Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Katika maisha au kazi, tofauti na elimu ya darasani ambayo ndio wengi huitumia kama kigezo yatupasa kujua kuna kitu kinaitwa Skill. Kila mtu amepewa kwa kadiri ya karama yake, changamoto huwa ni jinsi ya ku identify. Makazini asilimia kubwa wenye skills zifuatazo huwa ni ngumu kujikomba; Integrity; Communication skills; team working; business acumen (good judgement and quick decision); experience; qualifications; self confidence.

Asilimia kubwa ya wanaojipendekeza wengi wana lack mengi ya hivo, na haya mambo hushamiri sana kwenye ofisi na makampuni ya kibongo. Huwezi kuta huu ujinga wa kujipendekeza kwa wenzetu wazungu maana kwao wanajali sana muda na performance basi. Wao wana deal na wewe mwajiriwa kwa target basi, ukishindwa kudeliver basi off you go pasipo kinyongo.

Na ndiko watu wanapiga mzigo hasa, Ofc za kibongo ukiwa mpambanaji sana na unatimiza wajibu wako tayari unaonekana ni tatizo, hatari kwa watu, basi majungu ni mengi sana.

From experience, kuna tofauti kubwa sana katika utendaji kazi baina ya Ofc za kibongo na wenzetu. Wengi umbeya kwao ni skill ilhali wengine kwao sio
 
Mimi tabia yangu ya Kutopenda Unafiki, Ujinga, Utoto, Upuuzi, Upumbavu, Kujikomba na Kuongopa imenifanya nichukiwe sana kuliko hata Shetani.
Umenisema mkuu, staff kwetu sipendwi kabisa kwa sbb km hizo, sijui kwanini wabongo tuko hivi.
 
Kuna mtu bidada aliniambia anafanyaga huo UPUUZI wa kujipendekeza kwa Boss kufikia hadi kuleta zawadi mbali mbali na kunishauri eti bami niuanze.

Nikamwambia I have too much PRIDE to lower my standards to that level, but if you are comfortable doing that all powers to you.

Urafiki ukapungua sana na hata kunitafuta akaacha. Mie nachapa kazi tu vile inavyostahili lakini mambo sijui ya kujikomba kupeleka zawadi etc siwezi kuyafanya wala SITAKI kuyafanya.

 
Mimi tabia yangu ya Kutopenda Unafiki, Ujinga, Utoto, Upuuzi, Upumbavu, Kujikomba na Kuongopa imenifanya nichukiwe sana kuliko hata Shetani.
Tatizo lako wewe umekosa BUSARA humu.

Ishu ndogo TU ya kumwelewesha mtu,

Solution yake wee unaona Ni kumchamba mtu,

Unaporomosha mvua ya mitusi ya nguoni mpk watu wanahama kwny mada ya Uzi husika.

[emoji3525]NANI ANAKOSA KUKUCHUKIA KWA MAMBO HAYO YA KI-ASHA NGEDELE HUMU NDANI.
 
Daai eti ukute nacheka cheka huku naitikia sawa!
hii ni kitu sina mura, mara nyingi ntanyamaza kusikiliza kama ni point au pamba ili nikosoe au kufanyia kazi full stop
 
Maisha bila unafki hayaendi
 
Huu Uzi Nadhan watumishi wa serikali hasa hasa walimu Ni Bora mkae tu kimya.

Miaka 5 Sasa hamjaongezwa mshahara, ila kila MEI MOSI mnamshangilia na kumpigia makofi.

Wakati wa Uchaguzi, nyie ndo vinara wa kuhakikisha liwalo na liwe bao la mkono lazima lifungwe.
Bila hata Aya, Wengi wenu mna kadi za chama.

Mbaya Zaid,
Juz juzi kawaambia mridhike na vyeo vyenu.

Kisha yeye akaenda kuchukua fomu ya peke ake
Wala hamjalalamika, mmeishia TU kumsifia kinafiki.

Mkajitutumua angalau kuonyesha Nia,
Ujira wenu hajawalipa,wengine mmefutwa kabisa.
Wala hamjalalamika,mmeishia TU kumsifia kinafiki

AFU MNAKUJA HUMU,
Mmejificha nyuma ya Keyboard, Mnasema mnachukia kujipendekeza.

ACHENI UNAFIKI WATUMISHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…