Tabora: Watu 6 ikiwemo askari wauawa, silaha ya kivita AK-47 yachukuliwa

Tabora: Watu 6 ikiwemo askari wauawa, silaha ya kivita AK-47 yachukuliwa

Jeshi la Polisi mkoani Tabora limeanza uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa watu sita, wakiwemo askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Walinzi wa Hifadhi za Vijiji (VGS) na madereva wawili, baada ya kuvamiwa na kundi la wananchi katika Hifadhi ya Wanyamapori Iswagala, iliyopo Kijiji cha Utimle, Wilaya ya Sikonge.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Twaha Lulengelule, amewaambia waandishi wa habari jioni hii kuwa kundi la wafugaji lilivamia kambi ya askari wa doria likiwa na silaha za jadi.


Amesema wakati wa tukio hilo, askari walikuwa wakishirikiana na maafisa wengine wa Halmashauri katika operesheni ya kukamata mifugo iliyoingizwa kinyume cha sheria ndani ya hifadhi hiyo.


Kwa mujibu wa Kamanda Lulengelule, kundi hilo liliwashambulia askari na watu wengine waliokuwapo, kisha kuchoma moto gari aina ya Land Cruiser na kuchukua silaha moja ya kivita aina ya AK-47.


Amesema watu wengine watano walijeruhiwa katika tukio hilo na kwamba Polisi inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
Wamejikita sana kwenye magwaride ya ukakamavu mbele ya viongozi huku wakiwa watupu mbele ya majangiri.
 
IGP , nikipe ushauri wa Bure, SACP Jumanne Muliro, ahamishiwe Mkoa wa Tabora haraka! Huku Tabora hali sio shwari, kuna vikosi kutoka nchi Jirani.
 
Ni sawa ila retaliation itakayopigwa hilo eneo! Sijui kwa kweli, hiyo AK ipatikane haraka la sivyo Ile wanaitaga task force ikifika huko watakufa watu na watakimbia kijiji hadi bunduki ipatikane.

Task force sikuizi inakabwa na sheria nyingi. Kipindi cha jk walikuwa waki commit hayo mambo sana
 
Matukio kama hayo ni ya kuyachukulia kwa umakini sana ili kutatua tatizo sio kusema tu kuwakamata waliohusika bila kutatua tatizo mauaji yataendelea kuwepo na zaidi ya hapo..
 
Matukio kama hayo ni ya kuyachukulia kwa umakini sana ili kutatua tatizo sio kusema tu kuwakamata waliohusika bila kutatua tatizo mauaji yataendelea kuwepo na zaidi ya hapo..
Uonevu ukizidi ndiyo matokeo yake hayo mkuu. Umesikia kuna kiongozi amenunua nissan civillian kwa matumizi ya umma kwa bei ya mil 334 😂😂 Hiyo pesa sipati mtumba wa ZhongtongClimber kweli😂
FB_IMG_1789834557810.jpg
 
Hizi ndo changamoto zinazotokea nchini kwenye sekta ya ufugaji, taarifa nilizonazo ni kwamba taarifa hiyo japo ni rasmi ila imechujwa kupoza makali.


wafugaji kanda hiyo wanaendelea kukaa maporini kwenye hifadhi, mamlaka za kudhibiti nazo hua zinafanya jambo hilo kama kitega uchumi ukikamata ng'ombe faini za hapa na pale si haba mifuko inajaa.

Kufupisha story, waziri mkuu wiki iliyopita tu kasisitiza mamlaka hizo za kudhibiti wasikamate mifugo, yani waziri mkuu na nickname waliyompa "magufuli wanna be" anasema mifugo isikamatwe, lakini haonekani akieleza nini kinafata baada ya hapo , wafugaji wanaondokaje kwenye hifadhi? Au sasa ni ruksa? , nani mwenye jukumu la kusimamia miongozo?

askari pampja na wananchi wanakufa kwa porojo za viongozi, inasikitisha sana
 
Uonevu ukizidi ndiyo matokeo yake hayo mkuu. Umesikia kuna kiongozi amenunua nissan civillian kwa matumizi ya umma kwa bei ya mil 334 😂😂 Hiyo pesa sipati mtumba wa ZhongtongClimber kweli😂View attachment 3674645
Kwa nini ununue hiyo mkuu tafuta Scania Ir 6 Intercape au Greyhound wanazo used zimeisha warranty ya kampuni hiyo ni rand 2m na chenji juu hizo chenji zake unabaki nazo kulipia kodi hiyo pesa nanunua Scania G 460 horse za 2016 au 17 za 70m 5 bila kodi zinafika Tunduma hapo zinapumua na Service nimefanya Scania, Borgsburg.
 
Ni sawa ila retaliation itakayopigwa hilo eneo! Sijui kwa kweli, hiyo AK ipatikane haraka la sivyo Ile wanaitaga task force ikifika huko watakufa watu na watakimbia kijiji hadi bunduki ipatikane.
Hiyo sio suluhu Bali itakuza tatizo kuwa kubwa
 
Back
Top Bottom