Bunzali Jidola (30), mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Igunga mkoani Tabora, anadaiwa kumchinja na kumuua mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili kwa kutumia kitu chenye ncha kali, kumjeruhi mke wake, na kisha kujinyonga.
Kamanda wa Polisi, Richard Abwao ameeleza kuwa mwanaume huyo alimtuhumu mke wake kuwa mtoto hakuwa wake.
======
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Buzali Budola (30), Mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Wilayani Igunga Mkoani Tabora, anadaiwa kutekeleza tukio la kusikitisha la kumuua Mtoto wake wa Kike mwenye umri wa miezi miwili.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, inadaiwa kuwa Mwanaume huyo alimchinja Mtoto huyo kikatili Nyumbani kwao, na baada ya kutekeleza tukio hilo, aliondoka eneo la tukio na baadaye kujinyonga kwa kutumia shuka alilolifunga kwenye nguzo ya umeme katika Kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinahusishwa na wivu wa mapenzi, ambapo Mwanaume huyo alikuwa akimtuhumu Mke wake kuwa Mtoto huyo si wa kwake.
Aidha, imeelezwa kuwa kabla ya kujinyonga, Mwanaume huyo alimjeruhi vibaya Mke wake katika tukio hilo hilo na Mwanamke huyo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, iliyopo Wilayani Igunga, akiwa katika hali mbaya na akipatiwa matibabu.Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini mazingira kamili ya tukio hilo na kuchukua hatua stahiki.