Tabia ya kuweka miziki yenye video za nusu uchi kwenye usafiri wa umma ikome

Tabia ya kuweka miziki yenye video za nusu uchi kwenye usafiri wa umma ikome

Kwani sebule yako haichagui cha kuangalia?
Kwani mda wote unashinda nyumbani,anaeshinda nyumbani mda mrefu na watoto ni nani zaidi ya dada wa kazi.
Kwani bongo flavors zaidi ya ngono kipi wanafundisha, na vipindi vyote vya tv wanaigana wakianza miziki ni Chanel zote uweka miziki
 
images (75).jpeg

Haya mambo ukikimbizana nayo utachoka wewe, pambana na wanao wakue kulingana na unavyotaka, Dunia huwezi shindana nayo, Babu zako na bibi zako hao hapo bila maadili. Dunia haina jipya, mzunguko ni ule ule. Miaka ya mbele huenda watoto wa wajukuu zako watakaa na chupi tu saa ya kula sebuleni.
 
Tatizo nyimbo nyingi siku hizi wanavaa nusu uchi, katika nyimbo 10 utakuta 2 tu ndio wamevaa kwa staha
 
Mkuu kiukweli najisikia vibaya sana kila ninapokusudia kusafiri na familia yangu maana siwezi kumzuia 100% mtoto wa miaka saba asiangalie kwenye luninga ya gari.
Hawa watu wanachukulia simple kwa kuwa they don't care
Cha muhimu ni kuwa makini maana , Ngono inaharibu akili ya Binadamu , na Akili ikiharibika unabidi kuzikwa mara moja
 
Kubaliana tu uhalisia. Uko kwenye dunia ya utandawazi. Hivyo hakuna namna nyingine ya kuepuka hiyo hali. Labda uwe unatumia usafiri wamo binafsi.
...So, siku ikija 'Nudist Colony' tukubali TU Kwa Sababu ni Dunia ya Utandawazi?
Mambo mengine Tunapaswa kuweza Kukata.
Mbona ya 'Rangi za Upinde' tumeweza kuyadhibiti?? [emoji35]
 
View attachment 2454211

Haya mambo ukikimbizana nayo utachoka wewe, pambana na wanao wakue kulingana na unavyotaka, Dunia huwezi shindana nayo, Babu zako na bibi zako hao hapo bila maadili. Dunia haina jipya, mzunguko ni ule ule. Miaka ya mbele huenda watoto wa wajukuu zako watakaa na chupi tu saa ya kula sebuleni.
Huwezi kupambana na wanao tu wakati wakiwa nje wanakutana na upumbavu mkuu
 
Kwani mda wote unashinda nyumbani,anaeshinda nyumbani mda mrefu na watoto ni nani zaidi ya dada wa kazi.
Kwani bongo flavors zaidi ya ngono kipi wanafundisha, na vipindi vyote vya tv wanaigana wakianza miziki ni Chanel zote uweka miziki
Sishindi nyumbani na siwezi kusema hawaangalii upumbavu lakini naweka juhudi ya kuhakikisha wanakuwa selective katika wanavyoviangalia
 
...So, siku ikija 'Nudist Colony' tukubali TU Kwa Sababu ni Dunia ya Utandawazi?
Mambo mengine Tunapaswa kuweza Kukata.
Mbona ya 'Rangi za Upinde' tumeweza kuyadhibiti?? [emoji35]
Mtanibishia weehh! Lakini ukweli hata nyinyi mnao mioyoni mwenu. Au mnataka mniambie mkipanda kwenye hayo mabasi, mna ujasiri wa kuwapangia hao wafanyakazi kitu mnachotaka kuangalia?
Maana hata abiria wenzenu watawashangaa!

Dawa pekee ya kuondokana na changamoto za usafiri wa umma, ni kumiliki tu usafiri wako binafsi. Kinyume na hapo, kubali tu kuangalia hizo nyimbo za nusu uchi! Au uangalie filamu za Mkojani mpaka unafika safari yako.
 
Huwezi kupambana na wanao tu wakati wakiwa nje wanakutana na upumbavu mkuu
Dunia huwezi shindana nayo. Pambana na wanao kuwaeleza dunia ilivyo na jinsi ya kusurvive. Maadili yanatengenezwa nyumbani siyo duniani.
 
Shalooom!
Wakuu, nilisafiri kwa basi flani kuelekea mkoani Mtwara ila nilijiskia vibaya sana kuona kila muziki unaochezeshwa kwenye luninga ya gari unaonesha watu walio nusu uchi. Mbaya zaidi nilikuwa na mtoto wa sister naye macho yake yalikuwa yanakodolea kila kinachoendelea. Moyoni nilijisemea "dah hivi huyu dogo hapa anajifunza nini'?

Anyway, madereva wa magari nawashauri mufikirie mnavyotuonesha abiria wenu maana kuna ukakasi flani tunauona kupitia luninga zenu. Msilazimishe haya maungo ya wadada yaonekane ya kawaida mbele ya watoto na wakwe zetu.

Tambueni ya kwamba mnatuharibia maadili ya watoto wetu kwa kiasi kikubwa kutokana na tabia ya kuwaonesha vitu kama hivi mbele ya macho yetu. Naamini zipo video ambazo mkizionesha watu watafurahi na pia hamtowapa huzuni mbele ya watu wanaowaheshimu.

Najua wapo ambao watapinga na kuniona pengine "a primitive guy" ila watambue kuwa usipoziba ufa utajenga ukutaa.
Unaelewa maana ya neno utanda (wazi)
 
Sishindi nyumbani na siwezi kusema hawaangalii upumbavu lakini naweka juhudi ya kuhakikisha wanakuwa selective katika wanavyoviangalia
Na shuleni nako utawazuia? Wakienda kuwatembelea ndungu na jamaa pia utawazuia? Kubali tu tuko kwenye Dunia tofauti kabisa kwa sasa.

Hivyo kuna baadhi ya mambo utatakiwa tu kukubaliana nayo; whether you like, or not.
 
Mnakuwa programmed kufikiri hovyo hovyo bila kujua.
Wabongo mnapenda sana ubishi na malumbano yasiyo na tija. Nani kawa programmed? Mimi naongelea hali halisi ya utandawazi.

Au unataka kusema dunia unayoishi wewe, hukutani na hizo athari za utandawazi?
 
Lengo la miziki hii ya kizazi kipya ni kuibomoa jamii na kuondoa utu wa mwanamke kwa kumfanya bidhaa au jalala la kutupia uchafu. Leo wapo uchi hata bila kuvua
Nakazia hapa.
 
Mtanibishia weehh! Lakini ukweli hata nyinyi mnao mioyoni mwenu. Au mnataka mniambie mkipanda kwenye hayo mabasi, mna ujasiri wa kuwapangia hao wafanyakazi kitu mnachotaka kuangalia?
Maana hata abiria wenzenu watawashangaa!

Dawa pekee ya kuondokana na changamoto za usafiri wa umma, ni kumiliki tu usafiri wako binafsi. Kinyume na hapo, kubali tu kuangalia hizo nyimbo za nusu uchi! Au uangalie filamu za Mkojani mpaka unafika safari yako.
Mkuu hatuna uwezo wa kuwapangia na ndo maana nimewaomba kubadili huo utaratibu wao.
Lakini pia tambua tuna mamlaka kama LATRA ambayo inaweza kuset kanuni na kuondosha haya majambo.
 
Na shuleni nako utawazuia? Wakienda kuwatembelea ndungu na jamaa pia utawazuia? Kubali tu tuko kwenye Dunia tofauti kabisa kwa sasa.

Hivyo kuna baadhi ya mambo utatakiwa tu kukubaliana nayo; whether you like, or not.
Mkuu nilichogundua ni kwamba watanzania tuna hali ya "hakuna jinsi" lakini kama ingekuwa tunaangalia madhara ya hili jambo basi michango mingi ingekuwa ni "tumejikwaa wapi na tunafanya nini"
 
Watoto wa kike karibia wote ni Malaya,,, nashangaa kwnn wanaume wanakaza fuvu kuwa wanapendwa
NB:Mmomonyoko wa maadili umeshamiri kwa watoto wa kike
 
Back
Top Bottom