TAESA imekuwa ni janga kubwa la kukata ndoto za vijana. KwaniniSerikali (PSRS) isianze na vijana wa TAESA kwanza kwa uzoefu walio nao?

Wamenipa mkataba wa Tanga uwasa na mshahara wa 500k
 
Wamenipa mkataba wa Tanga uwasa na mshahara wa 500k
Umeona mkuu safi kila.la.heri chapa kazi sanaa kama.mjinga tanga uwasa wanaweza wakakkubakisha mind you taesa ni only one year kwahyo jenga uhusiano mzur na tanga uwasa ili mkataba wa taesa ukiisha ubaki hapo
 
Umeona mkuu safi kila.la.heri chapa kazi sanaa kama.mjinga tanga uwasa wanaweza wakakkubakisha mind you taesa ni only one year kwahyo jenga uhusiano mzur na tanga uwasa ili mkataba wa taesa ukiisha ubaki hapo
Kweli mkuu maana mkataba wa Tanga uwasa umesema wanauterm as probation period so wanaweza nibakiza Ngoja tukomae
 
Nimejisajili nimetumiwa message nimekua verified lakini sijapewa registration number nimeenda office zao wameniambia ni mfumo nisubiri jamani nifanye ninauhitaji wa internship
 
Nimejisajili nimetumiwa message nimekua verified lakini sijapewa registration number nimeenda office zao wameniambia ni mfumo nisubiri jamani nifanye ninauhitaji wa internship
Wenye mamlaka wamekwambia usubiri system ikae sawa, harafu wewe unakuja huku unatuuliza ufanyeje
FANYA KUFUTA TU HIYO ACCOUNT
 
Relax kila kitu kipo kwa system , utapewa reg no na uta book training na interview ..
Hahahha hata siis tuna uhitaji na bado hatujui lini tutaitwa ..kikubwa labda una connection
 
Kama tunavofaham, TaESa chini ya ofisi ya waziri Mkuu wanajitahidi sehemu kubwa kuwaunganisha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini katika nafasi za ajira na internship. Hasa internship kwa ajili ya kuwapatia vijana uzoefu wa kazi ukizingatia waajiri wengi siku hizi wanataka watu wenye uzoefu. Hivyo bas, vijana wengi wanaomaliza mtaani na kujiunga na mfumo wa TaESa, ikitokea amepata nafasi ya intern, anatoka mtaani hana chchote na kuripoti kituo alichopangiwa na anataraji POSHO atakayopewa imesaidie kwenye mahitaji muhimu.

SHIDA kubwa inayotatiza kwa vijana wengi wa intern kupitia TaESa, wanacheleweshewa sana malipo, Malipo yanachukua wiki mbili na Zaid baada ya mwezi kuisha pengine hadi miezi miwili inaisha pasina kuipata. Hivyo basi, vijana hujikuta wanaishi maisha magumu sana wengine kujaa madeni na posho kuisha kwa madeni kabla ya kuipata. Na wengine pia kwa sababu ya kucheleweshewa POSHO, huamua kuvunja mkataba na kuonelea bora akafanye hata kazi zingine.
Hili tatizo ni hasa kwa vijana wa TaESa kanda ya Ziwa kwa kanda zingine sifahamu.

Kwa mfano, mpaka kufikia tarehe 17/10/2023, TaESa ilikuwa bado haijaingiza POSHO ya intern ya mwezi wa tisa (9). Na ukizingatia vijana wamejitolea na hawana wanachotegemea Zaid ya hiyo posho.
Mmoja katika watumishi wa serikali kanda ya ziwa alisema, nanukuu

"TaESa siku hizi katika utawala wa awamu ya sita wanachelewesha sana malipo sijajua ni kwa nini ukilinganisha na awamu tano, walikuwa wakilipa kwa muda muafaka sijajua kwa nini imekuwa hivi" alisema.

Ombi langu ni kutaka kujua, Je, Ofis ya waziri Mkuu kama msimamizi mkuu, inalifahamu hili? Hatua zipi imechukua au kuna tatizo gani kwa TaESa kanda ya ziwa kuhusu Malipo kwa intern?
Au ni nini hasa kinaendelea? Mana vijana wanajitolea sana na wapo tyar kufanya intern tena wengi ili wapate uzoefu japo ni POSHO kiasi kidogo sana kama 150000. Lakin suala la kuchelewa kuwalipa POSHO kwa muda mrefu linawaumiza na kuwafanya kuishi maisha magumu na pengine kukata tamaa kuendelea na internship na kuamua kuvunja mkataba.


Ahsanteni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…