Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -11
Siku ile nilitembea hatari ila sikufanikiwa kupata sehemu ya kazi ,nilijaribu kwenda mpaka hospital ya wilaya ,wakanielekeza kuandika barua ya kujitolea ,Sasa nikaona huku Niko ugenini nikijitolea maisha yangu nitayamudu vipi ,nikaona nirudi home nikajipange kesho niende dar labda dar naweza kubahatisha
Basi bana nilirudi na uchovu nikapumzika ,kesho yake asubuhi nikaanza safari ya dar ,kumbuka nilitoka nyumbani kama na laki 6 hivi Sasa hapo nimeshatumia kama laki na nusu
Baadae nikafika mbagara rangi 3 nikaona nianzie hapo kutafuta kazi ,aise nilitembea nikajikuta nimefika sehemu inaitwa kizuiani basi nikafika kwenye zahanati moja nikamkuta mzee fulani hivi amevaa nguo za nursing sijui ndio alikuwa in charge pale ,basi mzee akaanza kuniuliza maisha yangu , nyumbani ,nilikosomea ,baadae mzee alianza kunitukana hatari ,wewe kwenu mwanza huku dar umefuata ni Nini ,utembezi tembezo tu watoto wadogo wadogo ,dah niliondoka bila kuaga naona mzee aliona nitampokonya nafasi yake ,basi nilitembea mpaka ilivyofika jioni nikaamua kurudi mkuranga
Kesho yake asubuhi nikaamkia dar ila safari hii nikishukia ubongo darajani nikaanza kutafuta kazi maeneo ya ubongo baadae nikajikuta Niko tandale ,nikafika zahati moja hivi inaitwa Mico ,nikamkuta Dr nikamueleza shida yangu ,akaniambia pale waga wanafanya kazi kwa shift yaani Kila baada ya masaa nane anaingia mtu mwingine ,ila yeye akaniambia leo anaunganisha nitembee tembee nirudi pale saa 7 mchana ,ataniachia huyo mchana mpaka asubuhi yaani nipige shift mbili ,basi nikashukuru mungu nikazunguka zunguka ilivyofika saa 7 nikaenda pale ,mzee akanipa maelekezo basi akaniachia kijiwe ,baadae nikamtaarifu juma jamaa yangu kwamba Leo sitirudi hata funguo za geto langu nilikuwa naacha kwa juma
Sent from my TECNO P703 using
JamiiForums mobile app
Muendelezo soma
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu