Tabora: Atapeliwa saa ya Milioni 1 na mganga wa kienyeji

Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora, ametapeliwa na kuporwa saa yenye thamani ya shilingi milioni moja baada ya kudanganywa na mganga wa kienyeji mjini Sumbawanga kuwa atapata utajiri wa haraka.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.

Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.

#EastAfricaRadioView attachment 3270549
Angeenda Katanga kama alikuwa anataka utajiri.
Kule wanatoa kila siku
 
Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri. View attachment 3270549
😂😂😂😂 👆
 
Yaani mkuu wa wilaya anathibitisha tukio hili. Kweli Mkuu wa wilaya hana shughuli za maana na hadhi yake za kumuhusisha nazo? Kuna siku kijana atakufa kwa kupiga punyeto, na mkuu wa wilaya atathibitisha tukio hilo na kututaka wananchi tujiepushe na upigaji wa punyeto.
Kwani wakuu wa wilaya wana kazi gani Mkuu,wale ndio kazi zao hizo,kudandia mambo tofauti wilayani
 
Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora, ametapeliwa na kuporwa saa yenye thamani ya shilingi milioni moja baada ya kudanganywa na mganga wa kienyeji mjini Sumbawanga kuwa atapata utajiri wa haraka.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.

Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.

#EastAfricaRadioView attachment 3270549
Hao wananchi wajinga kabisa wee umemkuta makuburini sii ndio fursa hiyo ya kumla yas🤣🤣🤣🤣
 
Hiyo dawa inaanza kufanyakazi baada ya saa 17, amefanya haraka ona sasa ameizimua haifai tena.
 
Yaani mkuu wa wilaya anathibitisha tukio hili. Kweli Mkuu wa wilaya hana shughuli za maana na hadhi yake za kumuhusisha nazo? Kuna siku kijana atakufa kwa kupiga punyeto, na mkuu wa wilaya atathibitisha tukio hilo na kututaka wananchi tujiepushe na upigaji wa punyeto.
Ndo utaelewa aina ya wateuliwa.
 
Back
Top Bottom