Trinity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2017
- 1,828
- 3,508
Au sio.!mkuu huwezi ishi mjini bila kujipendekeza ikiwa unajua kabisa huna wa kushika mkono.kujiendekeza ni nguzo muhimu tena kwa malengo
Sawa nimekupata ni jambo jema pia.!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Au sio.!mkuu huwezi ishi mjini bila kujipendekeza ikiwa unajua kabisa huna wa kushika mkono.kujiendekeza ni nguzo muhimu tena kwa malengo
Unamaanisha kila member wa Jf amekomenti kwenye huu uzi?Kila mtu hapa kasema kujipendekeza hawezi now nani anaweza? Ila jf bwana
Sawa pachaKaribu Pacha.
Nitumie Siivii inbobo
Usipende mambo marahisi mkuu, gharama yake ni kubwa sana.Lakini wanaojipendekeza na kujipitisha huwa wanatusua kirahisi sana aisee natamani ningejaaliwa hicho kipaji
Ulishawahi kujaribu? Mimi naona maisha huwa yanakuwa mepesi sanaUsipende mambo marahisi mkuu, gharama yake ni kubwa sana.
yani mkuu umenigusa kabisa, mbaya zaidi Mimi nilikua mchapakazi Sana wakati naajiriwa, kwaiyo niiawa natokea kupendwa na mabosi bila jitihada kubwa, lakini Sasa hivi vimbilimbili ambavyo havijui kazi vinajua kujipendekeza tu ndio shida inapoanzia, Mana unamkuta mtu kazini unapiga mzigo kivyako anaona Kama unachukua nafasi yake vile, Kama unamfunika flani.Kama kawaida baada ya kumaliza chuo nikaingia mtaani kusota na maisha bahati nzuri nikapata intern kwenye moja ya taasisi za serikali zinazolipa vizuri.
Changamoto ikawa kumbe kwenye taasisi hizi za serikali inatakiwa ufanye kazi kwa bidii bila kusahau kujipendekeza kwa boss.Kwa jinsi nilivyo tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza wala kufitini wafanyakazi wenzagu mm nikawa natimiza Majukumu kama kawaida.
Kumbe ilitakiwa niwe naenda hata kumuona boss personly angalau mara moja kwa wiki kumsalimia tu ambavyo wengine hufanya sasa mm nawaza nikamuone manager nimweleze nini Cha zaidi wakati meeting za Kila wiki tunakutana na kila mtu anawasilisha ripoti yake?.
Basi bwana boss akaanza kulalamika ooh sina msaada kwenye office ikabidi nifuatilie kujua ninakwama wapi bassi wadau wakanitonya jipendekeze nenda hata mara moja peleka umbea wowote ule atakukubali tu.
Asikwambie mtu hakuna kazi ngumu Kama kuwa mmbeya eneo la kazi Kama hauna tabia hiyo.
Mm nikasema potelea mbali ilimradi natimiza Majukumu yangu na nipo qualified siwezi kujipendekeza kwenye ofsi hii nitapata kazi hata kwingine.
Mkataba wa intern ukaisha boss Kama kawaida akaaniambia nitafute kazi sehemu nyingine.
Mwamba nikaona siyo kesi nikaingia mtaani nikapata kazi kampuni nyingine ya kibongo aisee kule ndo ikawa balaa bila kuwa mbeya humalizi mwezi unatimuliwa boss anataka kila siku mpishane na wafanyakazi ili apate taarifa mara huyu kapeleka fulani mwizi kaiba mafuta, kifusi.
Daah nikaona pia isiwe kesi nikaacha kazi.Sasa Nina mwaka nasota mtaani nimezunguka kinoma hamna kazi kila Kona patupu wadau wanashauri tafuta hata viongozi wa kisiasa ujipendekeze kazi siku hizi kujuana mm naona wananisumbua tu.
Natafuta kazi nikiamini qualifications zangu zitanibeba lakini patupu nimeapply sehemu nyingi hata kuitwa hakuna.
Nikatafuta mpaka sehemu za vibarua patupu. Sasa nawaza hii tabia ya kutojipendekeza nitaachaa vipi maana kubadili tabia ni ngumu kama kubadili ngozi.
Upi huo my dearKuna ushauri wako nimeufuata umenisaidia.
hujawajua maboss wa kibongo, eneo la kazi anakuwa na nyoka wake wawili hadi watatu wa kumpa udaku na umbea, hata akiwa hayupo nakuhakikishia atajua deep down ya kila jambo(kiofisi na yasiyo ya kiofisi!) hapo ndipo utakaposhangaa huyu jamaa anapata wapi taarifa!They didn't tell you the truth. Utendaji kazi wako uko below average. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali kumpoteza mfanyakazi jembe kisa hajipendekezi.
Hujaliwa papuch kwa kujipendekeza?Yaan kama unanisemelea Mimi
Hiki ndo kipo ofisin kwetu, usipojipendekeza unapigwa chini
Kama mpaka Sasa hivi bado upo kwenye hiyo ofisi basi na wewe unajua kujipendekeza!Yaan kama unanisemelea Mimi
Hiki ndo kipo ofisin kwetu, usipojipendekeza unapigwa chini
Huu ni ushauri bora kabisa. Fuata ushauri huuUsiogope na usijali. Kaa ukijua wema na uaminifu unalipa sana. Pia kumbuka giza na nuru haviishi sehemu moja lazima nuru italiangamiza giza.
Brother, utapata kazi nzuri sana ambayo hukuwahi kuiwaza kabisa maana ni aina ya kazi ambayo ndio ndoto ya watu wengi.
Mungu akusimamie katika kila jambo.
Mkuu ukifika kazini fanya kilichokupeleka, habari za kusabahi ni nje huko baada ya muda wa kazi. Mambo ya kusabahi watu ofisini ndio kujipendekeza kwenyewe. Unashindwa kutulia sehemu yako ya kazi unazunguka kusalimia watu, kama sio kujipendekeza ni nini?Kitu pekee ntakua mdogo na mnyenyekevu kuliko maelezo ni pale nimekamatwa na mke wa mtu..vinginevyo kwenye mambo ya kazi hapana kabisa kuendekeza kujipendekeza.
Mtu umeacha kazi zako na kwa nia njema umeenda kusabahi tu, anashindwa hata kuthamini akatumia lugha ya staha kukufukuza badala ya kuwa muungwana?
Niliwahi kuacha kazi sehem kwa mambo haya haya.