Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Ufunuo 22:12?

  • Total voters
    131
  • Poll closed .
Yesu kuja ni bado sana.Ishi subiri ufe uje uchimbwe mafuta million years huko mbeleni.Dunia bado mbichiiii..
 
😂😂😂😂
 
Duh, aliyekuelewa anifafanulie hoja yako.
Namaanisha wengi wana taswira yao kichwani teyari ya Yesu na Mungu wao kutokana na mapokeo,ila Muumba alishasema akili yake haichunguziki.
 
Kwenye io dhiki itabidi wayatoe maisha yao KRISTO, ndio wataungana tena na walionyakuliwa.
 
Kwenye io dhiki itabidi wayatoe maisha yao KRISTO, ndio wataungana tena na walionyakuliwa.
Haitakuwa rahisi kihivyo. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza kuwa mapigo watakayoyapata yatakuwa mazito sana, lakini ajabu watu badala ya kuutubia uovu wao watazidi kumtukana Mungu!
 
Kwakuwa Hujasema Anakuja Wapi Nimekupa Kura ya Ndiyo
1 Wathesalonike 4:16 (SRUV)
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

Kwa Andiko hilo ni wazi atakuja duniani, lakini this time, hatakanyaga ardhini, badala yake ataishia mawinguni. Kufumba na kufumbua, waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kujiunga na wale watakaokuwa hai, kisha sote tutanyakuliwa na Yesu kwenda kwenye Arusi ya Mwanakondoo🙂

Wewe unafikiri atakuja wapi, Israeli?
 
Kwani Mbinguni Ni Wapi Ni mawinguni Au ni wapi?
Na Tukidhamlaki Tunaenda wapi??
Na Hilo Andiko la Kutokanyaga Ardhini umelipata wapi?

KULAKI maana Yake ni Kumpokea Yaani kama Nikienda Kumpokea Mgeni kama Rais akija kwangu Kinachofuata ni Kuleta Kwako..

Kwahyo baada ya kumlaki Itakuaje tena arudi alikotoka?

Na Kingine Baada ya Kunyakuliwa (Kuvutwa) kwenda Mawinguni Nini Kinafuata
 
Tahadhari tu. Kipindi hiki kina mashahidi wengi wa uongo na ushetani mwingi. Take care kujiingiza kupiga kura katika vitu ambavyo hujui msingi wake
 
Haitakuwa rahisi kihivyo. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza kuwa mapigo watakayoyapata yatakuwa mazito sana, lakini ajabu watu badala ya kuutubia uovu wao watazidi kumtukana Mungu!
Najua
Ila ukiisoma vizuri hicho kitabu pameelezea kuna watu baadhi watashinda.
 
Najua
Ila ukiisoma vizuri hicho kitabu pameelezea kuna watu baadhi watashinda.
Ni sawa. Hiyo itakuwa kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!
Halafu tena, issue kubwa ni hii, mtu anaweza akaiaga dunia kabla ya kuja kwa Yesu. Akiondoka katika hali ya dhambi, hapo hakuna tena uwezekano wa kutubu.
Ndio sababu tunambiwa "wakati uliokubalika ni sasa na siku ya wokovu ndio sasa."
 
2040
Mnaweza msitoboe hapa duniani.
mkuu nimekuwa nikiwaza sana jambo hili... naona kama hatuko mbali sana na ujio wa bwana.....nimesikia kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
 
kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
Ni kweli. Wako kwenye maandalizi. Kilichokuwa kinasubiriwa ni kupata ng'ombe wekunde wasio na doa kabisa.
The red heifer (Hebrew: פָּרָה אֲדֻמָּה,) was a reddish brown cow sacrificed by Temple priests as a purification ritual in biblical times.
Tayari ng'ombe hao wameishapatikana. Search youtube utaona video nyingi za habari za kupatikana kwa ng'ombe hao. Hizi zote ni ishara za kuja kwa Yesu, ila watu wanapuuza tu.
 
mkuu nimekuwa nikiwaza sana jambo hili... naona kama hatuko mbali sana na ujio wa bwana.....nimesikia kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
Sijafatilia ila kuna dalili za kuja kwake na dalili ya juja kwake, hapo kwenye za , zimeshatimia , naona imebaki moja ya .....
Chukio la uharibifu.
 
Tahadhari tu. Kipindi hiki kina mashahidi wengi wa uongo na ushetani mwingi. Take care kujiingiza kupiga kura katika vitu ambavyo hujui msingi wake
Wewe ni mgeni JamiiForums? Polls ni kitu cha kawaida kwenye forums na social media zote. Polls zina faida kubwa sana ila members wengi humu hawajajua jinsi ya kuzitumia.

Maelezo ya kupiga kura si yote yameandikwa?

Kinachokuogopesha ni nini?
 
Mimi ni kikongwe humu. Sijaogopa. nachukua tahadhari kwa mambo haya kiroho zaidi.
 
Atakuja kama jinsi mwizi ajavyo, "ghafla"
 
Sijafatilia ila kuna dalili za kuja kwake na dalili ya juja kwake, hapo kwenye za , zimeshatimia , naona imebaki moja ya .....
Chukio la uharibifu.
Tunamsubiria yule mnyama wa ufunuo(the beast)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…