Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Tafadhali sana piga kura yako hapa: Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi? Ndio au Hapana

Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Ufunuo 22:12?

  • Total voters
    131
  • Poll closed .
Yesu kuja ni bado sana.Ishi subiri ufe uje uchimbwe mafuta million years huko mbeleni.Dunia bado mbichiiii..
 
Usijiaibishe, mkuu. Anayepiga kura kuhusu Yesu ni nani hapa? Hii inaitwa Forum Poll
Kama hujui faida ya poll, ngoje nikumegee:
1️⃣ Encourages Engagement – Polls make discussions more interactive by encouraging users to participate and share their opinions.
2️⃣ Quick and Clear Feedback – Instead of long debates, a poll provides instant insights into what the majority of the community thinks.
3️⃣ Data-Driven Decision Making – Results help forum moderators or members understand trends, preferences, and opinions in an organized way.
4️⃣ Sparks Further Discussion – A simple poll can lead to deeper discussions, as people explain their choices and debate different viewpoints.
5️⃣ Anonymous & Inclusive Participation – Users who may not feel comfortable posting long replies can still express their opinions through a simple vote.
6️⃣ Reduces Spam and Off-Topic Comments – Since users can express their stance with a single click, it minimizes unnecessary or repetitive replies.
7️⃣ Saves Time – Polls provide a structured way to gauge opinions without requiring lengthy explanations from each participant.
8️⃣ Visual Representation of Opinions – Polls often include percentages, making it easier to grasp public sentiment at a glance.
9️⃣ Increases Objectivity – A poll prevents heated arguments and emotional bias by focusing on collective results rather than individual opinions.
🔟 Easy to Set Up and Moderate – Compared to open-ended discussions, polls are simple to create, monitor, and analyze.

Mithali 4:13
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake...
😂😂😂😂
 
Hatujui yatakayojiri 2040.
Yesu akirudi kabla ya mwaka huo uko tayari kunyakuliwa? Kama bado, tubu dhambi zako sasa na umwamini Yesu, usije ukaachwa. Baada ya Yesu kuja na kuwachukua watakatifu, watakaoachwa duniani wataingia katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Kwenye io dhiki itabidi wayatoe maisha yao KRISTO, ndio wataungana tena na walionyakuliwa.
 
Kwenye io dhiki itabidi wayatoe maisha yao KRISTO, ndio wataungana tena na walionyakuliwa.
Haitakuwa rahisi kihivyo. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza kuwa mapigo watakayoyapata yatakuwa mazito sana, lakini ajabu watu badala ya kuutubia uovu wao watazidi kumtukana Mungu!
 
Kwakuwa Hujasema Anakuja Wapi Nimekupa Kura ya Ndiyo
1 Wathesalonike 4:16 (SRUV)
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

Kwa Andiko hilo ni wazi atakuja duniani, lakini this time, hatakanyaga ardhini, badala yake ataishia mawinguni. Kufumba na kufumbua, waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kujiunga na wale watakaokuwa hai, kisha sote tutanyakuliwa na Yesu kwenda kwenye Arusi ya Mwanakondoo🙂

Wewe unafikiri atakuja wapi, Israeli?
 
Kwani Mbinguni Ni Wapi Ni mawinguni Au ni wapi?
Na Tukidhamlaki Tunaenda wapi??
Na Hilo Andiko la Kutokanyaga Ardhini umelipata wapi?

KULAKI maana Yake ni Kumpokea Yaani kama Nikienda Kumpokea Mgeni kama Rais akija kwangu Kinachofuata ni Kuleta Kwako..

Kwahyo baada ya kumlaki Itakuaje tena arudi alikotoka?

Na Kingine Baada ya Kunyakuliwa (Kuvutwa) kwenda Mawinguni Nini Kinafuata
 
Tahadhari tu. Kipindi hiki kina mashahidi wengi wa uongo na ushetani mwingi. Take care kujiingiza kupiga kura katika vitu ambavyo hujui msingi wake
 
Haitakuwa rahisi kihivyo. Kitabu cha Ufunuo kinaeleza kuwa mapigo watakayoyapata yatakuwa mazito sana, lakini ajabu watu badala ya kuutubia uovu wao watazidi kumtukana Mungu!
Najua
Ila ukiisoma vizuri hicho kitabu pameelezea kuna watu baadhi watashinda.
 
Najua
Ila ukiisoma vizuri hicho kitabu pameelezea kuna watu baadhi watashinda.
Ni sawa. Hiyo itakuwa kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!
Halafu tena, issue kubwa ni hii, mtu anaweza akaiaga dunia kabla ya kuja kwa Yesu. Akiondoka katika hali ya dhambi, hapo hakuna tena uwezekano wa kutubu.
Ndio sababu tunambiwa "wakati uliokubalika ni sasa na siku ya wokovu ndio sasa."
 
2040
Mnaweza msitoboe hapa duniani.
mkuu nimekuwa nikiwaza sana jambo hili... naona kama hatuko mbali sana na ujio wa bwana.....nimesikia kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
 
kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
Ni kweli. Wako kwenye maandalizi. Kilichokuwa kinasubiriwa ni kupata ng'ombe wekunde wasio na doa kabisa.
The red heifer (Hebrew: פָּרָה אֲדֻמָּה,) was a reddish brown cow sacrificed by Temple priests as a purification ritual in biblical times.
Tayari ng'ombe hao wameishapatikana. Search youtube utaona video nyingi za habari za kupatikana kwa ng'ombe hao. Hizi zote ni ishara za kuja kwa Yesu, ila watu wanapuuza tu.
 
mkuu nimekuwa nikiwaza sana jambo hili... naona kama hatuko mbali sana na ujio wa bwana.....nimesikia kuwa wayahudi hivi karibuni wanataka kuanza kujenga hekalu la tatu..... sijui ni kweli...????
Sijafatilia ila kuna dalili za kuja kwake na dalili ya juja kwake, hapo kwenye za , zimeshatimia , naona imebaki moja ya .....
Chukio la uharibifu.
 
Tahadhari tu. Kipindi hiki kina mashahidi wengi wa uongo na ushetani mwingi. Take care kujiingiza kupiga kura katika vitu ambavyo hujui msingi wake
Wewe ni mgeni JamiiForums? Polls ni kitu cha kawaida kwenye forums na social media zote. Polls zina faida kubwa sana ila members wengi humu hawajajua jinsi ya kuzitumia.

Maelezo ya kupiga kura si yote yameandikwa?

Kinachokuogopesha ni nini?
 
Mimi ni kikongwe humu. Sijaogopa. nachukua tahadhari kwa mambo haya kiroho zaidi.
 
Katika Ufunuo 22:12 Yesu anasema: “Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda."

Swali: Je, unaamini kuwa Yesu yuaja upesi kama alivyoahidi katika Maandiko hayo?
Jibu NDIYO au HAPANA

Maelezo ya Upigaji Kura:
  • Huruhusiwi kubadili jibu lako ukishapiga kura
  • Kura hii ni ya wazi hivyo idadi ya kura/matokeo yataonyeshwa publicly
  • Lakini usipopiga kura hutaweza kuona matokeo!
  • Zoezi la kupiga kura litafungwa baada ya siku 10 tu
=============
Kama unaamini kuwa Yesu yuaja upesi tafadhali piga kura yako ya NDIYO, usimuonee Yesu aibu na maneno yake. Luka 9:26
"Mtu yeyote akinionea aibu mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu naye atamwonea aibu atakapokuja katika utukufu wake na katika utukufu wa Baba, pamoja na malaika watakatifu."

Kama huamini kuwa Yesu yuaja upesi, uwe mkweli tu, piga kura ya HAPANA
Atakuja kama jinsi mwizi ajavyo, "ghafla"
 
Sijafatilia ila kuna dalili za kuja kwake na dalili ya juja kwake, hapo kwenye za , zimeshatimia , naona imebaki moja ya .....
Chukio la uharibifu.
Tunamsubiria yule mnyama wa ufunuo(the beast)
 
Back
Top Bottom