Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -15

Boss ;aise Dr yuhu ni Dr samweli tulikuwa nae hapa kwa muda mrefu lakini akawa amepata kazi sehemu nyingine yenye mshahara mkubwa zaidi akawa ameondoka na aliondoka kwa uzuri tu ,Sasa hivi yupo likizo kwa muda wa mwezi mmoja ,Sasa itabidi upokezane nae kwenye shift zako

Asassin Eagle ; ok bosi nimekusikia lakini Mimi Niko hapa nimelidhika na nikipatacho kutoka hapa ,Niko hapa muda wote Sasa nikimpisha jamaa nitadistabu kipato changu tofauti na hapo naona Kuna haja ya kutafuta kazi sehemu ingine ,yaani kunipumzisha jamaa kwenye muda wa likizo wa jamaa sidhani kama ni sawa

Bosi ; basi chagua moja kama kuacha kazi au kumpisha jamaa afanye kazi kwa muda .


Asassin [emoji1659] ;sawa bosi Mimi naona Bora niache kazi ,nilifanya hivyo kwa sababu tayari Nina sehemu ya kujishikiza nikaona sehemu za ubabaishaji zitanipotezea muda


Basi Mimi nikaamua kuondoka zangu ,nikachukua Kila kilicho changu nikasepa , niliendelea kufanya kazi kinondoni wakati huo naendelea kutafuta kazi sehemu ingine

Baadae nikapata kazi mbezi ,nikafanya interview pale ikaonekana Mambo mengi nayamudu ikiwemo swala la uongozi ,bosi akaniambia ,bosi akaniambia nahitaji uwe msimamizi wangu ,watumishi wa hapa ni changamoto wanapenda sana kudokoa dokoa pesa hivyo inahitajika umakini mkubwa ,nikamwambia hakuna shida ila naomba kufanya kazi siku tano ila naomba jumamosi na jumapili nipumzike hapo nilikuwa nalenga kinondoni

Baada ya Mimi kuondoka bunju yule jamaa aliendelea kufanya kazi lakini hata wiki mbili hazikuisha ,akaitajika ofisin kwao kwa kazi ya dharula ,basi jamaa ikabidi arudi kazini kwake pale akawaacha hawana mtu




Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -11
Siku ile nilitembea hatari ila sikufanikiwa kupata sehemu ya kazi ,nilijaribu kwenda mpaka hospital ya wilaya ,wakanielekeza kuandika barua ya kujitolea ,Sasa nikaona huku Niko ugenini nikijitolea maisha yangu nitayamudu vipi ,nikaona nirudi home nikajipange kesho niende dar labda dar naweza kubahatisha

Basi bana nilirudi na uchovu nikapumzika ,kesho yake asubuhi nikaanza safari ya dar ,kumbuka nilitoka nyumbani kama na laki 6 hivi Sasa hapo nimeshatumia kama laki na nusu

Baadae nikafika mbagara rangi 3 nikaona nianzie hapo kutafuta kazi ,aise nilitembea nikajikuta nimefika sehemu inaitwa kizuiani basi nikafika kwenye zahanati moja nikamkuta mzee fulani hivi amevaa nguo za nursing sijui ndio alikuwa in charge pale ,basi mzee akaanza kuniuliza maisha yangu , nyumbani ,nilikosomea ,baadae mzee alianza kunitukana hatari ,wewe kwenu mwanza huku dar umefuata ni Nini ,utembezi tembezo tu watoto wadogo wadogo ,dah niliondoka bila kuaga naona mzee aliona nitampokonya nafasi yake ,basi nilitembea mpaka ilivyofika jioni nikaamua kurudi mkuranga

Kesho yake asubuhi nikaamkia dar ila safari hii nikishukia ubongo darajani nikaanza kutafuta kazi maeneo ya ubongo baadae nikajikuta Niko tandale ,nikafika zahati moja hivi inaitwa Mico ,nikamkuta Dr nikamueleza shida yangu ,akaniambia pale waga wanafanya kazi kwa shift yaani Kila baada ya masaa nane anaingia mtu mwingine ,ila yeye akaniambia leo anaunganisha nitembee tembee nirudi pale saa 7 mchana ,ataniachia huyo mchana mpaka asubuhi yaani nipige shift mbili ,basi nikashukuru mungu nikazunguka zunguka ilivyofika saa 7 nikaenda pale ,mzee akanipa maelekezo basi akaniachia kijiwe ,baadae nikamtaarifu juma jamaa yangu kwamba Leo sitirudi hata funguo za geto langu nilikuwa naacha kwa juma

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
Hii mico ndio ile ya sinza ya watoto au?
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -16
Kote huko nilikozunguka kufanya kazi Kuna changamoto niliyokuwa naipitia kutoka kwenye familia yangu,kwangu Mimi naziita tabu ,tukianzia kwa kina anko mpaka na kwa ndugu ambao nilikuwa siwafahamu

Kina mjomba walivyosikia tu Nina kibarua Kila mtu akaanza kuniorodhoshea shida zake ,mara mwingine anahitaji nimnunulie gali la biashara , mwingine anunuliwe mashine ,duh kwa mshahara gani ninaopata mpaka nifanye hayo Mambo ,shida ndogo ndogo ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wangu nilikuwa nawasaidia tatizo ni kwamba hawaridhiki ,siku ukiwa hauna basi maneno na dua mbaya hutozimaliza

Sema ukweli hiyo hali ilikuwa inaniongezea stress sana kwa sababu unajikuta una solve shida za watu mpaka unakosa pesa ya kutumia

Hali hii ilipelekea mpaka nikawa nashindwa kuwatafuta kwenye simu kuwasalimia ,yaani unampigia mtu kumsalimia ndio kwanza anakuelezea shida zake

Nisiseme wengine Hata mama yangu pia alikuwa hanitamkii maneno mazuri ,kwakweli nilikuwa na mawazo sana

Misaada hii tunayochukua kwa watu ni madeni makubwa ,sema kwa sababu katika safari ya maisha Kuna changamoto nyingi huwezi jua ,ukikutana na watu wanaosaidia kwa lengo ukifanikiwa na yeye anufaike aise utajuta

Basi baada ya kupata kazi mbezi ikabid niende kuhamisha vitu vyangu mkuranga ,tayari nilishakuwa na vitu vingi kidogo ikiwemo godoro na vyombo

Basi nilihamisha vitu vyangu kutoka mkuranga mpaka sehemu moja mwananyamara kwa manjunju ,pale ilikuwa rahisi kufika makumbusho lakini karibu sana na kinondoni

Chumba nilipata kwa elfu 40 ,kigeto geto niliona sio mbaya

Yule mchumba wangu tulikuwa bado tunawasiliana na nilipanga mwisho wa mwezi niende kwao kujitambulisha kama sio kuoa kabisa

Basi niliendelea kupiga kazi kwakweli maisha yangu yalibadilika sana ,ilivyofika mwisho wa mwezi niliomba ruhusa ya wiki moja kote nilikokua nafanyia kazi ili niweze kwenda mwanza kwao na mchumba wangu



Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom