meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,832
Ipo Tabia chafu ya baadhi ya wanasiasa kugeuza huduma za tiba na maeneo ya hospitali kuwa sehemu ya kujipatia umaarufu wa kisiasa hususani nyakati hizi za uchaguzi.
Inaeleweka wazi kuwa ukibrand hoja yako na maswala yanayohusu afya,uhai,kifo au huduma za dharura basi jamii lazima itataharuki na kukuonea huruma .Jambo hili linafanya wanasuasa uchwara kukimbilia kwenye maeneo haya ya huduma za afya ili tu waonekane wanajali haki na utu ..kitu ambacho sio kweli.
Kama kweli ulikuwa unajali basi tungekusikia wakati sera ya bima ya afya kwa wote wakati inajadiliwa ungeweka ushauri wako na sio kuitisha wanahabari kutaka kuwachafua wataalamu wa afya.
Wana tasnia ya afya tuwaumbue wanasiasa wote wanaotaka kutumia chaka la huduma za afya kujijenga kisiasa.