Tabiri Top 4 yako VPL

Tabiri Top 4 yako VPL

Yanga kwasasa changamoto zake si vikombe vya Tanzania, Hakuna kikombe chochote apa nchini kinacho simamiwa na Tff ambacho Yanga haongozi kwa kukichukua. Changamoto za Yanga ni kimataifa apa ndani Simba ndio wanatakiwa kupambana kufikia mafanikio ya Yanga.

Out of topic
 
Out of topic
Maana yangu, Yanga kuchukua ubingwa au ngao ya jamii sio ishu, Mimi nimeishuhudia Yanga ikichukua Mataji mengi ya apa ndani. Mimi binafsi kusikia Yanga bingwa kwa kikombe chochote Cha apa ndani si shtuki Tena. Ningependelea Yanga indelee kujengwa kitaalamu kwa ajili ya kupambana Afrika. Aya mambo ya ubingwa wa Tanzania kwa Yanga ni kwaajili ya heshmaya mashabiki wetu.lakini Lengo liwe mashindano ya Caf Uko ndio kwenye changamoto halisi.
 
Washabiki wengi wa Simba wanajitahidi sana kujiaminisha kuwa Azam ipo juu ya Yanga, wakati si kweli. Ukiangalia mechi yao na Prisons jana na mechi yao na Namungo, utagundua Azam ni ileile ya msimu uliopita.

Yanga ime -improve. Sarpong ni mwepesi na ana qualities za ukubwa wa Molinga na Yikpe ila amewazidi speed sana ingawa sidhani kama amefikia ya Makambo. Ila kama midfield ya Yanga ikipata chemistry nadhani kutakua na shughuli pevu zaidi ya mwaka jana.

Namungo, hapana. Haitakuwa top 4
 
Kama ubingwa siyo ishu kwanini mnashiriki ligi ?utaendaje kimataifa wakati siyo bingwa au huna kombe ?ndo maana kocha aliyeondoka aliwaita ile jina
Maana Yangu, Yanga kuchukua ubingwa au ngao ya jamii sio ishu, Mimi nimeishuhudia Yanga ikichukua Mataji mengi ya apa ndani. Mimi binafsi kusikia Yanga bingwa kwa kikombe chochote Cha apa ndani si shtuki Tena. Ninge pendelea Yanga indelee kujengwa kitaalamu kwa ajili ya kupambana Afrika. Aya mambo ya ubingwa wa Tanzania kwa Yanga ni kwaajili ya heshmaya mashabiki wetu.lakini Lengo liwe mashindano ya Caf Uko ndio kwenye changamoto halisi.
 
Baada ya mechi ya ngao ya jamii kupigwa, ni kiashiria tosha kuwa ligi inakaribia kuanza.

Timu zimejiandaa vizuri, kuanzia kwenye usajili wa vikosi vyao mpaka kwenye benchi la ufundi.

Huu ni msimu ambao timu kama Yanga imejiandaa kweli hasa kwenye usajili wa wachezaji wa kimataifa kama vile Mukoko na wengineo, lengo ikiwa ni kufuta ufalme wa Simba, huku Simba nayo ikijiimalisha vya kutosha kama maingizo mapya ya akina Bwalya na Onyango. Azam Fc inakimbiza mwizi kimya kimya, KMC wapi kama hawapo, Namungo ndio kama hivyo ina kikosi kizuri chenye morali. Bila kuwasahau timu kama Polisi Tanzania, Ihefu, Kagera na Mtibwa Sugar.

Tabiri nani atakuwa bingwa na top 4 kwa ujumla.

Kwangu mimi, Bingwa ni Simba Sc kwa mara nyingine. Top 4 yangu ni hii;
1. Simba Sc
2. Azam Fc
3. Yanga Sc
4. Namungo

Karibu na wewe uweke utabiri wako...
Naunga mkono
 
GSM imewasajilia Yanga matatizo kwani ujue mishahara ndio litakuwa tatizo kubwa kwa Yanga.Hela za mishahara watakosa na wachezaji hawataonyesha kiwango
1.Simba
2.Azam
3.Namungo
4.Police Tanzania

Yanga bado inaendeshwa kiswahili sana kama ianze kuimarika kama taasisi itachukua kama miaka 3 na approach ya GSM ya kuwanunulia wachezaji na kuwanunulia wasemaji au wahasishaji wa Timu unaendelea kuibomoa Yanga.

Angalia suala dogo tu kama msemaji wa Timu pale Yanga ni vurugu.Kuna Bumbuli, Baba Levo, Antonio Nugaz na wote hawajui kazi yao. Mwakalebela au Msola ukimuuliza mishahara GSM walikubaliana shs ngapi kwa mwezi hata hawajui na huyo Senzo hana kazi hapo
5.Yanga
Kwa hiyo?!?!
 
Washabiki wengi wa Simba wanajitahidi sana kujiaminisha kuwa Azam ipo juu ya Yanga, wakati si kweli. Ukiangalia mechi yao na Prisons jana na mechi yao na Namungo, utagundua Azam ni ileile ya msimu uliopita.

Yanga ime -improve. Sarpong ni mwepesi na ana qualities za ukubwa wa Molinga na Yikpe ila amewazidi speed sana ingawa sidhani kama amefikia ya Makambo. Ila kama midfield ya Yanga ikipata chemistry nadhani kutakua na shughuli pevu zaidi ya mwaka jana.

Namungo, hapana. Haitakuwa top 4
Sio kila unachokiamini na wengine wakiamini.
 
Back
Top Bottom