TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.
Bora waende. Ni aibu kuendelea kupokea msaada wa ARVs pamoja na condoms. Magufuli na regime yake sasa wafill hili gap. Hakuna namna nyingine

Wee unasemaje, yaani akili zako kama za mjinga mmoja ambaye akili yake haifiki hata robo kilo. Unahisi wakijitoa itakuwaje kwa wagonjwa wanaohitaji hizo dawa.

Anyway nisikulaumu sana huenda usijue mambo yalivyo kwenye huduma za kiafya kwenye vituo vya kutolea huduma hasa hizi dawa za kufabaza VVU.
 
Nasema hivi: hamuwezi kuwa mnagongana daily harafu mnasubiri beberu aje kuwapa condoms na ARVs bure. Kama mnaweza kununua ndege kwa cash money, mnaweza kulipia condoms ninyi[emoji846]

IMG_4980.jpg

KUNA UJUMBE WAKO HAPA
 
Usishangilie ujinga

Jiupushe na ngono zembe ukizingatia yakuwa na mwenza mmoja muaminifu,

Fanya mazoezi Mara kwa Mara na zingatia kula mlo kamili pamoja na matunda,

Fanya kazi kwa juhudi kusaidia familia yako na taifa lako la Tanzania kukamilisha lina simama imara,

Linda usalama wako na wa mwenzako ili kuhakikisha nchi yako Tanzania inabaki salama kiafya na mazingira.
 

Moshi. Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
USITUTISHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Yeye sasa si kashikilia koba la hela hazina 😂 atajiagizia tu hata boksi 100! Shida ipo kwa raia ambao walishasahau kwamba kuna kirusi cha miwaya
Kama aliweza kupeleka ndege Madagascar, hili kwake ni dogo. Hapo South Africaetu kuna pharmacy za watu binafsi wana supply ya moja kwa moja kutoka Ulaya na Marekani.
 
Kama aliweza kupeleka ndege Madagascar, hili kwake ni dogo. Hapo South Africaetu kuna pharmacy za watu binafsi wana supply moja kwa moja kutoka Ulaya na Marekani.
Hahahahah kwamba awaagizie na nyie😂!!! Nikikumbuka "Serikali haijaleta tetemeko" huwa nawaza deep sana.
 
Wee unasemaje, yaani akili zako kama za mjinga mmoja ambaye akili yake haifiki hata robo kilo. Unahisi wakijitoa itakuwaje kwa wagonjwa wanaohitaji hizo dawa.

Anyway nisikulaumu sana huenda usijue mambo yalivyo kwenye huduma za kiafya kwenye vituo vya kutolea huduma hasa hizi dawa za kufabaza VVU.
Hali ikoje huko field mkuu?
 
Hili jambo ni hatari sana

Ukweli ni kwamba hizi ARV zimesaidia sana kupunguza maambukizi hasa kwa sababu watu wanaanza kutumia mapema. Sasa zikikosekana tutaanza kutafutana hapa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom