Tafadhali TANAPA angalieni hali ya vyoo vya umma Serengeti na Ngorongoro Crater

Tafadhali TANAPA angalieni hali ya vyoo vya umma Serengeti na Ngorongoro Crater

Hichi ndicho mgeni anakutana nacho pale anapotaka kuoga au kutumia public toilet kwenye campsite, ni tatizo kubwa kwa image ya nchi yetu,,,, Bar wanawezakuweka mtu wa usafi chooni ila Tanapa na Ngorongoro mnashindwa kweli au mko busy na mambo mengine?
Hili ndilo tatizo la Tanzania na sehemu nyingi za Afrika. Utamaduni wa kuwekeza kwenye usafi wa choo haupo. Najua hata sehemu za Asia utamaduni huo haupo. Lakini Latin Amerika na China, hawatofautishi usafi wa sahani ya chakula na sahani ya chooni! Lakini kwa Tanapa ambao wamesomea kazi zao ni uzembe usio kifani kuacha vyoo kwenye hali hiyo!
 
Aisee bafu zuri lakin halifanyiwi usafi,kitu kisipotunzwa lazima kiharibike ,halaf waache kuweka milango ya mbao bafuni ,wapige dawa hapo kinabadilika na kuwa cheupee peee wabongo usafi zeroo
 
Hichi ndicho mgeni anakutana nacho pale anapotaka kuoga au kutumia public toilet kwenye campsite, ni tatizo kubwa kwa image ya nchi yetu,,,, Bar wanawezakuweka mtu wa usafi chooni ila Tanapa na Ngorongoro mnashindwa kweli au mko busy na mambo mengine?
Watu wa mikoani swala la usafi ni zero bora ukae Tanagale lakini iwe Dar
 
Inawezekana Royal Tour phase 2 inaelezea uchafu na mende sehemu ya kivutio cha utalii
 
Kama kusema ukweli ni dhambi basi nimetenda dhambi

Katika vitu sisi waswahili tuko kushoto ni choo. Nenda hata kwenye bonge ya ofisi ili miradi iko chini ya utawala wa waswahili, utakuta watu wamepiga suti za hatari na vitambi vyao, ingia chooni sasa, hapo ndio utajua ujinga wetu ulipo. Usishangae kukuta choo hakina maji, wala toilet paper, na ina vinyesi vya kumwaga. Utashangaa boss anaingia humo huko na akitoka kukata gogo anapeana mikono na watu!

Zunguka kwenye hotel hapa mjini au nje ya Dar, unakuta choo kimejaa vinyesi na nzi kibao, ukikosea ukaingia mdomo ukiwa wazi, usishangae bonge la nzi kuingia kinywani.

Hicho kinachoendelea huko mbugani kwenye public toilet, ndio reflection ya akili ya maafisa waliokabidhiwa hizo mbuga kuzisimamia. Cha ajabu sasa maafisa wa afya wakienda kwenye hoteli binafsi wakikuta hali hata kidogo ya hiyo, watakula bonge la penalti, au hata kufungiwa.
 
Back
Top Bottom