Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu

Moja ya story inayohuzunisha Sana,
Cha muhimu achana na ndgu , saidia kidg Kwan we ukifa nani,

Saidia kiasi tu
 
Nje ya box;
mkuu nahisi wewe una matatizo ndiyo maana hao wanawake wawili mmeshindwana bila sababu za msingi kuwa makini na ujirekebishe hata huyo watatu angalia sana.Yawezekana una matatizo fulani kwa vyovyote hutayazungumza hapa.
Mke wa kwanza alipata mtu akamwambia kuwa nakuacha.
Wa Pili alioa akiwa mentally unfit Tena single mama watt watatu .ama hujaelewa. Nesi alimuelewa pia nadhani.

Narudia kusema Kama kila siku kuwa wanaume tuko vizuri Ni mbususu ndio zinazotuangusha Basi. Yaani ikiwepo dawa ama kidonge unameza miaka mitano huna hisia unaweka Mambo yako sawa tungekuwa sawa. Niko primary namuomba Mungu anisaidie niende boarding school wanaume. Namshukuru nilipata hitaji langu
 
Sjaona kosa katika maisha yako ila fata sana akili yako mwanamke alikushauri omba kazi wakati ulishakua vizuri biashara itakua ngumu kwako bora utulie save pesa yako tu
 
Ila jamaa huyu Ni mpambanaji mno Nina Imani na wewe utatoboa.

Yaani aliyekuchomea kwa aliyekubinafishia labda alitaka aibe mbinu unazotumia.


Ila binadamu Ni wanyama kiasili.


Naomba tuwe tunabadilishana mawazo Kama hutojali your no kwa pm yangu.

Naona kwa mbali Kuna vinasaba vinashabihiana.


Ama hapa watu watahisi kuwa Kuna upigaji labda ama.


Ila let us be close, just kwa phone tu I can see Kuna something ahead
 
Mimi ni kijana nilizaliwa mwaka 88 Mwanza mjini, tuliishi kwenye nyumba ya familia ile nyumba tuliishi familia mbili babu alikuwa na wake watatu hivyo pale walekaa Bibi zangu wawili na watoto wao ambao Kila Bibi alikuwa na watoto Saba Kila mtoto alikuwa na watoto wake pia hivyo waligawana vyumba, Bibi mwingine yeye hakuzaa, japo babu alikuwa na nyumba nyingine tatu.

Kila Bibi alikuwa amepewa nyumba moja na nyumba hizi zilikuwa zimejengea mitaa tofauti, kwa kifupi maisha hayakuwa mazuri pale tuliishi kigumu gumu, uwezo wangu darasani pia haukuwa mzuri japo nilikuwa siwi wa mwisho mwaka 2000 walielewana wauze ile nyumba sisi tulienda kuishi na Bibi yetu ambae alikuwa ameacha chumba kimoja katika ile nyumba waliogawiwa, vyumba vingine walikuwa wamepangisha Kodi watoto ndio waliokuwa wanachukua yeye hakupewa kitu.

Bibi yangu alikuwa mpole sana, watoto wa kiume ndio walipanga pembeni watoto wa kike walikaa na mama yao pamoja na wajukuu wale wa kiume pia kula walikuwa wanakula pale kwa bibi ,Bibi yangu alikuwa anajishughulisha na biashara ndogo ndogo aliweza kutulisha wote na matumizi madogo madogo alikuwa anatupatia ,kwakweli maisha Yale yalikuwa yananiumiza sana yaani kulala ni tabu wajukuu wengi mna lala mpaka uvunguni nilijaribu kwenda kwa mzee wangu kukaa sababu yeye alikuwa na nyumba kubwa tu ,lakin yule mke wake akakataa Mimi kukaa pale yule mwanamke alisusia Kila kitu akasema kama Mimi nakaa pale basi yeye ataondoka.

Baba ikabidi anifukuze ila niligoma kuondoka baadae baba akaniita pembeni kwa upole akanieleza nirudi tu kwa mama yangu akaniambia hanichukii ila Sasa hivi ni ngumu kumuelewa ila nikiwa mkubwa nitakuja kumuelewa basi bwana ikabidi niondoke zangu niende kwa Bibi tuliishi hivyo hivyo kwa tabu aise ,mwaka 2002 nilimaliza darasa la Saba sikufanikiwa kufaulu Bibi nae alikuwa ameshachoka Kila siku anaumwa baadae Bibi alishindwa kabisa kuendelea kufanya biashara ikabidi apumzike huwezi amini watoto walishindwa kumtunza kabisa yule mzee.

Itaendelea
===
Muendelezo soma Tabu ninayopata kutoka kwenye familia yangu
,Nakadori wangu ukuje my
 
Nduguyangu,mm mwenyewe ni Dr.kama ww hapo nanipo serikalini,,napia natokea hukohuko kanda ya ziwa,ushauri wangu mkuu,nikua kwanza pole kwa changamoto nyingi sana,kingine nikua malengo yako uliyoyaorodhesha hapo nimengi,mazuri nayenye kukukwamua kimaisha nakua mtu mwenye mafanikio,ila ningumu snaa narudia tena ningumu mno kuyatekeleza ukiwa umeajiriwa ktk hizi ajira zetu za serikali cjajua utachanga vipi karata zako hadi ufanikiwe kuwa mfanya biashara wa ku-run hizo business at the same time ukiwa muajiriwa wa serikalini kwenye changamoto lukuki,nakusihi jaribu kuacha kazi baada ya kua umepata mtaji either kwa kukopa then fanya mradi kama ulivyokua unafanya kule dar kabla hujaajilwa serikalini hapo unaweza kuadvance kabla hujawa mzee,naimani naww nikijana wa below40 tu.nawasilisha!!!!
Ni kweli mkuu ,lengo langu ni kuja kuacha kazi serikalini ili niweze kusimamia Mambo yangu ,kwa Sasa kwenye upande wa ufugaji wa kuku Niko vizuri ,siku nikifikisha mil 100 nitaacha kazi ,hivyo vitu nikivyoorodhesha hapo ni vingi lakini naanza na kimoja kimoja
Kule nilipotoka Nina nyumba 2 ,dodoma Nina kiwanja ,mwanza ninacho pia ,kile Cha dar yule mwanamke wa kwanza alichukua ,nasikia ameshakiuza

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wangu rudi jijini Dar es salam , huko wilayani utatumia nguvu kubwa na miaka mingi sana ili kufika unapotaka kufika.
 
Mke wa kwanza alipata mtu akamwambia kuwa nakuacha.
Wa Pili alioa akiwa mentally unfit Tena single mama watt watatu .ama hujaelewa. Nesi alimuelewa pia nadhani.

Narudia kusema Kama kila siku kuwa wanaume tuko vizuri Ni mbususu ndio zinazotuangusha Basi. Yaani ikiwepo dawa ama kidonge unameza miaka mitano huna hisia unaweka Mambo yako sawa tungekuwa sawa. Niko primary namuomba Mungu anisaidie niende boarding school wanaume. Namshukuru nilipata hitaji langu
Asante kwa umakini wako

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Ila jamaa huyu Ni mpambanaji mno Nina Imani na wewe utatoboa.

Yaani aliyekuchomea kwa aliyekubinafishia labda alitaka aibe mbinu unazotumia.


Ila binadamu Ni wanyama kiasili.


Naomba tuwe tunabadilishana mawazo Kama hutojali your no kwa pm yangu.

Naona kwa mbali Kuna vinasaba vinashabihiana.


Ama hapa watu watahisi kuwa Kuna upigaji labda ama.


Ila let us be close, just kwa phone tu I can see Kuna something ahead
Poa mkuu nitakutafuta

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Tabu Ninayopata kutoka kwenye familia yangu -25

Tulivyorudi nyumbani nikamueleza baba mwanzo wa matatizo yote ,nikamwambia baba ngoja tu nitafute mwanamke mwingine nioe ,baba akaniambia ngoja ataongea nae

Basi baadae baba akamuita tukaanza kuongea basi akaonekana ameelewa ,baadae nikaingia ndani kunywa dawa akanipa dawa vizuri nikameza

Baadae akaniambia naomba uoe mwanamke mwingine ili akusaidie si unaona unaumwa , akaniambia kwani tokea nimekwambia hivi hujawahi kufanya maandalizi ya kutafuta mtu ,nikamwambia nilitafuta lakini bado hajanielewa ,basi akaniomba namba ya simu ya huyo Dada wakaongea kwamba ameruhusu Mimi nimuoe ,yeye atakuwa mke mkubwa halafu mwenga atakuwa mke mdogo

Baadae alivyomaliza kuongea nae akanisisitiza kwamba nihakikishe naoa ,kesho yake akawa ameondoka kurudi kazini

Baadae Mimi nikamwambia baba uyu mwanamke naona hanitaki Tena ,basi yule mke wangu alikuwa anakaa na mtoto wa shangazi yake ,Sasa uyo binti akanipigia simu akaniambia yule Dada yake siku hizi anamtu waga anakuja kulala pale nyumbani aise niliumia sana

Basi baadae baba aliondoka Mimi nikabaki pale na braza na wale watoto wa Dada yangu ,baadae nikafanya process ya kumuoa yule mwanamke ,niliona nichague mtu ambae hajasoma

Bado ndoa changa nikapata uhamisho wa kuhamia wilaya ingine uhamisho kutoka kwa RAs ,basi mke wangu alivyosikia nimeoa ndio ikawa tiketi ya kuniacha

Akawaambia kwao kwamba amenikuta nimeshaoa ndio maana ameamua kuniacha ,kumbe ile kunilazimisha kuoa alitaka apate sababu ya kuniacha

Unajua Kuna kipindi kaka yangu mtoto wa mama mkubwa alijiua kwa sababu mke wake ambae alizaa nae watoto wawili alimkataa ,japo nilikuwa nahuzunika lakini nilikuwa nishangaa ni kwa Nini braza ajiue wakati wanawake wapo wengi


Aise usiombe ikakukuta yaani hauoni another option Zaid ya hiyo ya kujiua ,

Yule mwanamke niliemuoa alikuwa single mother wa watoto watatu ,nae sijui alikuwa na mental trauma alikuwa ni mkorofi sana anapenda kugombana yaani ukimkosea kidogo tayari makofi
Sasa nikaona uyu tunaweza Kuna kuumizana tulibahatika kupata nae mtoto mmoja wa kike ,lakini baadae ilibid niachane nae

Mwaka huu nimeoa mke mwingine naomba mungu sana anijaalie nidumu na uyu,

Baadae yule mke wangu wa kwanza alinitafuta na kuniomba msamaha ilikuwa bado sijaoa uyu wa tatu lakini nikaona haina haja ya kuwa na mtu asie na msimamo

Ndio maana nikaona nioe tu mtu mwingine

Sasa tabu ninazopata kutoka kwenye familia yangu ni ;-

1 wazazi na ndugu hawaniongelei vizuri pindi ninapo oa ,mke wa kwanza waliongea Mambo mengi sana hasa mama

2-hata ukitoa msaada hawathamini siku ukiombwa na ukawa huna basi ni maneno mabaya mabaya wanakuongelea

3- mama Sasa hivi ameshazeeka lakini bado anang'ang'ania kufanya zile shughuli za uvuvi Kila siku ni kupoteza pesa ,anahitaji nimnunulie mashine lakini Mimi naona ameshachoka halafu Kuna wadogo zangu wapo chuo nikinunua hiyo mashine nitashindwa kuwasapoti

4 - nimeoa mke wa tatu ,mama alitoa maneno mabaya sana but Sina Cha kufanya Zaid ya kumshukuru mungu

Kule nilipohamishwa nilitengeneza mazingira mazuri sana lengo langu ni kufungua kampuni
Ambayo itakuwa ina deals with

1 .Agroproduction (kilimo na ufugaji )
Yaani na Lima nafuga pia nakuwa na mashine za kusanga na kukoboa halafu nafunga kwenye viroba nauza

2.viwanda vidogo vidogo kama mikate na mashine ya kuprocesa ngozi

3.usagirishaji (magari ya abiria

4.duka la dawa , zahanati na maabara

5.maduka ya jumla

6 .magari ya mizigo

Naamini nitafanikiwa kwa sababu naona kabis siwezi kubadili maisha yangu kwa kazi za kuajiriwa Tena humu serikalini kulivyo na changamoto

Ndio hivyo ndugu zangu ,naombeni ushauri wenu nifanye Nini ili niweze kufikia malengo yangu

Dunia tunayoenda nayo ni ngumu sana

Mwisho



Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

The risen and fallen of the bravo [emoji1490] man..


Wanawake ni mashetani fullstop...

Ungekua pekee yako toka mwanzo ndoto zako zingekamilika vizuri kabisa
 
Chief

Kwanza pole Sana Kwa changamoto ulizopitia

Mosi, kama walivyosema baadhi ya wadau nadhan biashara ya huduma za afya ingekufaa Sana ukichukulia uzoefu ambao uliupata dar na ulifanikiwa Sana,hivyo hauanzi na kitu kipya.

Pili,nimependa wewe ni famili man,na ni Jambo zuri Sana la kuoa,na hata kama bahati mbaya huyu mke akizingua usiseme Sito oa tena,hapana ndoa ndio kila kitu,ndio tulizo la nafsi na ndio umbile tulilo umbiwa na Allah, Ila usiwe mpole Sana Kwa mkeo,hakikisha nidhamu ya nyumba inachukua mkondo wake la sivyo utapandwa kichwani,kumbuka wanawake ni watu WA ajabu Sana,anaweza sikia mwenzake anakoromewa na mumewe akajikuta anatamani kuwa na mwanaume mwenye mamlaka anayeweza kusimama kama mwanaume.

Mwisho, fanya biashara zote lkn ya magari ya abiria ni pasua kichwa Sana,kama ukitaka kuwa na stress basi fanya hiyo biashara Yani hata ukiwa kibonge hauhitaji kupunguza uzito Bali stress za kuyafuatilia ni dawa tosha ya kupunguza uzito, kifupi inahitaji usimamizi WA karibu Sana, nimewahi kuwa na uzoefu huo kupitia mradi WA familia,kwahiyo najua hizo changamoto vizuri Sana. Na hata ukifanya tafiti Kwa wenye biashara hizo kama watakuwa wakweli kwako watakwambia Hali halisi.

Wewe ni mpiganaji na Kikubwa huna Maisha ya anasa na starehe hivyo future nzuri inaonekana.

Kila la kheri.
 
Mi naona una nyota ya biashara bora ungebaki Dar au utafte mtaji ukafungue ofisi Dar,utoke vijijin utatoboa mapema,kosa ulilofanya mwanzo hukua na mlinzi thus why, yule nes alipata mwanya wa kuingia ndani na kufanya vitimbwi,ungekuwa umetoa order kwa mlinzi, kuwa haruhusiwi kuingia ,angeishia getini,. All in all, nimegundua kuwa mimi nna roho ngumu sana, yaani jasiri mno..maana nilishapitia maswahibu km hayo kazin(lakini kada nyingine) ,jumlisha mahusiano,mixer ndugu, lakini nilisurvive.bila kupelekwa milembe,ngoja nijipepige kifuani mara tatu ,aisee mimi ni jembe..[emoji3]
 
Back
Top Bottom