Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Daa pole sana boss pambana ujiajiri,kuna mshikaji wangu alipiga chini u lab manager kwa sababu ya majungu

California love
 
yani mkuu umenigusa kabisa, mbaya zaidi Mimi nilikua mchapakazi Sana wakati naajiriwa, kwaiyo niiawa natokea kupendwa na mabosi bila jitihada kubwa, lakini Sasa hivi vimbilimbili ambavyo havijui kazi vinajua kujipendekeza tu ndio shida inapoanzia, Mana unamkuta mtu kazini unapiga mzigo kivyako anaona Kama unachukua nafasi yake vile, Kama unamfunika flani.
Dah kazi zote nilizoajiriwa isipokua moja- tu niliondoka kwa fitna za wajumbe, kazi ya mwisho nilikua na gari Fulani ya pfisi natumia ila weekend napaki natumia tu katikati ya wiki, j3 moja- naingia job nikachkua ndinga nikaisogeza kidogo tu nikajua Ina shida nikatoa taarifa kwa Kila mtu na kuuliza kwamba Nani katumia weekend, sikupata ushirikina mzuri ila baadae nilimbaini huyo mjumbe, kiufupi gari ilibidi ikae gereji siku tatu, na ikaonekana Mimi ni mzembe pamoja na kajitetea kote kumbe wadau walishapeleka maneno kwamba gari siijali halafu natoka nayo weekend. Nikajikataa nikawaachia kazi yao, ndani ya mwaka mmoja hakuna hata mjumbe mmoja alibaki kwenye ile kampuni, walitolewa wote. Mwisho nikajigundua Sina nyota ya ajira tu
 
kujipendekeza na kujikomba ni vitu ambacho nimefeli kwa kweli, ila kuwa friendly ni kitu ambacho kiasili nipo hivyo hivyo nimejikuta nina marafiki wengi sababu ya kuwa muwazi, kitu kinachosababisha wengi wanifate na kuniomba ushauri au kunikosoa pale napoyumba.

ila chuki makazini huwa zina sababu nyingi kuna jamaa yangu ye kazi anapiga fresh tu ila maboss wanamchukia kinoma sababu jamaa havungi akiona pisi kali kiasi kwamba kuna muda anapita na usingizi wa maboss zake
 
Hata mimi nimeona, kuna tofauti ya kumheshimu boss na kujipendekeza kwa boss, huyu jamaa anazarau either kwa kujiona ana elimu kubwa au sawa na boss wake.

Katika maisha mtu unatakiwa kuwa na heshima na sikujipendekeza kwa msimamizi wako au mkuu wako haijalishi unamzidi elimu au anakuzidi.
 
They didn't tell you the truth. Utendaji kazi wako uko below average. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali kumpoteza mfanyakazi jembe kisa hajipendekezi.
 
They didn't tell you the truth. Utendaji kazi wako uko below average. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali kumpoteza mfanyakazi jembe kisa hajipendekezi.
hujawajua maboss wa kibongo, eneo la kazi anakuwa na nyoka wake wawili hadi watatu wa kumpa udaku na umbea, hata akiwa hayupo nakuhakikishia atajua deep down ya kila jambo(kiofisi na yasiyo ya kiofisi!) hapo ndipo utakaposhangaa huyu jamaa anapata wapi taarifa!
 
Huu ni ushauri bora kabisa. Fuata ushauri huu
 
Mkuu ukifika kazini fanya kilichokupeleka, habari za kusabahi ni nje huko baada ya muda wa kazi. Mambo ya kusabahi watu ofisini ndio kujipendekeza kwenyewe. Unashindwa kutulia sehemu yako ya kazi unazunguka kusalimia watu, kama sio kujipendekeza ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…