Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna cha hirizi wala mavi ya kuku kapigwa na Polisi huyo wanamtafutia sababu.
VIP bado serikali haiamini uchawi?Michael Paschal mwenye umri wa miaka 33, mkazi wa Uhemeli Ndala, Nzega, mkoa wa Tabora, afariki baada ya kuporwa hirizi zake na polisi akifanyiwa upekuzi.
Kijana huyo ambaye ni bodaboda alifikishwa kituoni mara baada ya kumkaba na kumchania sare CPL Lucas aliyekuwa katika majukumu ya usalama barabarani.
Askari (Lucas) alipomsimamisha Michael akiwa anaendesha pikipiki yenye usajili MC.246 BXH kwa ukaguzi, Michael alifanya fujo kwa kumkaba polisi na kumchania sare zake.
Askari alifungua mashtaka ya kuzuiwa kufanya majukumu yake, kijana Michael alikamatwa na kufikishwa kituoni alipokuwa akifanyiwa upekuzi alikutwa na hirizi mbalimbali sehemu ya mwili wake.
Mtuhumiwa akaomba asitolewe hirizi zake kwani zikitolewa atakufa, kulingana na sheria za upekuzi kwa mtuhumiwa anayewekwa mahabusu walizitoa hirizi hizo.
Baada ya kuzitoa hirizi hali yake ikaanza kubadilika kwa kuishiwa nguvu na kuzilai alipelekwa zahanati ya Kashishi kwa matibabu ilipofika saa 3.00 usiku akafariki dunia. Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora.
Jiepushe na huu unanga.*KUMZUIA ASKARI KUFANYA KAZI YAKE (.)*
MLALAMIKAJI :F.196 CPL LUCAS
MTUHUMIWA :MICHAEL s/o PASCHAL, 30YRS, MNYAMWEZI, MKAZI WA UHEMELI NDALA NZEGA MKOA WA TABORA (.) MNAMO TAREHE 02/11/2019 MAJIRA YA SAA 16:00 HUKO MAENEO YA KASHISHI SENTA KATA/TARAFA KASHISHI, WILAYA YA KALIUA NA MKOA WA TABORA (.)NCO NO F. 196 CPL LUCAS AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA DORIA USALAMA BARABARANI
ALIMSIMAMISHA MTUHUMIWA KWA LENGO LA KUMKAGUA CHOMBO CHAKE CHA USAFIRI PIKIPIKI YENYE NO ZA USAJILI MC. 246 BXH SUNLG NYEKUNDU, NDIPO MTUHUMIWA ALIPOANZA KUFANYA FUJO AKIWA NA ABIRIA WAKE AITWAE RAMADHAN S/0 HAMIS 33YRS, MNNYAMWEZI NA MKAZI WA NDALA UHEMELI KWA KUMKABA UNIFORM YA POLISI NA KUICHANA NA KUMSABABISHIA MAUMIVU YA MWILI (.) ABIRIA HUYO ALITOWEKA NA PIKIPIKI WAKATI WA FUJO HIYO AMBAPO ALIKAMATWA BAADAE AKIWA NA PIKIPIKI TAJWA HAPO JUU (.) JUHUDI ZA KUOMBA MSAADA KITUONI ZILIFANYWA NA MLALAMIKAJI NA KUFANIKISHA KUMFIKISHA KITUONI NA KUFUNGULIWA KESI YA KUMZUIA ASKARI KUFANYA KAZI YAKE. LAKINI WAKATI ANAPEKULIWA ALIKUTWA NA HILIZI MBALIMBALI SEHEMU ZA MWILI WAKE NA ALIOMBA ZISITOLEWE KWANI UKIZITOA ATAKUFA HATA HIVYO KULINGANA NA SHERIA ZA UPEKUZI KWA MTUHUMIWA ANAEWEKWA MAHABUSU TULIZITOA HIRIZI HIZO NA BAADA YA KUZITOA HIZO HIRIZI HALI YAKE ILIBADILIKA NA KUKOSA NGUVU NA KUZILAI HIVYO ALIKIMBIZWA ZAHANATI YA KASHISHI KWA MATIBABU NA ILIPOFIKA SAA 03:00 USIKU ALIFARIKI DUNIA (.) MWILI WA MAREHEMU UMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TABORA KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
101%Hakuna cha hirizi wala mavi ya kuku kapigwa na Polisi huyo wanamtafutia sababu.
Ndio mada zake hz!
Ndio mada zake hz!