DOKEZO Tabora: Wanafunzi wafukuzwa kwa kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza

DOKEZO Tabora: Wanafunzi wafukuzwa kwa kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakuu habari zenu!

Kuna hii taarifa ya hawa watoto wa Shule kufukuzwa huko Tabora, kuna namna sauti inatakiwa kupazwa kutokana na adhabu kubwa waliyopewa ukilinganisha na umri wao, walikuwa na nafasi yakuonywa na kuendelea na masomo ila sio kukatiza mazima.

Wanafunzi wawili wa kike kutoka shule moja ya sekondari mkoani Tabora, wamefukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Gwajima D , amewataka maafisa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii na maafisa Elimu wote nchini kuimarisha madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kusaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Soma, Pia:
+
Tabora: Wanafunzi Tabora wakamatwa na simu zaidi 120 zilizoungwa makundi wanayotumia kutumiana picha/video za ngono

Hawa watoto wangeelimishwa tu hakukuwa na haja ya kuwafukuza.
 
JAPO SIJAONA HIZO PICHA NA SITAKI KUZIONA.
Naungana na wachangiaji waliopinga ADHABU KUBWA waliyopewa ya kufukuzwa shule.
wangesimamishwa shule kwa muda suspension na kupewa adhabu nyingine.
Pia ikiwezekana wangehamishwa shule wapelekwe shule maalumu za watoto watukutu kama zipo nchini kama hazipo ni vizuri zikawepo ili ziwe maalumu kwa mafunzo hasa ya watoto watundu.
Haki ya kupata elimu katika karne hii ni muhimu ,kumnyima mtoto haki ya kupata elimu ni kumnyima fursa sababu ,foolish age ikiisha ,kipindi cha mpito cha ukuaji cha watoto huwa wanakuwa watundu na kupenda kujaribu kila kitu.ILA WANAWEZA KUPATA NEEMA YA KUBADILIKA NA KUWA RAIA WEMA
Na wakipata support ya kisaikolojia itawasaidia wabadiilike ,na hata sasa wameshajutia kosa lao pengine.
Pia walikuwa wanahitaji msaada wa matibabu ya kliniki ya kisaikolijia kutoka kwa wataalamu wa afya ya saikolojia na msaada wa huduma za kiroho.Kuwafukuza shule ni kuwaongezea stress na hakuwasaidii watoto wenyewe.
Malezi ya watoto miaka hii sio rahisi sana yana athiwa sana katika njia hasi na utandawazi ,na ubize wa wazazi katika kutafuta riziki ,wazazi wanakosa muda wa kuwa karibu na watoto wao.Lakini hata baadhi ya wazazi nao maisha wanayoishi na mazingira wanayoishi imekuwa na athari hasi katika maadili ya na malezi ya watoto.
Kama jamii na Taifa utandawazi umeathiri athari hasi katika maadili kumongnyoa maadili,
kuanzia Tv stesheni kurusha maudhui ya ngono,mitandao ya kijamii radio,na michezo ya luninga maigizo,nyimbo,
wasanii wa sanaa ambao ndio wanaushawishi kwa watoto kusifia kuhamasisha maadili mabaya.
Wazazi wenyewe wengine maadili yao na malezi yao siyo mazuri,na mazingira .
 
Wakuu habari zenu!

Kuna hii taarifa ya hawa watoto wa Shule kufukuzwa huko Tabora, kuna namna sauti inatakiwa kupazwa kutokana na adhabu kubwa waliyopewa ukilinganisha na umri wao, walikuwa na nafasi yakuonywa na kuendelea na masomo ila sio kukatiza mazima.

Wanafunzi wawili wa kike kutoka shule moja ya sekondari mkoani Tabora, wamefukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka maafisa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii na maafisa Elimu wote nchini kuimarisha madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kusaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Soma, Pia:
+
Tabora: Wanafunzi Tabora wakamatwa na simu zaidi 120 zilizoungwa makundi wanayotumia kutumiana picha/video za ngono
Sheria gani imetumika kuwafukuza?
 
Hiyo ni adhabu kubwa Kwa watoto
Tushajua ni watoto na walifanya utoto
Wawape adhabu hata ya viboko
Lakini wawape fursa ya kusoma tena
Mtu hubadillika, wanaweza kubadilika na kuwa wema

Sio hekima hiyo kumfukuza mtoto shule
Watafundisha wengine tabia mbaya. Adhabu hiyo ni sawa
 
Wakuu habari zenu!

Kuna hii taarifa ya hawa watoto wa Shule kufukuzwa huko Tabora, kuna namna sauti inatakiwa kupazwa kutokana na adhabu kubwa waliyopewa ukilinganisha na umri wao, walikuwa na nafasi yakuonywa na kuendelea na masomo ila sio kukatiza mazima.

Wanafunzi wawili wa kike kutoka shule moja ya sekondari mkoani Tabora, wamefukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Gwajima D , amewataka maafisa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii na maafisa Elimu wote nchini kuimarisha madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kusaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Soma, Pia:
+
Tabora: Wanafunzi Tabora wakamatwa na simu zaidi 120 zilizoungwa makundi wanayotumia kutumiana picha/video za ngono
Shenzi kabisa hilo ndio onyo sahihi kwao .hao ukiwabakisha wata waaribu wengine
 
hakuna siri, kwa mtazamo wangu, katika mawaziri failures wa mama Samia huyu Dkt. Gwajima D anaongoza.

Taifa limeporomoka kabisa kimaadili mpaka naamini kuwa yeye ndiye muhusika mkuu wa maadili kuporomoka kwa kushindwa kwake kudhibiti kwa njia za kisasa.

Nilicheka peke yangu, aliponambia humu JF kuwa anatumia mbinu za enzi za mMkapa kupambana na matatizo ya sasa.

Nilimponda hapohapo, kwani hata nilipojaribu kumshauri alikuwa hanielewi kabisa. Nikaelewa kuwa huyu mwanamke hana ubunifu kabisa.

Tunajionea maadili ya jamii yanavyozidi kuporomoka kila kukicha.

Sidhani kama tuko sawa tunaposema naye ni mhusika mkuu, tatizo hili lilianza zamani na wahusika ni mifumo na viongozi wakubwa wa hii mifumo kuanzia kichwa mpaka chini.

Tunaweza kumlaumu kwa kushindwa kuona ukubwa wa tatizo kama Waziri na kuja na mipango madhubuti ya haraka kutatua tatizo.

Binafsi naamini tatizo kuu ni kuupokea utandawazi mzima mzima bila kuasses athari zake na kuziwekea control measures.
Sasa kama waziri alipaswa kuanzia hapo, kupima ukubwa wa tatizo, kutibu waathirika na kulizuia lisilete madhara zaidi.

Juzi nilimwambia Mh, wengine sisi ni waumini wa matokeo ya mipango Bali sio waumini wa mipango ya kwenye makaratasi na maneno.
 
hakuna siri, kwa mtazamo wangu, katika mawaziri failures wa mama Samia huyu Dkt. Gwajima D anaongoza.

Taifa limeporomoka kabisa kimaadili mpaka naamini kuwa yeye ndiye muhusika mkuu wa maadili kuporomoka kwa kushindwa kwake kudhibiti kwa njia za kisasa.

Nilicheka peke yangu, aliponambia humu JF kuwa anatumia mbinu za enzi za mMkapa kupambana na matatizo ya sasa.

Nilimponda hapohapo, kwani hata nilipojaribu kumshauri alikuwa hanielewi kabisa. Nikaelewa kuwa huyu mwanamke hana ubunifu kabisa.

Tunajionea maadili ya jamii yanavyozidi kuporomoka kila kukicha.
Kwa hili yuko sahihi hao wanafunzi ni washenz na hakuna kutetea uovu hakj sawa kwa wote
 
Hio ni kazi ya wazazi wao wafanyiwe yote hayo na wazazi wao wafanye nn
Kimsingi kuwafukuza watoto sio swala wawataftie Ata fani "tusitumie tu Ile kauli ya asiyefunzwa na mamaye maana wahenga wanasema mtoto akinyea mkono usimkate mkono usafi she na umuelekeze kwa adhabu " ambayo ni win win to both side mkosea na mkosewa wapewe viboko vingi nawakae chini ya uangalizi mara nyingi

Watoto kama hao kama ni dull darasani wapelekwe veta Nina imani watatoka vizuri jaribu kufanya research vijana ambao hawakuwa wazuri darasani Ata kinidhamu kweny maisha au mtaani kuna angle wanakuwaga na ustadi mkubwa
 
Acheni kutetea uovu dizain hio haifai kukaa darasa moja na wengine
Hawana sifa za kuendelea kusoma hapo ,
Kosa ni kosa hata kama ni mwanafunz haiondoi ukal wa kosa
 
Back
Top Bottom