Hii mimi pia nimetoka kuipata kwa mtu wangu wa karibu wiki mbili zilizopita.Kuna best yangu alifungua mgahawa, daaaahhh, waliroga mpaka akafulia.
Siku nyingine moto hauwaki mpaka jirani amalize kuhudumia chai ya asubuhi kwa wateja.
Siku nyingine supu aliyopika alfajiri asubuhi anakuta funza ishaharibika
Alifungua mgahawa, yeye akipika chakula, sana sana maharage na nyama, maharage anapika asubuhi, ikifka mchana yameharibika.
Mara anaboresha miundombinu na kubadili mapishi ila watu wanaenda sehemu nyingine ambayo ni chafu na sio chakula kizuri. Akaanza kushusha bei ya chakula, lakini bado ngoma bado ikawa ni ngumu mno kwake.
Mwisho akaona ni bora tu afunge biashara.