elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,733
Yani nyoka kiboko, na uji kanywa bure na kutoka hajatoka. Yani ni mbishi zaidi ya nickNimecheka kwa sauti, nimepata picha anavotoka nduki.
Yaani kazimia tu hajapata madhara ya sumu?
Bora walivoamua kuwaita wataalamu wa kisayansi....sasa wao wakaleta mganga ambaye akaamua kumuunguza kwa uji.....ha ha ha ha....nyoka hasira yake ikaishia kwake.
Technology yake ilifika kikomoKama ni mganga basi koboko baada ya kunywa uji angekufa.
Tena kamuuma mara nne! Halafu jamaa bado yu hai? Hakika huyo si koboko ninayemjua.Nitaamini kama ni koboko nikipewa taarifa za huyo mganga huko alipo,sitegemei kusikia yupo hai maana mziki wa huyo bwana ni weka mbali na watoto.
Usifanye maisha yawe magumu mambo mengine yaache kama yalivyoKuna watu wataiamini hii habar
Wapo nyoka wanaogonga meno yanabaki na anaweza kukugonga tena na tena, mojawapo ni Mamba's awe green/ black Mamba anaweza gonga zizi zima la ng'ombeKawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?
Hatari sanaHapana kaka huyu ni zaidi ya BM, huyo akikugonga huchukui nusu saa sehemu aliyokugonga inaanza kuoza
Kumbee!Huyo jamaa pamoja na kujuwa vizuri nyoka lakini anamheshimu koboko
Hao hawawezi kumrudisha labda wamuue.... jamii zinazoendekeza ushirikina ni tabu sana. Si kuna idara ya wanyama pori waitwe wamrudishe mgeni kwenye makazi yake sahihi?
Mganga kawazidi akili yaani hivi baada koboko kuingiza kichwa kwenye uji wa moto sumu yake inakuwa haina nguvu kali tena kama awali japo mbinu ya mganga aliye mbwinu mbunu ilifeli maarifa tu.Au labda ni artificial,maana kama nyoka amefikia kugida uji wa moto kama maji ya baridi huyo tutaamini ni wa kawaida mkuu??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787]!
Piga picha anakimbia huku amefunga msuliView attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.
Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.
Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.
Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.
Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.
Chanzo cha habari: CG FM Radio
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Piga picha anakimbia huku amefunga msuli
Ndio KAZI yao waliyosomea.Hao hawawezi kumrudisha labda wamuue.
Kwanini waganga wote ni waislamu?View attachment 2060887
Nyoka aina ya koboko anadaiwa kuweka kambi katika eneo la Mlimani City kata ya Ng'ambo manispaa ya Tabora ambapo amegeuka kuwa tishio la maisha kwa wananchi wa mtaa huo.
Katika jitihada za kumuondoa nyoka huyo wananchi walimleta mganga wa kienyeji ambaye alitamba kumuondoa nyoka huyo.
Mganga huyo Hassan Jumanne anasema alipanda juu ya mti wa muembe yalipo makazi ya nyoka huyo akiwa na chungu chenye uji wa moto ambao nyoka huyo alitoka na kuingiza kichwa kwenye uji kabla ya kumshambulia kwa kumgonga mara nne.
Mganga alizimia na kuanguka na alipopata fahamu alikimbia akiacha vifaa vyake vya uganga katika eneo hilo.
Uongozi wa kata hiyo umeanza jitihada za kuwasiliana na maliasili ili kumuondoa nyoka huyo.
Chanzo cha habari: CG FM Radio
ChaiKawaida nyoka wa kawaida hagongi zaidi ya Mara moja kwasababu akigongo meno hubakia je huyu kapata wapi uwezo wa kugonga mara nne?