TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.
Kama aliweza kupeleka ndege Madagascar, hili kwake ni dogo. Hapo South Africaetu kuna pharmacy za watu binafsi wana supply ya moja kwa moja kutoka Ulaya na Marekani.
✓[emoji769] Mzungu kakasirika. Afanyi bihashara kichaaa kama mchina anauza dawa kwa South Africa people kwa kujua idadi ya wagonjwa na ndio aliposhikilia rungu la kuziazibu nchi za Africa na sehemu zingine.
 
Hili jambo ni hatari sana

Ukweli ni kwamba hizi ARV zimesaidia sana kupunguza maambukizi hasa kwa sababu watu wanaanza kutumia mapema. Sasa zikikosekana tutaanza kutafutana hapa
✓[emoji769] Yaani iyo kauli, baada ya kuongea tuuuu, uwezi kukuta dawa inapatikana kirahisi rahisi itapatikana kwa wenye fedha zao tuuu na viongozi, maaskari na madaktari. Hiii itakuwa dawa kupatikana kama dawa za kulevya
 
Sisi ni matajiri hakuna shida, tunajenga SGR, Bwawa kubwa la kufua umeme wa megawati 2000+, tumenunua ndege 11, mbali na ujenzi wa vituo vya afya, nk hivi vyote ni fedha za ndani nini dawa za magonjwa nyemelezi!!

Maboko awe makini kusema ni miaka miwili tu
Zile Bilioni 27,mlizoomba EU zilikuwa za nini km kweli mna huo uwezo?.
 
Moshi. Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
Magufuli oyeeee
 
MATAGA wanafikiri CHADEMA ndio watadhurika, kumbe nao ndio watumiaji wakubwa ARV .
 
Hali ikoje huko field mkuu?

Hali ni njema ila sehemu kubwa ya Dawa hizi hupatikani kupitia mifuko ya wahisani kama hao USAIDS na UK AIDS na mashirika mengine. Sasa kama wahisani wanajitoa unadhani itakuwaje juu ya upatikanaji wa dawa Mkuu. Na kuna kipindi baadhi ya wagonjwa walikuwa wanakosa hizi za dawa za magonjwa nyemelezi na baadhi uwezo wao kifedha haukua mzuri kitu kilichopelekea baadhi ya wagonjwa kutoonekana tena kwenye vituo kuja kuchukua dawa ambayo inaacha maswali labda huyu mtu alivuta au alihama kituo.
Lakini hoja yangu hasa ni kwamba, wahisani hawa tunaowaita mabeberu wamekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu hasa watu wanao ishi na VVU. Sasa hizo dawa zikianza kukosekana kwa msaada maana yake anapaswa ajinunulie mwenyewe. Ni changamoto kubwa sana na ukizingatia watu hawa baadhi yao Afya zao zinakuwa zimedhoofika hata kazi za kujiingizia mia mbili mia tatu wengine wanakuwa hawawezi . Mungu aibariki Tanzania na viongozi wake.
 
Hatuwezi kupoteza utu wa wananchi wetu kisa misaada, Tz ni nchi huru hatujawahi kushindwa ktk vita yoyote, wapeleke kule misaada yao!
 
Wee unasemaje, yaani akili zako kama za mjinga mmoja ambaye akili yake haifiki hata robo kilo. Unahisi wakijitoa itakuwaje kwa wagonjwa wanaohitaji hizo dawa.

Anyway nisikulaumu sana huenda usijue mambo yalivyo kwenye huduma za kiafya kwenye vituo vya kutolea huduma hasa hizi dawa za kufabaza VVU.
Anafikiri kila mtu mwenye VVU alijitakia kwa ngono zembe. Wengine maskini hata hatia hawana wamezaliwa tu wanayo. Alafu mtu anakuja kuongea ugoro huku bila kufanya uchunguzi
 
Hii habari njema, UKIMWI ulijisahau umezoeleka sana... endeleeni tu kusafisha mitaro na kujivunia vumbi la Kongo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom