Zipi hizo ambazo ni mpya hazijawai kuwepo? Maana kama matukio mabaya ya kutisha yalishakuwepo tangu zamani na huenda mabaya kuliko hivi leo kipindi cha ustaarabu.
Dini ni upofu wa akili kuamini upuuzi
Ni kweli kwamba mambo mabaya yamekuwa yakitokea tangu zamani. Vita, magonjwa, majanga, na dhuluma si mambo mapya. Lakini mambo hayo yanazidi kuongezeka kwa ukubwa na kasi.
Kwa mfano, Yesu alisema dalili mojawapo ya kurudi kwake ni magonjwa mabaya(pestilences). Huoni jinsi ongezeko la magonjwa mabaya lilivyo sasa? Vipi kuhusu matetemeko ya ardhi (Mathayo 24:7).
Yesu alisema hayo yatakuwa kama utungu wa kujifungua (Mathayo 24:8), yaani, yataongezeka kwa nguvu na kasi kadri siku zinavyosogea. Yesu alisema maasi yataongezeka. Tunaona leo, kwa mfano, mizozo ya kimataifa inaongezeka kwa kiwango kisichowahi kushuhudiwa.
Hata hivyo kuna dalili maalum za nyakati za mwisho ambazo hazikuwepo zamani kwa kiwango cha leo:
Kwa mfano, sasa hivi kuna teknolojia inayowezesha udhibiti wa dunia nzima – Biblia inasema wakati wa mpinga Kristo, kutakuwa na mfumo wa kimataifa wa kudhibiti uchumi (Ufunuo 13:16-17). Leo, mifumo ya kidijitali na benki za kidunia zinaelekea huko.
Kuporomoka kwa maadili na ongezeko la dhambi – 2 Timotheo 3:1-5 inazungumzia jinsi watu wa siku za mwisho watakavyokuwa wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Leo hii, mambo yaliyoonekana kuwa mabaya zamani(kama ushoga) yanasifiwa waziwazi.
Injili kuufikia ulimwengu wote – Yesu alisema injili itahubiriwa duniani kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo mwisho utakapokuja (Mathayo 24:14). Leo, kwa teknolojia za mitandao ya kijamii, injili inafikia maeneo ambayo zamani haikuweza kufika.
Ilitabiriwa tena kwamba watu watabeza ahadi yake ya kurudi.
Katika kitabu cha 2 Petro 3:3-4 imeandikwa kwamba katika siku za mwisho, watu watasema:
"Iko wapi ahadi ya kuja kwake?" Huoni na wewe tayari umetimiza unabii huo kwa sasa? Hii ni ishara yenyewe ya nyakati za mwisho!
Je, dini ni upofu wa akili? La hasha. Watu mashuhuri waliodhani Ukristo ni udanganyifu, kama atheists wakubwa
C.S. Lewis na
Lee Strobel, walipoichunguza Biblia kwa kina, walikiri kuwa ushahidi wa kuwepo kwa Yesu ni wa kweli.
Kwahiyo ndugu, usikubali kudanganyika. Kataa hoja za kina Kiranga, zitakupoteza.
Naomba Mungu akuwezeshe kuujua ukweli huu. Ubarikiwe sana.