Tabora: Atapeliwa saa ya Milioni 1 na mganga wa kienyeji

Yaani kuna watu wanaamini utajiri wa hivyo unaupata kwa kulala makaburini
Ujana wake alikuwa wapi?
Anahangaika sasa na kutafuta utajiri kwa waganga
Huwa siwahurumii wajinga wa hivyo

Kwenye shamba la familia kulikuwa na miti mingi ila kulikuwa na mti mmoja mkubwa sana
Kwa haraka haraka ukiuangalia utaona ni mti wenye umri wa zaidi ya miaka mia 2 au zaidi
Sasa hapo huwa kila wakati tukiwa tunazunguka kuchuma matunda unakuta nyembe na vikaratasi vidogo vidogo na maji yaliyokauka

Ila panaonekana kama aliogeshwa mtu
Ila bado unaona umasikini tu kwa watu

Wapeni elimu sana kuwa hela za hivyo hazipo
Wajinga hawaishi tangu enzi na enzi.. Imagine tangu enzi za pyramid schemes. Ponze mpaka DECI lakini mpaka leo bado wanapatikana wa kupigwa
 
Hao itakuwa ni wale vijana wa tuma hela kwanamba hii

Maana Sumbawanga wapo wengi saaana 😄😄😄
 
Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora, ametapeliwa na kuporwa saa yenye thamani ya shilingi milioni moja baada ya kudanganywa na mganga wa kienyeji mjini Sumbawanga kuwa atapata utajiri wa haraka.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.

Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.

#EastAfricaRadioView attachment 3270549
Hana akili, tayari alikua na saa ya milioni halafu anaenda kwa mganga kutafuta utajiri
 
Zingatia haya maneno......Baada👉🏿👉🏿👉🏿 ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa.
🤣🤣🤣..Bro, unataka kusisitiza nini hapo ? ..
🏃‍➡️🏃‍➡️🏃‍➡️
 
Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora, ametapeliwa na kuporwa saa yenye thamani ya shilingi milioni moja baada ya kudanganywa na mganga wa kienyeji mjini Sumbawanga kuwa atapata utajiri wa haraka.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.

Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.

#EastAfricaRadioView attachment 3270549
Elimu elimu elimu
 
Huyo mmzee alivyonyoa tuu nae nitapeli sema kakutana na watoto wa mboka mana wale kwa utapeli ndo wenyewe sasa. Itakua alienda kuoga dawa ili alio watapeli huko atokako wasimtafute. sasa kakutana na wenye kazi yao
 
Baada ya kuona uchawa haulipi umeamua kuwa mkulima wa mboga mboga. Vizuri kabisa
bidii katika elimu, kilimo na ufugaji biashara ndio msingi wa maisha ya familia na ukoo wetu gentleman.

hii ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uaminifu ni Neema na Baraka ya ziada tu niliojaaliwa 🐒
 
Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora, ametapeliwa na kuporwa saa yenye thamani ya shilingi milioni moja baada ya kudanganywa na mganga wa kienyeji mjini Sumbawanga kuwa atapata utajiri wa haraka.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.

Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.

#EastAfricaRadioView attachment 3270549
Safi sana mkiambiwa muokoke kwa Yesu Kristo hakuna fedheha kama hizo hamtaki! Bado mnang'ang'ania uchawi na ushirikina! Wajinga ndio waliwao!
 
Back
Top Bottom