Tabia ya kuomba hela (Kiholela) imekuwa desturi ya Watanzania wengi

Kuna barbershop nilikuwa naenda kunyoa, basi ikawa zile chenji maiti namwachia yule jamaa alikuwa ananinyoa, basi nikaacha kumpa vile vibuku mbili tatu nikashangaa kaanza kuninunia.

kumamake nikawa nikifika pale sitaki tena mazoea nae nikinyoa huyooo nasepa.

kuna watu unaweza wapa hela kwa mapenzi yako ukiacha tu kuwapa wanaanza kukuchukia , binadamu bhana!!!!
 
Tena hakuna watu wenye figisu kama vinyozi.. ole wako uende kunyoa saloon nyingine tofauti na yake, utaona tu anavyokumaind
 
Fact

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Juzi Kuna Mzee wa kimasai nimekaa sehemu anafika ananiambia nimnunulie bia,

Nikamwambia samahani Mzee nimekuja na bajeti ya mtu mmoja tu inayonitosha Mimi.

Jana nakutana nae namsalimia haitikii.

Sasa Leo ,najiandaa kwenda kumtolea uvivu,
 
Watu wa kuwasaidia Hela ni wazazi wako na watu ambao hawana uwezo wa kufanya kazi ( watoto).

Mtu mzima wa afya lazima apige kazi apate Hela.
 
Wewe kama unayo saidi, na kama hauna atasaudiwa na mwingine, haya ni maisha tu, hayajanyooka, kuna mabonde ya ufa pia
 
Waafrika wenzetu huwa wanatushangaa sana kwa tabia hiyo ya ajabu.

Yaani inawashangazaga mno!
 
Maisha kusaidiana kuna Leo na kesho.

Nyie mnaojifanya Miungu watu kumbe ndo wenye shida zimewajaa mpaka matakoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…