Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Ufunuo 22:12?


  • Total voters
    131
  • Poll closed .
Yesu Anarudi Upesi na sasa tupo Kwenye Kanisa la mwisho linaitwa Laodikia,Kabisa la viguvugu. Yesu Atusaidie sana Kuwa na Mwisho Mwema
 
-Anakuja kutokea wapi ..?
-Alipoondoka ulimuona..?
Anakuja kutokea mbinguni alikokwenda kutuandalia makao. Kabla hajapaa mbinguni alisema:
Yohana 14:2-3 SRUV
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.

New English Translation: There are many dwelling places in my Father’s house. Otherwise, I would have told you, because I am going away to make ready a place for you. And if I go and make ready a place for you, I will come again and take you to be with me, so that where I am you may be too.

Alipoondoka Mitume walimuona na malaika walitokea kuelezea tukio hilo
Mdo 1:9-11
Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili[malaika] wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

1 Wathesalonike 4:16-17
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
 
Hakija siku parapanda itakapo lia tanzania wengi waliokuwa na jezi za chama cha ccm na mashabiki hawata paaa kwenda mbinguni.

Watakimbilia ofisi zao chama kuwauliza mbona tumeshindwa kupaa.
Sababu ni uwongo na hamna akili
Tumuombe Mungu awasaidie wengi waamini, ili Yesu akija waweze kupaa
 
Inaaminika kwamba kitabu cha Ufunuo kiliandikwa mwaka 96 CE. Kwa muktadha huo, hata Yesu angerudi leo hawezi kuwa amerudi "upesi" wakati imeshapita miaka karibu 2000 tangu aseme hayo.
Kwa Bwana miaka elfu ni kama siku moja (2 Petro 3:8-9)
Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili...kwa Bwana...miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali anawavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote watubu.

Yesu alipaa mbinguni takriban mwaka 33 BK.
Huu ni mwaka 2025, hivyo tunaweza kusema amekaa mbinguni kwa miaka 1992

Tukibadili hiyo miaka kuwa siku (kwa mujibu wa 2 Petro 3:8), miaka 1992 duniani ni sawa na siku 1.992 (1992÷1000 = 1.992)

Kwahiyo tangu Yesu apae mbinguni hadi sasa Machi 2025, amekaa mbinguni kwa takriban siku 1.9 tu!

Hii inaendana na unabii wa Hosea 6:2
Baada ya siku mbili atatufufua...

Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba kuja kwa Yesu sio jambo la mbali, tuko karibu sana na siku ya pili, aliyoinena Nabii Hosea, ambayo wengi wanaamini ni wakati wa kuja kwa Yesu!

Kwa hesabu hiyo na kwa unabii huo wa Hosea, ni wazi Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Ufunuo 22:12, kwakuwa atakuwa amekaa mbinguni siku 2 tu!

Hatujui siku wala sasa ya kuja kwake. Tunachotakiwa tu ni kukesha maana kwa siku na saa tusiyodhani, Yesu atakuja(Mathayo 24:42).

Kukesha ni kuhakikisha tunaishi maisha matakatifu na kujiepusha na usingizi wa kiroho(Ebr 12:14).
 
Bila shaka na wasiwasi wowote naamini yu aja upesi yesu kristo mnazarethi...
Kulingana na mafundisho ya imani yangu pamoja dalili za ujio wake kitqbu cha ufunuo: zishaanza kujionesha hivyo tuishi katika utqkatifu/sala/toba ya kweli kila wakati. Amen!
Amina Johnie2323
 
Unataka kubishana naye?
Nope. Nataka kujua Atheists ni wangapi humu. Kama ni wengi niongeze "gia" ya kuwaombea Mungu awaokoe, maana Mungu hapendi wapotee bali waifikie toba.
 
Uthibitisho!
jamiiforums #JFKUMBUKIZI: Mwaka 2008 Waumini

51 wa Dhehebu la Wasabato Masalia, walianzisha kambi katika maeneo ya Tabata baada ya kuzuiwa na kufukuzwa zaidi ya mara 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakita kusafiri kwenda Ulaya kuhubiri Injili bila hati yoyote ya kusafiria huku wakidai wameagizwa na Mungu

Wakiwa Tabata, Waumini hao waliokuwa 17 na kuongezeka hadi 51 walikumbana na hali ngumu ya Maisha, (hivyo kugeuka ombaomba), pia walikuwa wakiugua hawaendi Hospitali kwa kudai "Mungu atawaponya". Majirani walilalamikia uchafuzi wa Mazingira na kero ya kuombaomba

Imeelezwa, 24 kati yao walihukumiwa kwenda jela Mwaka 1 baada ya kuvamia eneo la Watu, lakini hata walipokuwa wakipelekwa gerezani, bado walisema, "Hii ni safari pia na Mungu ana mipango yake."

Mdau, kipindi tukio hili linatokea ulikuwa wapi?
Source: JamiiForums
 
Back
Top Bottom