TABORA: Mtu mmoja afariki baada ya kupokonywa hirizi zake

Ukute walipishana kauli tu na hata kuchaniwa hajachaniwa,mara paap mbaroni, kichapo na kudedishwa🙆
 
Police huwa wanajifichaga ktk shamba la karanga kila wakigundua washafanya makosa, uelewa huwa finyu mno. Serikali haiamini ktk ushirikina hirizi wala uchawi, ndugu zake wakifungua kesi mahakamani mnaweza kuuthihirishia uma kuwa marehemu alikufa kwa kuondolewa hirizi ilihali uchawi hautambuliki ktk mhimili huo wa mahakama?
 
Kachomoa betri, hakujua kwamba ndo bima yake.
 
Hakuna cha hirizi wala mavi ya kuku kapigwa na Polisi huyo wanamtafutia sababu.
kwa mfumo wa utendaji kazi wa jeshi hilo, hakuna mchana sare za polisi anaeweza toka salama kituoni mwao. Na hakuna daktri atakaye fanya postmortem ya ukweli. Hiyo kapata kisago cha uhakika.
 
Michael Paschal mwenye umri wa miaka 33, mkazi wa Uhemeli Ndala, Nzega, mkoa wa Tabora, afariki baada ya kuporwa hirizi zake na polisi akifanyiwa upekuzi.

Kijana huyo ambaye ni bodaboda alifikishwa kituoni mara baada ya kumkaba na kumchania sare CPL Lucas aliyekuwa katika majukumu ya usalama barabarani.

Askari (Lucas) alipomsimamisha Michael akiwa anaendesha pikipiki yenye usajili MC.246 BXH kwa ukaguzi, Michael alifanya fujo kwa kumkaba polisi na kumchania sare zake.

Askari alifungua mashtaka ya kuzuiwa kufanya majukumu yake, kijana Michael alikamatwa na kufikishwa kituoni alipokuwa akifanyiwa upekuzi alikutwa na hirizi mbalimbali sehemu ya mwili wake.

Mtuhumiwa akaomba asitolewe hirizi zake kwani zikitolewa atakufa, kulingana na sheria za upekuzi kwa mtuhumiwa anayewekwa mahabusu walizitoa hirizi hizo.

Baada ya kuzitoa hirizi hali yake ikaanza kubadilika kwa kuishiwa nguvu na kuzilai alipelekwa zahanati ya Kashishi kwa matibabu ilipofika saa 3.00 usiku akafariki dunia. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora.
Uongo, kafa kwa kipigo cha polisi
 
Nitapenda kuhudhuria huu msiba

Wamepiga mtu wa watu wanasingizia uongo tu kipidi hiki ukikamatwa ma polisi uwe kimya kwa lolote ukiomba msamaha tu basi unapigwa mpaka ndio yanayotokea kama visingizio hivyo!
 
Uchunguzi unahitajika likely kala kichapo heavy!

Kumchania sare askari halafu upelekwe kituoni ukawe chini ya askari!!
 
Huu ni uongo tena bila aibu,

Polisi wanapiga hovyo watuhumiwa halafa wanakuja na sababu za kijinga wanapofariki kwa Mateso.

Hapa mmenikera, hovyo kabisa aliyetoa sababu hii kuwa imepelekea kifo.
 
Polisi waache uongo,tangu lini mtu akivuliwa hirizi anakufa?uchunguzi ufanyike atakuwa kapigwa huyo
 
Back
Top Bottom