SoC03 Tabia ya uwajibikaji hutengenezwa ndani ya mtu

SoC03 Tabia ya uwajibikaji hutengenezwa ndani ya mtu

Stories of Change - 2023 Competition

dennistheodory

New Member
Joined
Oct 4, 2021
Posts
2
Reaction score
1
TABIA YA UWAJIBIKAJI HUTENGENEZWA NDANI YA MTU

Mara nyingi mtu anapopokea cheo au nafasi flani, kwa zile siku za mwanzo huanza kwa kasi ya ajabu, lakini muda unavozidi kusonga mbele, ile kasi inapungua, kwanini inakuwa hivyo? Kuna sababu nyingi ambazo hupelekea jambo hilo kutokea. Familia zetu zinamchango mkubwa sana katika kutengeneza kizazi cha wawajibikaji.

mfano mdogo tukiwa watoto wadogo baba na mama walikuwa wakitufundisha kubeba majukumu, kila siku asubuhi kabla hawajaenda kazini walikuwa wakiandika majukumu kwa kila mtoto ambayo wanataka wakirudi waone yamekamilika, kila mmoja wetu alipewa kitu chake cha kufanya, na jioni ulitakiwa kutoa mrejesho wa kilichofanyika na ambacho hakijafanyika na kwanini hakikufanyika.

Tabia ya namna hii imetufanya hata katika ukubwa wetu tuendelee kufanya kile ambacho tumekuzwa nacho, na sasa sisi wenyewe ndo tunaumiza kichwa kutafuta nini na nini kifanyike. Sasa kumfanya mtu mzima ambaye hajazoeshwa kuwa mwajibikaji aanze sasa itakuwa ngumu kidogo, lakini itamfanya yeye aanze kufanya ili asimkwaze bosi wake na mambo kama hayo.

Kwaiyo msingi wa uwajibikaji wa mtu yeyote kwanza unaanzia katika familia aliyolelewa, mwingine tu kwasababu hakuishi na mzazi mmoja ilimfanya yeye aanze kuwajibika kumsaidia mzazi aliyepo, na mambo kama hayo.

Mambo ambayo yanawafanya watu kuwa wawajibikaji ni mambo madogo tu yakudharaulika lakini yanamadhara makubwa, ukisoma “1Wathesalonike 3” unaona Paulo kuna mahali anawaambia wajishughulishe na mambibyao wenyewe na sio ya wengine.

Watu wengi siku hizi wanapoteza mda wao kuangalia nani anafanya nini na kwanini, kuongelea watu walifanikiwa, kupiga umbea kutwa nzima, kupoteza muda kwenye Tv n.k. Sasa kama mtu muda wote anafanya hayo, ataanza saa ngapi kuwa mwajibikaji?

Wazazi wanatakiwa waanze kuwazoesha watoto wao kushughulika na mambo madogomadogo, watoto watajua natakiwa kufanya kazi fulani, hivyo ataugawa mda wa kufanya hiyo au hizo kazi na muda wake wakutulia kupumzika, kwa kufanya hivo kizazi cha wawajibikaji kitazaliwa,
 
Upvote 1
Back
Top Bottom