Tabora: Rais Samia akifungua barabara ya Tabora, Koga, Mpanda

Tabora: Rais Samia akifungua barabara ya Tabora, Koga, Mpanda

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifungua barabara ya Tabora - Koga - Mpanda (km 342.9) Sikonge, Mkoani Tabora leo tarehe 18 Mei, 2022. Rais yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku 3.


======
Rais apewa zawadi ya Ng'ombe


Hotuba ya Rais Samia Akifungua Barabara
Rais Samia aanza kwa kutoa salamu kwa wageni waalikwa wote waliohudhuria, viongozi mbalimbali wa taasisisi, dini, wanahabari na watu wote kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutoa shukurani kwa Mungu kwa kumjalia kuwepo hapo kwa kuzindua barabara mbili kwa leo Mkoani Tabora, awali alianzia Nyahua wilayani Uyui kabla ya kuzindua ya Sikonge Mpanda.

Kama alivyotangulia kusema watu wengine akiwemo waziri wa ujenzi na uchukuzi, barabara hii ni barabara muhimu kwa ukuaji wa uchumi kwa mikoa ya Katavi, Tabora na Rukwa na kanda mbalimbali zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani za Zambia, Burundi, Rwanda Kongo hivyo kukamiliaka kwa barabara hii kutachochea ukuaji wa uchumi na kurahisisha usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na bidhaa zingine mnazozalisha.

Natoa rai kwa wizara husika pamoja na uongozi wa Mkoa kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuendeleza kilimo cha kisasa na ufugaji wenye tija hali kadhalika mjiwekee mikakati wa ujenzi wa viwanda vidovidogo na kuvutia wawekezajiwa viwanda vikubwa, nafahamu uwekezaji wa viwanda ni miundombinu na serikali inajitahidi kujenga miundombinu hiyo. Kazi kwenu uongozi wa Mkoa kuhakikisha mnavutia uwekazaji wa viwanda vikubwa.

Nafahamu hapa Sikonge na maeneo mengi ya Tabora kuna wafugaji wa nyuki na hivyo ni wazalishaji wa mazao ya Asali na huko nyuma asali ilikuwa ikiuzwa bila kuongezwa thamani lakini nafurahi sasa uongezaji thamani unafanyika, Nimefurahi sana kusikia wenzetu wa FDB(Banki ya maendeleo ya Afrika) imetoa fedha ya kufundishwa elimu kwa wazalishaji wa asali na pia Taasisis ya misitu TFS yenyewe imejenga kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya asali, niwaombe sasa viongozi wa mkoa kuhakikisha asali inazalishwa kwa viwango bora ili kufikia viwango vya ubora wa masoko ya kimataifa maana asali ni zao muhimu sana.

Barabara ya Tabora, Koga Mpanda imejengwa kwa ushirikiano wa serikali yetu na Bank ya maendeleo ya Afrika kwa gharama ya shilingi Bilioni mia nne sabini na tatu pointi nane, saba, tisa(473,879,000,000) . Na kwakweli banki hii imekuwa washirika wakubwa kwenye maendeleo ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara.

Miradi iliyokamilika kupitia ufadhili wa bank hii ni, barabara ya Namtumbo- Tunduru, km 193, Barabara ya Dodoma- Iringa km 260, Barabara ya Dodoma - Babati km188 barabara ya Sakina - Tengeru km 14, barabara ya mchepuo ya Arusha km 42.4, Mbinga Mbamba bay km 66, Tunduru Nakapanya Mambaka Mtamba swala km 242 hizi zote tumeshikwa mkono na bank ya maendeleo ya Afrika.

Viongozi, na wananchi jana nilisisitiza kuhusu kulinda miondo mbinu lakini nimesikitishwa kuwa katika mradi unaondelea kuna watu wameng'oa nguzo za taa za barabarani na kuiba panel 9 za sola katika kijiji cha Kasandalala tumbili usenga na Sikonge Mjini, huu ni uhujumu uchumi, nimetjaja mabilioni tunayokopehswa ili tufanye miradi hii mtu kwa utashi wake anakwenda kung'oa nguzo ili apate panel ya sola, inampeleka wapi? itamfaa nini? Hata ukiitumia nyumbani kwako hutaitumia muda mrefu.

Miradi hii ni kwa ajili yenu wananchi, taa zikimulika zinawamulikia ninyi mtu unaweza kukaa hapo chini ya taa na kufanya biashara yako hapo, Nina imani jeshi la polisi litawafatilia wote waliofanya uhalifu huu, pia watu wanaofanya uhalifu huu mnakaa nao majumbani naomba sana toeni polisi za wahalifu hawa.

Wizara ya Ardhi itumie vyema ardhi kwa kupanga vyema matumizi ya ardhi ili itumike kama ilivyo kusudiwa, pia Niwaombe wanyemwezi na wasukuma wenzangu huu si wakati wa kukaa na ng'pmbe wengi ambao hawakuletei faida, kukaa na ng'ombe wengi wasio na faida si zama hizi kwani wanasababisha kuhitaji ardhi kubwa na kuharibu vyanzo vya maji na kuharibu mazingira pamoja na kukosekana kwa mvua kutokana na ukataji miti. Wizara ya uvuzi, misitu, ardhi kaeni pandeni matumizi mazuri ya ardhi ili kilimo kiwepo, uvuvi uwepo na ufugaji uwepo mvua ipakane na maendeleo yapatikane bila kuhardibu mazingira.

Nina taarifa za wavivi kwenye mto Ugala kuwa maafisa wanatengeneza mazingira ya rushwakwa kuwazuia watu kuvua ili wale wanaotoa fedha ndio wanaruhusiwa kuvua, naomba wizara husika iliangalie swala hilo ipasavyo.

Kero nyingine ni kero ya mboela tunaelewa kwamba misimu 2 ilipitwa ya kilimo hapakuwa na mbolea ya kutosha na hiyo si kwa matakwa ya Seriakli ila uzalishaji wa mbolea ulisimama kutokana na UVIKO, na mbolea ilikuwepo nchi nyingi ilirudisha mbolea kutokana na kutokuwa na vigezo na hata kwa ukanda huu wa kwetu ilirudishwa na mbolea kidogo iliyopatikana iligawiwa kwa wakulima na si kwa kiwango cha kutosha, na kwa kuliangalia hilo tumeanza kujenga viwanda vya kuzalisha mbolea, na kiwand akimoja kimejengwa Dodoma.

Kuhusu Utoaji wa kodi
"Simamieni ukusanyaji wa mapato, serikali haina muujiza mwingine wa kuimarisha mapato isipokuwa kukusanya kodi, tuwahimize wafanyabiashara walipe kodi na kutumia mashine za risiti za kielektroniki. Tunahitaji sana kuleta fedha nyingi katika halmashauri zetu nchini ili maendeleo ya wananchi yapatikane na miradi ya maendeleo iendelee kujengwa" - Rais Samia Suluhu Hassan wakati akifungua barabara ya Tabora-Koga mpaka Mpanda.
 
TRA na Mamlaka zingine zinazokusanya mapato mumeusikia ujumbe wa Rais Samia lakini?

Mjumbe hauwawi 👇

Screenshot_20220518-145635.png
 
TRA na Mamlaka zingine zinazokusanya mapato mumeusikia ujumbe wa Rais Samia lakini?

Mjumbe hauwawi 👇

View attachment 2229429
Rais uko sahihi kabisa. Kwa kuongeza tu pengine tuangalie mfumo wetu wa utawala kama unahamasisha wanaosimamia ukusanyaji wa kodi kujiongeza. Au niulize, kuna motisha/adhabu kwa halmashauri inayokusanya mapato zaidi au vinginevyo. Katika kupanua mjadala tunaweza kutazama upya vigezo vya kuanzisha halmashauri zetu. Inawezekana tunatoa kipaumbele vivutio vya kisiasa au kiuchumi. Nani mwenye uhakika (kwa data) lipi ni lipi hapo.
 
Sawa hatukatai.

Vipi matumizi? Per diem? Posho? Vikao? Ukiritimba wa manunuzi?
Mkiongeza tija kwenye matumizi haitasaidia?
 
Wanyamwezi hatimaye sasa neema imefunguliwa kwenu...

na navyowajua nyie - hapa ni kama mmewekewa libwata vile - yaani nyie na CCM ni hadi kufa !!

Hongera kwa uamifu wenu tangu 1961 hadi leo.
 
Back
Top Bottom