Hedaru2022
Member
- Mar 26, 2022
- 10
- 15
- Thread starter
- #41
Issue ndugu zangu ni moja hapa, hata kama kweli kuna ulazima wa kuweka ratiba ya usaili Jumamosi, kweli ndio iwe kila Interview ya Mchujo ifanyike Jumamosi? mara nyingi saaaana tarehe ya Usaili wa Mchujo always ni Jumamosi, kwanini hatuoni siku zingine zikijirudia? kwanini wakati wote ni Jumamosi? Kwani hiyo pekee ndio siku ya mapumziko ya mwisho wa Juma?Siku za kazi pia ni shida maana wanaofanya interview na wanaoendesha interview wengine ni wasjiriwa Wana majukumu mengine. Binafsi wasabato hata wakipata kazi ,jumamosi kwao ni shida
Mimi nina ushauri kwa Sekretarieti ya Ajira na Waajiri wengine nashauri mambo mawili kama itawapendeza ili kuweza kuwa neutral :
a) Kupanga tarehe mbili za siku za Interview ya mchujo ili waombaji wapewe uhuru wa kuchagua siku mojawapo ambayo ataweza kuhudhuria , changamoto ni nyingi sana so kuweka option ya siku mbili ni njia bora kabisa.
b) Wakati mwingine kubadilisha/ altenate siku za usaili wa Mchujo kwa kuweka siku zingine za mapumziko ya mwisho wa juma badala kila wakati kuweka Jumamosi ili ongalao na wale wachache ambao wanashindwa kuhudhuria Jumamosi wapate nafasi ya kujaribu wakati usaili unapopangwa kwenye siku nyingine
Kuendelea kupanga usaili za mchujo kila mara siku ya Jumamosi inaweza kuleta hisia kwamba hatuwajali wale ambao wanaabudu ziku ya Jumamosi pengine kwakuwa ni minority ( wachache)