mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Na ku support ushogaLengo la miziki hii ya kizazi kipya ni kuibomoa jamii na kuondoa utu wa mwanamke kwa kumfanya bidhaa au jalala la kutupia uchafu. Leo wapo uchi hata bila kuvua
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na ku support ushogaLengo la miziki hii ya kizazi kipya ni kuibomoa jamii na kuondoa utu wa mwanamke kwa kumfanya bidhaa au jalala la kutupia uchafu. Leo wapo uchi hata bila kuvua
Bongo fleva inaharibu tu jamiiIla watoto wameharibika mno siku hizi nikivionaga vitoto vya kike vinavyokata viuno huko mtaani utafikiri vikahaba nikionaga hivyo najua tu vimeona kwenye haya manyimbo ya hovyohovyo
Wakome kabisaShalooom!
Wakuu, nilisafiri kwa basi fulani kuelekea mkoani Mtwara ila nilijiskia vibaya sana kuona kila muziki unaochezeshwa kwenye luninga ya gari unaonesha watu walio nusu uchi. Mbaya zaidi nilikuwa na mtoto wa sister naye macho yake yalikuwa yanakodolea kila kinachoendelea. Moyoni nilijisemea "dah hivi huyu dogo hapa anajifunza nini'?
Anyway, madereva wa magari nawashauri mufikirie mnavyotuonesha abiria wenu maana kuna ukakasi fulani tunauona kupitia luninga zenu. Msilazimishe haya maungo ya wadada yaonekane ya kawaida mbele ya watoto na wakwe zetu.
Tambueni ya kwamba mnatuharibia maadili ya watoto wetu kwa kiasi kikubwa kutokana na tabia ya kuwaonesha vitu kama hivi mbele ya macho yetu. Naamini zipo video ambazo mkizionesha watu watafurahi na pia hamtowapa huzuni mbele ya watu wanaowaheshimu.
Najua wapo ambao watapinga na kuniona pengine "a primitive guy" ila watambue kuwa usipoziba ufa utajenga ukutaa.