Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Ufunuo 22:12?


  • Total voters
    131
  • Poll closed .
Kuna watu bado wanaamini yesu alipaa mbinguni na ipo siku atarudi?!!! Amaa kweli imani za dini ni sawasawa na uraibu wa madawa ya kulevya
 
simuoni yesu ndani ya miaka mia nene ijayo labda ndo swali liulizwe
 
2040
Mnaweza msitoboe hapa duniani.
Hatujui yatakayojiri 2040.
Yesu akirudi kabla ya mwaka huo uko tayari kunyakuliwa? Kama bado, tubu dhambi zako sasa na umwamini Yesu, usije ukaachwa. Baada ya Yesu kuja na kuwachukua watakatifu, watakaoachwa duniani wataingia katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
 
Mwaka wa 2000 tuliambiwa hivihivi hadi wengine wakafilisika kwa kuacha kujishughulisha wakimngoja mwana wa Mungu lakini haikutokea.

Inakuaje Mungu na kiumbe wake mpendwa Mh lusifa wasikae mezani wakatumia diplomansia badala ya nguvu?
Pet 3:3-13
Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkiingojea hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
 
Yesu alisharudi kitambo tu mbona ?
Bado.
Waliokuja ni Makristo wa uongo
Mathayo 24:5
"Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi."
 
Aje kutoka wapi??
Anakuja kutoka mbinguni alikokwenda kutuandalia makao.

Kabla hajapaa mbinguni alisema:
Yohana 14:2-3 SRUV
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.

New English Translation: There are many dwelling places in my Father’s house. Otherwise, I would have told you, because I am going away to make ready a place for you. And if I go and make ready a place for you, I will come again and take you to be with me, so that where I am you may be too.

1 Wathesalonike 4:16-17
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
 
Angekuwepo kweli angesharudi kitambo kabla hata miaka ya leo haijatimia, bahati mbaya sana huyo Yesu hayupo na hajawai kuwepo, maana ni kama storie's character aliyeundwa na wazungu acheze uhusika wa story ya maandiko ya biblia kipindi kile cha uroma na ukatolic wao.

Narudia tena, kusubiri mtasubiri sana, yesu hatorudi, maana hayupo, atarudije kama uwepo wake haupo.

Ushahidi wa uwepo wake haupo kihistoria ktk nakala, wala kisayansi vile vile.

Mnapoteza muda wenu kuamini upuuzi wa wazungu+waarabu
Mkuu, ni muhimu kuchunguza mambo kwa kina kabla ya kuyakataa moja kwa moja.

Ushahidi wa kihistoria kuhusu Yesu haupo tu kwenye Biblia bali pia katika maandiko ya kihistoria kutoka kwa waandishi wa Kirumi na Kiyahudi wasiokuwa Wakristo, kama Tacitus, Josephus, na Pliny the Younger. Wote hawa waliandika habari zinazomhusu Yesu na wafuasi wake katika karne ya kwanza. Kama Yesu angekuwa hajawahi kuwepo, ni kwa nini waandishi hao wa historia wamemtaja?

Yesu sio "story character" iliyoundwa na Wazungu. Ukristo haukuanzishwa na Wazungu bali na Wayahudi wa Mashariki ya Kati. Yesu mwenyewe alikuwa Myahudi aliyeishi katika Israeli (eneo la Palestina), na Injili ilianza kuhubiriwa huko. Ukristo ulienea Ulaya baadaye, lakini asili yake si ya wazungu.

Yesu hajaja bado kwa sababu hapendi mtu yeyote apotee; hivyo anaendelea kutoa muda watu wote wapate nafasi ya kutubu (2 Petro 3:9). Hata hivyo hajachelewa kuja kama wengine wanavyodhani. Kuna member nimeishamjibu swali hilo, naomba ufuatilie replies zangu. Nimeeleza kwa undani kwamba tangu Yesu apae kwenda mbinguni zimepita kama siku 1.9 tu. Kwa sababu kwa Bwana, miaka elfu ni kama siku moja.

Sayansi inashughulika na mambo yanayopimika kwa vipimo vya kibinadamu, lakini haimaanishi kwamba mambo yasiyoweza kupimwa moja kwa moja hayapo. Kuna mambo kama upendo, maadili, au hata historia yenyewe ambayo hayawezi kupimwa katika maabara, lakini bado ni halali na ya kweli.

Wanaomwamini Yesu hawapotezi muda bali wanajiandaa kwa maisha ya milele. Tafakari kwa kina ndugu, suala hili. Siku utakapogundua Yesu yupo wakati umechelewa kumwamini, utafanya nini? Kumbuka, wasiomwamini, watatupwa motoni milele.
 
jamiiforums #JFKUMBUKIZI: Mwaka 2008 Waumini

51 wa Dhehebu la Wasabato Masalia, walianzisha kambi katika maeneo ya Tabata baada ya kuzuiwa na kufukuzwa zaidi ya mara 3 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakita kusafiri kwenda Ulaya kuhubiri Injili bila hati yoyote ya kusafiria huku wakidai wameagizwa na Mungu

Wakiwa Tabata, Waumini hao waliokuwa 17 na kuongezeka hadi 51 walikumbana na hali ngumu ya Maisha, (hivyo kugeuka ombaomba), pia walikuwa wakiugua hawaendi Hospitali kwa kudai "Mungu atawaponya". Majirani walilalamikia uchafuzi wa Mazingira na kero ya kuombaomba

Imeelezwa, 24 kati yao walihukumiwa kwenda jela Mwaka 1 baada ya kuvamia eneo la Watu, lakini hata walipokuwa wakipelekwa gerezani, bado walisema, "Hii ni safari pia na Mungu ana mipango yake."

Mdau, kipindi tukio hili linatokea ulikuwa wapi?
Source: JamiiForums
Haha sawa Mkuu,nimekumbuka,tupo pamoja!
 
Zipi hizo ambazo ni mpya hazijawai kuwepo? Maana kama matukio mabaya ya kutisha yalishakuwepo tangu zamani na huenda mabaya kuliko hivi leo kipindi cha ustaarabu.

Dini ni upofu wa akili kuamini upuuzi
Ni kweli kwamba mambo mabaya yamekuwa yakitokea tangu zamani. Vita, magonjwa, majanga, na dhuluma si mambo mapya. Lakini mambo hayo yanazidi kuongezeka kwa ukubwa na kasi.

Kwa mfano, Yesu alisema dalili mojawapo ya kurudi kwake ni magonjwa mabaya(pestilences). Huoni jinsi ongezeko la magonjwa mabaya lilivyo sasa? Vipi kuhusu matetemeko ya ardhi (Mathayo 24:7).

Yesu alisema hayo yatakuwa kama utungu wa kujifungua (Mathayo 24:8), yaani, yataongezeka kwa nguvu na kasi kadri siku zinavyosogea. Yesu alisema maasi yataongezeka. Tunaona leo, kwa mfano, mizozo ya kimataifa inaongezeka kwa kiwango kisichowahi kushuhudiwa.

Hata hivyo kuna dalili maalum za nyakati za mwisho ambazo hazikuwepo zamani kwa kiwango cha leo:

Kwa mfano, sasa hivi kuna teknolojia inayowezesha udhibiti wa dunia nzima – Biblia inasema wakati wa mpinga Kristo, kutakuwa na mfumo wa kimataifa wa kudhibiti uchumi (Ufunuo 13:16-17). Leo, mifumo ya kidijitali na benki za kidunia zinaelekea huko.

Kuporomoka kwa maadili na ongezeko la dhambi – 2 Timotheo 3:1-5 inazungumzia jinsi watu wa siku za mwisho watakavyokuwa wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Leo hii, mambo yaliyoonekana kuwa mabaya zamani(kama ushoga) yanasifiwa waziwazi.

Injili kuufikia ulimwengu wote – Yesu alisema injili itahubiriwa duniani kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo mwisho utakapokuja (Mathayo 24:14). Leo, kwa teknolojia za mitandao ya kijamii, injili inafikia maeneo ambayo zamani haikuweza kufika.

Ilitabiriwa tena kwamba watu watabeza ahadi yake ya kurudi.
Katika kitabu cha 2 Petro 3:3-4 imeandikwa kwamba katika siku za mwisho, watu watasema: "Iko wapi ahadi ya kuja kwake?" Huoni na wewe tayari umetimiza unabii huo kwa sasa? Hii ni ishara yenyewe ya nyakati za mwisho!

Je, dini ni upofu wa akili? La hasha. Watu mashuhuri waliodhani Ukristo ni udanganyifu, kama atheists wakubwa C.S. Lewis na Lee Strobel, walipoichunguza Biblia kwa kina, walikiri kuwa ushahidi wa kuwepo kwa Yesu ni wa kweli.

Kwahiyo ndugu, usikubali kudanganyika. Kataa hoja za kina Kiranga, zitakupoteza.

Naomba Mungu akuwezeshe kuujua ukweli huu. Ubarikiwe sana.
 
Ukifikia kwenye hatua ya kupiga Kura kuhusu Yesu/Mungu basi hujui unachokiamini
 
Hehehehehehehehehehehehehehehehe!!!
Usimcheke. Huyo ni wa kuombea sana maana ni vuguvugu. Hatari ya kuwa vuguvugu imeandikwa katika Ufunuo 3:16 SRUV
Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
 
Imani ya mtu si yakupigiwa kura,
Hii Poll ni nafasi ya watu kueleza mitazamo yao. Yesu mwenyewe aliwauliza wanafunzi wake: ‘Ninyi mnasema mimi ni nani?’ (Mathayo 16:15). Usifikiri hakuwa na jibu, bali alitaka kila mmoja atafakari imani yake. Hali kadhalika, Poll hii ni fursa ya kila mtu kutafakari ahadi ya Yesu na msimamo alio nao mtu kuhusu ahadi hiyo ya kuja kwake.
fia mbele huko
Laana yako haiwezi kunipata. Utasubiri sana!
Mithali 26:2 SRUV
Kama shomoro katika kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpati mtu.
 
Back
Top Bottom