Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

[emoji23] Wewe mpumbavuu umenikumbusha story fulani!

Kuna jamaa angu mmoja ni Mtumishi, aliitwa kwenye ushirika fulani mkoa fulani kufanya semina ya wiki nzima!

Sasa alifika hapo kwenye ushirika saa 5 kama 6 usiku maana safari ilikuwa ndefu kutokea Dar!

Sasa pale ushirikani hiyo siku palikuwa na mkesha! Akaona ngoja niende nikahudhurie mkesha kidogo afu ndo nikampuzike!

Katika ya mkesha maana alikuwa amekaa huku kwenye washirika! Akawa anasinzia Ile anasinzia anashutka!

Kumbe ilikuwa ni katika ya maombi! Kile kikosi kazi sijui kilitokea wapi kikambeba wakihisi jamaa ana mapepo [emoji23]

Si akaanza kugoma anasema "Niachieniiiii Sina mapepooo"

Wazee wakasema umeona mapepo yanaameanza ubishi na ndo wakazidi kumbeba vizuri [emoji23]

Jamaa akasema nilivyoona jamaa hawanielewei ili nibidi niwe Mpole tu

Akabeba mpk mbele. .. asubuhi watu wanashangaa ndio muhubiri na akapawa pongezi kikosi kazi [emoji23]

Ko wewe bisha tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naomba ufahamu hakika kuwa huku kwetu waumini na viongozi wa KKKT hawana tabia hiyo.
Jaribu kuweka wazi umeongelea KKKT usharika gani?
 
Me mwenyewe ni miongoni mwa hao tunaoondoka kabla ya ibada kuisha.
Yani kuna upuuzi mwingi ambao hauna maana,michango ndo usiseme..
Eti ooh sadaka ya kumshukuru mchungaji kwa neno tamu la siku ya leo,najiuliza huyo mchungaji si ndio kazi yake hiyo na analipwa mshahara!
😆Hii ni serious kabisa au umenogesha tu uzi? Ndo leo nasikia sadaka ya namna hii
 
Asante kwa hoja hii, suala la muda linaweza likawa gumu kwa watu wanaoingia ibadani kutimiza wajibu.
Unahudhuria ibada kwa wiki mara moja, alafu unakerwa na matangazo, Neno la Mungu, kwaya, unataka ufanye ibada nusu uondoke!?

Unaondoka ibadani unaishia kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii, kuongea na marafiki, kulala, kuangalia mpira, Movies, tamthilia, kukaa vijiwe vya kahawa, kukaa kwenye mahoteli.

Kurudiwa matangazo naona sio Jambo baya, huo ni mkazo, kwenye ma TV, ma radio, tunaona tangazo moja linarudiwa kwa siku mara nyingi, mengine yanaenda MIEZI ya kutosha.

Tunapaswa kujiuliza kwanini tunakereka kwa mambo ya ibada, nini kimetukuta, kwanini tusione Jambo jema kukaa kanisani siku ya ibada hasa jumapili?

Muhimu hapa ni kila kitu kwenda kwa utaratibu na mpangilio mzuri, kama vitu havina mpangilio mzuri hapo tuna haja ya kushauri. Wapo wazee wa kanisa au mashemasi kuwafikishia ujumbe wa maboresho vile tunaona inafaa. Tukiona hao hawatafikisha kwa usahihi tuombe kuonana na wachungaji/maaskofu.

Asante
Kila kitu kina kiasi, hata hayo matangazo ya kwenye luninga hayarudiwi kwa mfululizo hupita muda ndipo lirudiwe tena,
 
Misaa masaa zaidi ya 3 mnafanya nini humo ndani, kama ni matangazo ndio yanawakalisha muda wote huo basi kuna tatizo la kutumia muda vizuri.
Ni kheri muda upotee kwenye mahubiri ila sio matangazo.

Na ninyi si huwa mna jumuiya ndogondogo, sasa inakuaje mnakua na matangazo mengi?? Uongozi unakutana na viongozi wa hizo jumuia wanapewa matanga, o wanaenda kuwaelewesha waumini, ikifika jumapili basi maelekezo yanakua sio mengi.
 
Back
Top Bottom