Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -9
Baada ya kuridi nyumbani niliona nirudi kule visiwani nikafanye vishughuli vidogo vidogo wakati huyo nasubili matokeo ,nilifanya kazi ndogo ndogo nikawa natunza pesa kwa sababu nilikuwa Sina matumizi yoyote ,msosi nilikuwa napata kambi ya wavuvi ,baadae matokeo yalitoka tukawa tumefaulu fresh tu japo Mimi nilipata GPA ya gentromeni ila cathe yeye alipata second upper class .

Baada ya matokeo kutoka nikaona niende zangu dar nikatafute vibarua ,badi baba jumla ya fedha niliyotunza ilikuwa kama laki 6 hivi ,nikaanza zangu safari ya kwenda dar ,sehemu ya kufikia kulikuwa na rafiki yangu tulisomaga nae primary nilivyompa mchongo akaniambia nije tu .

Basi jioni nilisogea mwanza mjini pale nyegezi ,kulivyokucha nikapanda gali nakumbuka ilikuwa inaitwa happy national ,yaani hiyo ndio safari yangu ya kwanza ya umbali mrefu ,tulifika dar kwenye saa 2 hivi usiku ,jamaa yangu nikamkuta ubungo ananisubiri ,jamaa akaniambia anapokaa ni mbali inabid tulale pale ubungo stend tutaanza safari kesho asubuhi kukikucha ,tulilala pale mpaka asubuhi baadae tukatembea mpaka darajani tukapanda magali ya mbagara rangi 3 ,tulivyofika mbagara rangi 3 tukapanda magali ya mkuranga, nauli ilikuwa sh 1000 kutoka mbagara mpaka mkuranga .

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-10
Tulifika mkuranga kwenye saa mbili hivi tukafika mpaka nyumbani kwa jamaa ,jamaa alikuwa amepanga chumba kimoja ,alikuwa anaishi na mke wake na watoto wa watatu ,kutokana na uchovu wa safari nilifika nikalala humo humo chumbani kwake ,kwenye saa tisa alasiri niliamka nikaoga chakula kikikuwa tayari tukala baadae tukaenda barabarani kunyoosha miguu ,nikamuuliza vip mpango wa usiku kulala itakuwaje sababu naona unachumba kimoja tu jamaa yangu ,jamaa akasema nisiwaze Kuna rafiki yake anafanya kazi ya ulinzi nitalala kwenye geto lake ,basi nikasema fresh tu .

Baadae tulirudi home kwenye mida ya usiku tukala chakula baadae jamaa akanipeleka kwenda kulala ,hapakuwa mbali sana ni mwendo kama wa nusu kilomita ,tulipitia funguo kwa jamaa sehemu anapolinda jamaa ,tulivyofika kwenye geto la jamaa duh japo nilishawahi kuishi sehemu ngumu ila yule jamaa alikuwa amezidi uchafu yaani kunanuka hatari , jamaa sijui alikuwa anatumia pombe za kienyeji .

Basi Mimi nikamwambia jamaa yangu Mimi hapa nalala Leo tu ,kesho itabid tufanye utaratibu wa kupata chumba ,jamaa akaniambia nikiwahi kutoka kazini tutatafuta chumba ,jamaa yangu alikuwa anafanya kazi za saidia fundi ,pia alikuwa anajaribu jarubu kupaka rangi na kuandika maandishi kwenye mabango au sehemu mbali mbali

Basi jamaa akaondoka zake Mimi nikalala ,aise nilishindwa kulala kulikuwa na kunguni na mbu wengi hatari na sisimizi wanaita nyenyere ,nilihangaika usiku mzima kunguni mpaka ukutani ,kwenye muda wa saa 12 kasoro jamaa mwenye geto akaja kugonga mlango ,nilienda kufungua jamaa mwenyewe alikuwa amelewa hatari hata hiyo kazi ya ulinzi nilikuwa nashangaa anaifanyaje na hali ile

Basi kulivyopambazuka Mimi nikaelekea home kwa jamaa nilivyofika nikamwambia Shem ngoja nilale kidogo yaani sijalala huko nilipoenda ,Shem wangu akaniambia jamaa zamani alikuwa yupo vizuri tu ,alikuwa anaishi na mke wake na watoto ,baadae akamleta mdogo wake wa kiume pale home na jamaa kazi zake kipindi hiko zilikuwa za safari kwenye magali ya mizigo ,Sasa siku moja karudi zake usiku sijui alikuwa hajampa taarifa mke wake ,kufika dilishani akasikia sauti ya mwanamke analia kilio Cha mahaba ,jamaa ikabidi asikilizie pale dilishani akagundua ile sauti ni ya mke wake jamaa akabomoa mlango ,kuingia ndani akakuta bwana mdogo anamchakata shemeji yake ,
Nasikia jamaa alizimia kufika asubuhi mke hayupo Wala dogo hayupo

Basi baada ya stori kumuhusu jamaa ikabidi nilale zangu ,midamida ya mchana jamaa akarudi ,tukaanza kutafuta chumba tukapata chumba fulani kwenye nyumba ya miti ila imesakafiwa freshi tu ,Kodi ilikuwa elfu 10 kwa mwezi hakuna umeme ,baada ya kusafisha tulielekea barabarani kununua mkeka ,neti na dawa ya sisimizi ,basi nikaanza maisha rasmi nikawa pale kwangu naenda kulala kula kwa mshikaji siku ambazo jamaa Mambo magumi nilikuwa nachangia

Baadae nilimsimulia jamaa yangu kwamba Mimi nirudia shule na nimesoma Sasa hivi Nina diploma ya clinical medicine,hivyo nimekuja kutafuta kazi ila sehemu niliyolenga kwenda ni dar,jamaa yangu tumuite juma akanishauri nianzie kutafuta kazi palepale nikikosa ndio niende dar .

Basi kesho yake asubuhi nikaanza kutembea na bahasha ,ndugu acha kabisa kutafuta kazi ni bonge la kazi

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -11
Siku ile nilitembea hatari ila sikufanikiwa kupata sehemu ya kazi ,nilijaribu kwenda mpaka hospital ya wilaya ,wakanielekeza kuandika barua ya kujitolea ,Sasa nikaona huku Niko ugenini nikijitolea maisha yangu nitayamudu vipi ,nikaona nirudi home nikajipange kesho niende dar labda dar naweza kubahatisha

Basi bana nilirudi na uchovu nikapumzika ,kesho yake asubuhi nikaanza safari ya dar ,kumbuka nilitoka nyumbani kama na laki 6 hivi Sasa hapo nimeshatumia kama laki na nusu

Baadae nikafika mbagara rangi 3 nikaona nianzie hapo kutafuta kazi ,aise nilitembea nikajikuta nimefika sehemu inaitwa kizuiani basi nikafika kwenye zahanati moja nikamkuta mzee fulani hivi amevaa nguo za nursing sijui ndio alikuwa in charge pale ,basi mzee akaanza kuniuliza maisha yangu , nyumbani ,nilikosomea ,baadae mzee alianza kunitukana hatari ,wewe kwenu mwanza huku dar umefuata ni Nini ,utembezi tembezo tu watoto wadogo wadogo ,dah niliondoka bila kuaga naona mzee aliona nitampokonya nafasi yake ,basi nilitembea mpaka ilivyofika jioni nikaamua kurudi mkuranga

Kesho yake asubuhi nikaamkia dar ila safari hii nikishukia ubongo darajani nikaanza kutafuta kazi maeneo ya ubongo baadae nikajikuta Niko tandale ,nikafika zahati moja hivi inaitwa Mico ,nikamkuta Dr nikamueleza shida yangu ,akaniambia pale waga wanafanya kazi kwa shift yaani Kila baada ya masaa nane anaingia mtu mwingine ,ila yeye akaniambia leo anaunganisha nitembee tembee nirudi pale saa 7 mchana ,ataniachia huyo mchana mpaka asubuhi yaani nipige shift mbili ,basi nikashukuru mungu nikazunguka zunguka ilivyofika saa 7 nikaenda pale ,mzee akanipa maelekezo basi akaniachia kijiwe ,baadae nikamtaarifu juma jamaa yangu kwamba Leo sitirudi hata funguo za geto langu nilikuwa naacha kwa juma

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -7
Nilivyorudi kwa mama nikamuelekeza umuhimu wa hiyo elimu ninayopata ,pia tokea nimeingia chuo mungu alimjaalia sana mama yangu biashara zake zilikuwa zinaenda vizuri ,Kuna wale matajiri walikuwa ggwananunua dagaa pia walinisaidia kumshjjauri mama ,basi mama akalainikva akanipa ada niliyokuwa nadaiwa pia akahaidi atanisomesha kwa roho moja ,unajua mama yangu muamko wa kosomesha alikua Hana kabisa Kuna Dada yangu alifaulu vizuri tu lakini alishindwa kumsomeshia wakati Kuna watu wanafanya biashara ndogo ndogo lakini wanamudu kusomesha watoto wao ,hivyo mama alipata moyo nakuanza kusapoti hii ilifungua njia mpaka kwa wadogo zangu ,basi Mimi nirudi zangu chuo, aise nilijitahid sana kusoma yaani muda wote nilikuwa maeneo ya chuo sina Cha jumamosi Wala jumapili ni msuli kwenda mbele ,Sasa pale chuo kulikuwa na msichana mmoja alikuwa anapiga msuli hatari yaani alikuwa sometimes anakesha alikuwa anaitwa Catherine , Catherine akavutiwa na usomaji wangu tukaunda ka group ka kujisomea ,Lile group lilinisaidia sana hata ufaulu wangu uliongezeka,tulikuwa hatutofautiani sana maisha na Catherine japo mwenzangu alinizidi kidogo ,basi katika kusoma soma tukajikuta tumekuwa wapenzi japo Catherine alikuwa ni mkubwa kwangu alinizidi miaka mitatu ,Mimi getoni kwangu nilikuwa nalala chini nilikuwa na mkeka wangu (jamvi) ,basi bana mapenzi yalivyokolea ikabidi nihamie kwa Catherine tukawa tunaishi kama mke na mume ila msuli tulikuwa tunapiga kama kawa , Catherine japo alikuwa mpenzi want lakini alikuwa pia rafiki yangu yangu mkubwa ,muda wote huyo ilikuwa sijafanikiwa kutembea nae japo tulikuwa tuna lala wote lakini ilikuwa ngumu kwangu ku du nae ,yaani tulikuwa tunafanya romance unaona kabisa kalainika ukitaka kuweka anagoma anakubadilika ukizingatia Mimi mwenyewe nilikuwa mgeni wa hayo Mambo ,basi tulienda hivyo hivyo ,kuna siku akanipanga mapema kwamba today it's a day of reward .

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Hapa sasa
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu-10
Tulifika mkuranga kwenye saa mbili hivi tukafika mpaka nyumbani kwa jamaa ,jamaa alikuwa amepanga chumba kimoja ,alikuwa anaishi na mke wake na watoto wa watatu ,kutokana na uchovu wa safari nilifika nikalala humo humo chumbani kwake ,kwenye saa tisa alasiri niliamka nikaoga chakula kikikuwa tayari tukala baadae tukaenda barabarani kunyoosha miguu ,nikamuuliza vip mpango wa usiku kulala itakuwaje sababu naona unachumba kimoja tu jamaa yangu ,jamaa akasema nisiwaze Kuna rafiki yake anafanya kazi ya ulinzi nitalala kwenye geto lake ,basi nikasema fresh tu .

Baadae tulirudi home kwenye mida ya usiku tukala chakula baadae jamaa akanipeleka kwenda kulala ,hapakuwa mbali sana ni mwendo kama wa nusu kilomita ,tulipitia funguo kwa jamaa sehemu anapolinda jamaa ,tulivyofika kwenye geto la jamaa duh japo nilishawahi kuishi sehemu ngumu ila yule jamaa alikuwa amezidi uchafu yaani kunanuka hatari , jamaa sijui alikuwa anatumia pombe za kienyeji .

Basi Mimi nikamwambia jamaa yangu Mimi hapa nalala Leo tu ,kesho itabid tufanye utaratibu wa kupata chumba ,jamaa akaniambia nikiwahi kutoka kazini tutatafuta chumba ,jamaa yangu alikuwa anafanya kazi za saidia fundi ,pia alikuwa anajaribu jarubu kupaka rangi na kuandika maandishi kwenye mabango au sehemu mbali mbali

Basi jamaa akaondoka zake Mimi nikalala ,aise nilishindwa kulala kulikuwa na kunguni na mbu wengi hatari na sisimizi wanaita nyenyere ,nilihangaika usiku mzima kunguni mpaka ukutani ,kwenye muda wa saa 12 kasoro jamaa mwenye geto akaja kugonga mlango ,nilienda kufungua jamaa mwenyewe alikuwa amelewa hatari hata hiyo kazi ya ulinzi nilikuwa nashangaa anaifanyaje na hali ile

Basi kulivyopambazuka Mimi nikaelekea home kwa jamaa nilivyofika nikamwambia Shem ngoja nilale kidogo yaani sijalala huko nilipoenda ,Shem wangu akaniambia jamaa zamani alikuwa yupo vizuri tu ,alikuwa anaishi na mke wake na watoto ,baadae akamleta mdogo wake wa kiume pale home na jamaa kazi zake kipindi hiko zilikuwa za safari kwenye magali ya mizigo ,Sasa siku moja karudi zake usiku sijui alikuwa hajampa taarifa mke wake ,kufika dilishani akasikia sauti ya mwanamke analia kilio Cha mahaba ,jamaa ikabidi asikilizie pale dilishani akagundua ile sauti ni ya mke wake jamaa akabomoa mlango ,kuingia ndani akakuta bwana mdogo anamchakata shemeji yake ,
Nasikia jamaa alizimia kufika asubuhi mke hayupo Wala dogo hayupo

Basi baada ya stori kumuhusu jamaa ikabidi nilale zangu ,midamida ya mchana jamaa akarudi ,tukaanza kutafuta chumba tukapata chumba fulani kwenye nyumba ya miti ila imesakafiwa freshi tu ,Kodi ilikuwa elfu 10 kwa mwezi hakuna umeme ,baada ya kusafisha tulielekea barabarani kununua mkeka ,neti na dawa ya sisimizi ,basi nikaanza maisha rasmi nikawa pale kwangu naenda kulala kula kwa mshikaji siku ambazo jamaa Mambo magumi nilikuwa nachangia

Baadae nilimsimulia jamaa yangu kwamba Mimi nirudia shule na nimesoma Sasa hivi Nina diploma ya clinical medicine,hivyo nimekuja kutafuta kazi ila sehemu niliyolenga kwenda ni dar,jamaa yangu tumuite juma akanishauri nianzie kutafuta kazi palepale nikikosa ndio niende dar .

Basi kesho yake asubuhi nikaanza kutembea na bahasha ,ndugu acha kabisa kutafuta kazi ni bonge la kazi

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Shunie
 
Hahahaha umenifanya nicheke,ati mzee ulivyomwambia nia yako ya kazi akaanza kukutukana 😅aliona unataka kumnyang'anya tonge mdomon
 
Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu -11
Siku ile nilitembea hatari ila sikufanikiwa kupata sehemu ya kazi ,nilijaribu kwenda mpaka hospital ya wilaya ,wakanielekeza kuandika barua ya kujitolea ,Sasa nikaona huku Niko ugenini nikijitolea maisha yangu nitayamudu vipi ,nikaona nirudi home nikajipange kesho niende dar labda dar naweza kubahatisha

Basi bana nilirudi na uchovu nikapumzika ,kesho yake asubuhi nikaanza safari ya dar ,kumbuka nilitoka nyumbani kama na laki 6 hivi Sasa hapo nimeshatumia kama laki na nusu

Baadae nikafika mbagara rangi 3 nikaona nianzie hapo kutafuta kazi ,aise nilitembea nikajikuta nimefika sehemu inaitwa kizuiani basi nikafika kwenye zahanati moja nikamkuta mzee fulani hivi amevaa nguo za nursing sijui ndio alikuwa in charge pale ,basi mzee akaanza kuniuliza maisha yangu , nyumbani ,nilikosomea ,baadae mzee alianza kunitukana hatari ,wewe kwenu mwanza huku dar umefuata ni Nini ,utembezi tembezo tu watoto wadogo wadogo ,dah niliondoka bila kuaga naona mzee aliona nitampokonya nafasi yake ,basi nilitembea mpaka ilivyofika jioni nikaamua kurudi mkuranga

Kesho yake asubuhi nikaamkia dar ila safari hii nikishukia ubongo darajani nikaanza kutafuta kazi maeneo ya ubongo baadae nikajikuta Niko tandale ,nikafika zahati moja hivi inaitwa Mico ,nikamkuta Dr nikamueleza shida yangu ,akaniambia pale waga wanafanya kazi kwa shift yaani Kila baada ya masaa nane anaingia mtu mwingine ,ila yeye akaniambia leo anaunganisha nitembee tembee nirudi pale saa 7 mchana ,ataniachia huyo mchana mpaka asubuhi yaani nipige shift mbili ,basi nikashukuru mungu nikazunguka zunguka ilivyofika saa 7 nikaenda pale ,mzee akanipa maelekezo basi akaniachia kijiwe ,baadae nikamtaarifu juma jamaa yangu kwamba Leo sitirudi hata funguo za geto langu nilikuwa naacha kwa juma

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Endelea mkuu
 
Back
Top Bottom