TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

TABORA: Watu 9 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji na kuuza viungo vya binadamu, damu ya mtu inauzwa Tsh 600,000

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limekamata mtandao wa watu 9 ambao wametajwa kuhusika na tuhuma za mauaji pamoja na kuendesha biashara ya mauziano ya viungo mbalimbali vya sehemu ya mwili wa binadamu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, ACP. RICHARD ABWAO amesema mtandao huo umekamatwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kutokea mauaji ya kinyama ya binti mmoja huko wilayani Sikonge Mkoani Tabora.

Amesema kufuatia tukio la mauaji hayo watu watatu walikamatwa baada ya kutiliwa mashaka ambapo walimtaja mganga wa kienyeji ambaye amekuwa akinunua viungo vya mwili ikiwemo sehemu za siri za jinsia zote pamoja na matiti.

Aidha, mganga huyo ambaye hakutajwa jina lake kutokana na sababu za kiuchunguzi alikiri kuhusika na tuhuma hizo huku naye akimtaja mtu ambaye amekuwa akimuuzia viungo hivyo vya mwili ambaye pia alihojiwa na kukubali kufanya hivyo pamoja na kutekeleza matukio mengine ya mauaji ya kinyama yaliyo ambatana na kukinga damu katika chupa ambayo amekuwa akiiuza kwa kiasi cha shilingi laki 6.
 
Hivi bin-Adamu tumefika huko? Kisa ni kuhitaji MALI, iko shida mahali.....MUNGU utuokoe.
 
Umasikini ni mbaya sana ila tumuombe Mungu sana atuepushe mbali na tamaa za namna hii
 
... hivi Ulaya na Marekani kuna waganga wa kienyeji hasa wapiga ramli? Ifike mahali itungwe sheria kupiga ramli iwe kosa la jinai! Mpiga ramli/mganga kifungo kisichopungua miaka 10 jela; mpigiwa ramli jela miaka 2.
 
Hivi bin-Adamu tumefika huko???........kisa ni kuhitaji MALI.....iko shida mahali.....MUNGU utuokoe..
Tatizo lilianza pale hela ilipopewa nafasi tu ya kufanya kila kitu duniani!

Waturudishe kwenye barter trade tu😅
 
Mmm ushirikina na uchawi iwe ni jinai sasa, tatizo ushahidi sasa mpaka wakamatwe na viungo kama hao, maana unaweza kuishi naye maisha yote na usimtambue.
 
Back
Top Bottom