TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.

Summary​

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.
janet josephpic

By Janeth Joseph

Moshi. Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya vVirusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

By gazeti la Mwananchi online
 
Sisi ni matajiri hakuna shida, tunajenga SGR, Bwawa kubwa la kufua umeme wa megawati 2000+, tumenunua ndege 11, mbali na ujenzi wa vituo vya afya, nk hivi vyote ni fedha za ndani nini dawa za magonjwa nyemelezi!!

Maboko awe makini kusema ni miaka miwili tu
"Awe makn kusema MIAKA miwili tuu" [emoji848][emoji2955][emoji2955][emoji2955]
Kwann ?
Limeivaa
 
Ni hivi,kama Corona ilivoyeyuka,serikali yetu tukufu inaenda kuuondoa huu ugonjwa ndani ya miaka mitano
Tegemeeni kupungua kwa takwimu kila mwaka....mitano tena.
 
Malukanga dawa yake ni kutokua na mpenzi na mwanamke yeyote yule, piga punyeto hadi siku ya kufa kwako. Mbona rahisi tu. Ukijifanya shingo feni unaenda na maji.
 
Bora waende. Ni aibu kuendelea kupokea msaada wa ARVs pamoja na condoms. Magufuli na regime yake sasa wafill hili gap. Hakuna namna nyingine
Mkuu unajua dozi ya ARV kwa mwezi inagharimu kiasi gani?? Hata CCM hawako pamoja na wewe kwenye suala hili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom