Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoa uzi anaye ripoti tukio hili ni Askari polisi. maelezo yake tu yanathibitisha.Mmmh polisi wetu hawa kweli tena kwa maelezo kuwa alikorofishana nao!! Hapo lazima kachezea kipigo kweli akawa hoi mpaka mauti sasa sababu iwe ipi ili wajinasue katika kumpekua wakagundua alikuwa na powerbank ya asili na kwa kuwa wengi wanaamini hayo ikabidi watokee huko.
Shida ya watu wenye mamlaka wanajua bado wanaishi na watu wenye akili ya 1950 ambao wengi hawajaenda shule. Sasa hivi Tanzania imebadilika sana mpaka ufikie hatua ya kumdanganya mtu inabidi ujipange sana.Watanzania sio wajinga
kumchania sare afande...huyu atakuwa amekula kichapo heavy MPAKA akaona nyota.Hakuna cha hirizi wala mavi ya kuku kapigwa na Polisi huyo wanamtafutia sababu.
ha ha ha ha ha ha mtema kuni alafu ni mtu wa huko huko taboraInamaana alivyochana gwanda hakufanywa chochote? nahisi alipewa mkong'oto hawezi kuchana akaachwa tu! Hirizi is by the way ila watakuwa walimwonyesha cha mtema kuni.
I DOUBT HUYU ALIKUWA NI JAMBAZI HATARI SANA.Michael Paschal mwenye umri wa miaka 33, mkazi wa Uhemeli Ndala, Nzega, mkoa wa Tabora, afariki baada ya kuporwa hirizi zake na polisi akifanyiwa upekuzi.
Kijana huyo ambaye ni bodaboda alifikishwa kituoni mara baada ya kumkaba na kumchania sare CPL Lucas aliyekuwa katika majukumu ya usalama barabarani.
Askari (Lucas) alipomsimamisha Michael akiwa anaendesha pikipiki yenye usajili MC.246 BXH kwa ukaguzi, Michael alifanya fujo kwa kumkaba polisi na kumchania sare zake.
Askari alifungua mashtaka ya kuzuiwa kufanya majukumu yake, kijana Michael alikamatwa na kufikishwa kituoni alipokuwa akifanyiwa upekuzi alikutwa na hirizi mbalimbali sehemu ya mwili wake.
Mtuhumiwa akaomba asitolewe hirizi zake kwani zikitolewa atakufa, kulingana na sheria za upekuzi kwa mtuhumiwa anayewekwa mahabusu walizitoa hirizi hizo.
Baada ya kuzitoa hirizi hali yake ikaanza kubadilika kwa kuishiwa nguvu na kuzilai alipelekwa zahanati ya Kashishi kwa matibabu ilipofika saa 3.00 usiku akafariki dunia. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora.