Kama tunavofaham, TaESa chini ya ofisi ya waziri Mkuu wanajitahidi sehemu kubwa kuwaunganisha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini katika nafasi za ajira na internship. Hasa internship kwa ajili ya kuwapatia vijana uzoefu wa kazi ukizingatia waajiri wengi siku hizi wanataka watu wenye uzoefu. Hivyo bas, vijana wengi wanaomaliza mtaani na kujiunga na mfumo wa TaESa, ikitokea amepata nafasi ya intern, anatoka mtaani hana chchote na kuripoti kituo alichopangiwa na anataraji POSHO atakayopewa imesaidie kwenye mahitaji muhimu.
SHIDA kubwa inayotatiza kwa vijana wengi wa intern kupitia TaESa, wanacheleweshewa sana malipo, Malipo yanachukua wiki mbili na Zaid baada ya mwezi kuisha pengine hadi miezi miwili inaisha pasina kuipata. Hivyo basi, vijana hujikuta wanaishi maisha magumu sana wengine kujaa madeni na posho kuisha kwa madeni kabla ya kuipata. Na wengine pia kwa sababu ya kucheleweshewa POSHO, huamua kuvunja mkataba na kuonelea bora akafanye hata kazi zingine.
Hili tatizo ni hasa kwa vijana wa TaESa kanda ya Ziwa kwa kanda zingine sifahamu.
Kwa mfano, mpaka kufikia tarehe 17/10/2023, TaESa ilikuwa bado haijaingiza POSHO ya intern ya mwezi wa tisa (9). Na ukizingatia vijana wamejitolea na hawana wanachotegemea Zaid ya hiyo posho.
Mmoja katika watumishi wa serikali kanda ya ziwa alisema, nanukuu
"TaESa siku hizi katika utawala wa awamu ya sita wanachelewesha sana malipo sijajua ni kwa nini ukilinganisha na awamu tano, walikuwa wakilipa kwa muda muafaka sijajua kwa nini imekuwa hivi" alisema.
Ombi langu ni kutaka kujua, Je, Ofis ya waziri Mkuu kama msimamizi mkuu, inalifahamu hili? Hatua zipi imechukua au kuna tatizo gani kwa TaESa kanda ya ziwa kuhusu Malipo kwa intern?
Au ni nini hasa kinaendelea? Mana vijana wanajitolea sana na wapo tyar kufanya intern tena wengi ili wapate uzoefu japo ni POSHO kiasi kidogo sana kama 150000. Lakin suala la kuchelewa kuwalipa POSHO kwa muda mrefu linawaumiza na kuwafanya kuishi maisha magumu na pengine kukata tamaa kuendelea na internship na kuamua kuvunja mkataba.
Ahsanteni sana