TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

Kuna best yangu alifungua mgahawa, daaaahhh, waliroga mpaka akafulia.
Siku nyingine moto hauwaki mpaka jirani amalize kuhudumia chai ya asubuhi kwa wateja.
Siku nyingine supu aliyopika alfajiri asubuhi anakuta funza ishaharibika
Hii mimi pia nimetoka kuipata kwa mtu wangu wa karibu wiki mbili zilizopita.

Alifungua mgahawa, yeye akipika chakula, sana sana maharage na nyama, maharage anapika asubuhi, ikifka mchana yameharibika.

Mara anaboresha miundombinu na kubadili mapishi ila watu wanaenda sehemu nyingine ambayo ni chafu na sio chakula kizuri. Akaanza kushusha bei ya chakula, lakini bado ngoma bado ikawa ni ngumu mno kwake.

Mwisho akaona ni bora tu afunge biashara.
 
Ushahidi umepatkana lakn kesi itakaa miaka 2 na watatoka
 
Hii mimi pia nimetoka kuipata kwa mtu wangu wa karibu wiki mbili zilizopita.

Alifungua mgahawa, yeye akipika chakula, sana sana maharage na nyama, maharage anapika asubuhi, ikifka mchana yameharibika.

Mara anaboresha miundombinu na kubadili mapishi ila watu wanaenda sehemu nyingine ambayo ni chafu na sio chakula kizuri. Akaanza kushusha bei ya chakula, lakini bado ngoma bado ikawa ni ngumu mno kwake.

Mwisho akaona ni bora tu afunge biashara.
Unakuta ka hela ka mkopo😂😂
 
Siku za nyuma Kuna jamaa alishikwa na nyeti za binadamu ila alishushiwa kipigo cha mbwa mwitu na wananchi hadi kukata roho. Kumbe ndio hiyo biashara. Katika ulimwengu wa roho hizo nyeti zinatumika kupita filimbi huko angani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unaua kwenda kutibu huu si ujinga waganga walishaisha karne ya 19 waliobaki kwa sasa wote matapeli tu
 
Sasa sehemu za siri za ile gender unazikataje... Watu wamekuwa washenzi sana karne hiiii

Utu umeshuka bei, thamani ya pesa imepanda
 
Mikoa yote kuna washirikina lakini kanda ya ziwa, hasa maeneo ya usukumani, imani za kishirikina zimezidi sana. Hawa, walio wengi wanauabudu, wanauishi, na wanautumikia ushirikina.

Ukiwa kanda ya Ziwa, hasa maeneo ya wasukuma, ukipata ajali, kama unajimudu, kimbia haraka ukajifiche. Watakuja haraka, usije ukadhani wanakuja kukusaidia. Kama hujiwezi, watakuja kukukata viungo mbalimbali.

Niliwahi kushuhudia huko Kahama, kijiji cha Mbizi, mtoto aliyetoka kumaliza darasa la saba, aliyehisiwa kuiba begi tupu lililoanikwa, akipigwa, baadaye kumbe walimwua, wakamchoma moto. Nilipita sehemu hiyo baadaye wakiwa wamemchoma moto, baada ya muda mfupi, hakuna kiungo kilichosalia, na hata walipomchomea likageuka kuwa shimo maana walibeba majivu, mpaka udongo wa pale walipomchomea. Nikaambiwa kuwa eti mabaki hayo yote yalichukuliwa kwenda kutumika kwenye ushirikina.

Kanda ya Ziwa, bado kuna mambo mengi ya hovyo sana. Ustaarabu wa mwanadamu wa kawaida, kwa walio wengi haupo.

Hatuyasemi haya kwa nia ya kuwadharau bali kuwahamasisha wale waliostaarabika kutoka kanda hiyo, kusaidia kuibadili jamii yao.
 
Polisi mkoani Tabora inawashikilia watu wanne akiwemo mganga wa jadi anayetuhumiwa kununua viungo na damu za binadamu na kuvitumia katika shughuli zake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na msako uliofanywa na Polisi kwa lengo la kudhibiti uhalifu, likiwemo tukio la kuuawa mtoto wa miaka 14 wilayani Sikonge Januari 21.

Katika tukio hilo, msichana huyo anadaiwa kuuawa na kisha baadhi ya viungo vyake zikiwemo sehemu za siri kuondolewa na wauaji wake.

"Mara baada ya tukio hilo ufuatiliaji ulianza mara moja na kufanikiwa kuwakamata watu watatu waliotiliwa shaka. Katika mahojiano dhidi yao walimtaja mganga waliyedai kuwa anahusika na kununua viungo vya binadamu.

“Jitihada zilifanyika na hatimaye alikamatwa na baada ya kufanyiwa mahojiano alikiri kuwa huwa anapelekewa viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu za siri za mwanamke, sehemu za siri za mwanaume na kumtaja mtu anayempelekea," amesema Kamanda Abwao.

Mtuhumiwa huyo aliyekuwa anampelekea mganga huyo damu na viungo vya binadamu naye amekamatwa na katika mahojiano ya awali amekiri kuhusika katika utendaji wa matukio ya mauaji maeneo mbalimbali.

Kamanda Abwao ameeleza kuwa, mtuhumiwa ameeleza kuwa huwa anapata damu kutoka kwa watu kwa kuwachoma na kitu chenye ncha kali katika shingo na kukinga damu inayoruka katika chupa ndogo na kisha damu hiyo huuzwa kiasi cha Sh600,000 kwa chupa.

Ameongeza kuwa mbali ya damu pia huchukua baadhi ya viungo vya miili yao hasa sehemu za siri ambavyo wanavipeleka kwa waganga wa kienyeji ambao ndio wanaowaagiza na kisha kuwalipa fedha kulingana na makubaliano.

Ameeleza kuwa, katika mahojiano hayo mtuhumiwa huyo amewataja watu wengine ambao anashirikiana nao katika utekelezaji wa mauaji hayo na upelelezi unaendelea ili kufikia lengo la kuukamata mtandao wote wa watu wanaohusika na mauaji hayo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom