi au lah hadi kwenye vitu ambavyo ni lazima uchukue maamuzi fulani.

Kama kila mtu akiwa na uwezo wa kujitetea basi hakutokuwa na wa kumuonea mwengine na hakutokuwa na uonevu.
 
Kuna kitu umekiongea kina ukweli. Hata sku moja huwezi kusikia mpanbanaji analalamika ila mvivu anajivika gauni la kuwa yeye ni mnyonge kutia tia huruma ili mambo yalegee bila kufanya jambo.
Dunia haiendi kwa kuomba omba na kulegeza uso machozi mengi na huruma. Dunia inaenda kwa matendo yenye nguvu, ushupavu, kuforce na kujiamini zaidi.
Ili utembee lazima utumie nguvu kama utaonea huruma nguvu zako kwamba zitaisha au miguu yako na magoti vitachoka manake kaa chini usitembee ila kazi ya kutembea ni matumizi ya nguvu sio huruma huruma.
Survival of the fittest and perish of the weakest
Zingekuwa nguvu ndo kila kitu katika dunia bila akili basi sijui ingekuwaje hapa duniani.......akili nyingi nguvu kidogo ndo mpango.......tuwekee mfano mtanzania gani wewe uliyewahi mshuhudia akitaka kufanikiwa kwa kuonewa huruma.
Hata unavyotype unatumia nguvu na akili...ile kunyanyua mkono tayari kuna nguvu imetumika haijalishi ni kiasi gani
 
Lawama ni nzuri mdomoni, ila hazitaleta chochote mezani, Watanzania tupende utamaduni wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii, - Hayati Benjamini Mkapa
 
Back
Top Bottom